Baba mzazi wa Askari Polisi anayedaiwa kujinyonga Mtwara adai kutoridhishwa na taarifa ya mwanae kujiua

Kama alitumwa kuuwa na akakubali huo ni upumbavu wake.
Kwani angegoma angefukuzwa Kazi?
Ndiyo yaleyale ya Urio aka homeboy. Amri za kijeshi huwaga hazina maswali.wewe unatekeleza tuu amri ya bosi. kawaulize wale askari wa Hai,chini ya SABAYA.ambao leo hii unamsikia Sabaya pekee yake anahangaika na mikesi.Hata makonda wale askari walioingia clouds huwezi wapata.ila makonda unaweza mpata.


Huyo alikuwa shahidi mhimu angeeleza jinsi alivyotekeleza amri ya mkubwa wake
 
Huyo Sadi yupo wapi.
Maana wa Mahenge waliapa kulipiza kisasi kwa majambazi hao
 
CHAI CHAI
 
Yupo bize na vi Birthday na kupigia simu akina Mwijaku,. Ameshaingia kwenye Mtego wa kusifiwa na kuabudiwa
 
Hapo jaji awape kesi mbili za mauaji.
Moja ya mfanyabiashara mbili ya jambazi mwenzao. Kesi ya tatu uporaji. Jumla ya miaka 90 KILA mmoja inawatosha
 
Dah hii

Dah hizi kazi za haya majeshi hazifai bas kabisa..
Bora nikamwage pili pili zangu hoho barbrn,
Kazi ni kutumwa kuua mtu asokua na hatia na hutakiwi kukataa
Ila hatia,laana,kuwindwa na ndugu kimwili na kiroho shughuli unabakia nayo wewe muuaji. Waliokutuma wanachoma nyama. Hapa ni za kuambiwa
 
Ccm na police wanalindana kuwapora wananchi kwa common interests za kulindana.
Mmoja anapora kura zetu mwingine anapora pesa zetu. Ndo maana ma police wanauchikia Sana upinzani.
 
Lakini hata kesi ya Zombe na wenzake baada ya tume kuundwa na kutoa majibu kuhusu ukweli, tatizo likaja kwenye uandishi wa mashitaka!

Mtu wa taaluma hiyo alipokwisha kulambishwa mlungula akajifanya mamuma wa taaluma, akaandika kesi miguu juu kichwa chini, hali iliyofanya Zombe akaonekana ni muungwana, afisa mpole na hajashiriki kabisa kwenye mauaji hayo na kuachiwa huru kula pensheni na hewa tulivu ya uraiani!

Na hata sasa nasikia harufu ya mambo hayo kujirudia ingawa Makamo kafoka sana hadi povu limemtoka kumshurutisha Igp aingilie kadhia ya mauaji yanayoendelea kote nchini, lakini mwisho wa jambo hili tusitarajie lolote la maana.
 
Kama kundi zima la watuhumiwa walikuwa wameswendekwa ndani, ni nani aliyeshawishi na kusimamia mauwaji ya polisi mtuhumiwa mwenzao aliyefia mahabusu?

Hii cyndicate inamgusa moja kwa moja Rpc na viongozi wengine wakubwa wa polisi mkoa kama Rco!

Hawa watu wakiwekwa pembeni ama nao kuunganishwa katika tuhuma itasaidia kuupata ukweli wa jinsi mnyororo wa wauwaji ulivyokuwa umejipanga na kutekeleza uovu huo.

Kuwaacha hawa watu muhimu kuendelea kuvaa magwanda ya polisi na kukalia viti vya nyadhifa zao watasaidia kupotosha na kupoteza uelekeo wa kupata ukweli wa jambo hili haraka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…