Baba yangu hakuniachia urithi lakini ndugu zangu wengine wamepewa wote, je nikijitenga na ile familia nakosea?

Ilikuwa kabla mama alipomweleza akaishia kutukanwa matusi yote ngumi na mateke nakujibiwa kuwa sina mali za kumpa nishagawa tena kwa hasira inamaana kwamba mm ni mbwa nawala sistahili
Wewe sio mbwa ww ni mtoto wa nje ya ndoa
Fullstop acha kulialia tafuta mali zako,au nenda kwa baba'ko wa halali akugawie mali zake.
 
Pole for the trauma,

Talk more about this, inaweza sababisha stress saana hii
 
Kuna kitu baba alikigundua mapema sema tu wazee wa zamani hawapendi kuweka Mambo Yao hadharani.
 
Alinambia baba alikuwa katili sana kila alichomshauri aliishia kupigwa
Hadi hapa wewe sio wake. Mwambie mama yako akuoneshe baba yako halisi ukapate urithi wako huko
 
Wewe sio mbwa ww ni mtoto wa nje ya ndoa
Fullstop acha kulialia tafuta mali zako,au nenda kwa baba'ko wa halali akugawie mali zake.
Ndugu yangu mimi wacha nikae mbali na ile familia naanza kuiondoa akilini haiwezekani wakanitenda hivi
 
Unadhani hao waliopewa urithi walishiriki wakati marehemu alipokuwa akitoa na kuandika mirathi? kama hawakushiriki, kwanini chuki uiamishe kutoka kwa muhusika ( baba yako) uipeleke kwa ndugu zako?
Kama umeamua kumchukia mto mirathi usiwachukie waliopewa, kama hawakushiriki wakati mzee alipokuwa akiandika hiyo karatasi ya mirathi.
 
Unalilia urithi kwa mzee?

Wakati mzee ananigaia baadhi ya Mali zake nilikataa nikamwambia awape wadogo zangu kwa kuwa nina vyangu vya kutosha

Jifunze. Tafuta za kwako
Hata mimi mzee wangu alitaka kunigawia kiwanja nijenge nilikataa nikaanza mwenyewe from scratch.
Mali ya kurithi sio ya kuitegemea ukipewa ni sawa na usipopewa ni sawa maana aliyepambana kuitafuta ndio mwamuzi,cha msingi ni kupambana kutafuta zako kwa nguvu zote.
 
Ushauri wa busara sana huu,mtoa mada atulize kichwa na kutafakari
 
Wewe ni mtoto wa nnje ya ndoa unafikiri huyo mzee ni hajui?

Kumbuka amekulea tangu ukiwa mtoto kwhy anakujua zaidi ya ww unavyojijua.

Halafu kumbuka wazee wetu wanasemaga "kuchapiwa ni siri ya ndani"
Kiukweli kama ni kweli ni mtoto wa nje kwanza ashukuru kulelewa na kuwa mkubwa wazee wa zamani walikuwa wastaarabu sana kama ni hawa vijana wa sasa anakinukisha mapema sana.
 
Ulitupwa nje na baba'ko siyo familia yako.
 
Pole sana. Kiungwana ilipaswa hao ndugu wanne wazungumze jambo kuhusu wewe. Ila inaonekana ni wabinafsi ndio maana umefikia huku. Anyway, pambana ndugu. Usiwategemee kwa chochote. Utatoboa
 

Mama yako ana jibu. Kuna issue mbili hapo, ya kwanza, marehemu siyo baba yako, pili, will iliqndikwa kabla ya wewe kutungwa mimba au kuzaliwa.
 
Baba yako akuzae ,akuchagulie Mama,akuchagulie ndugu wako wa karibu ,akusomeshe ,akupe jina unalotumia hadi sasa.

Hata huu uwezo ulikuja hapa kuandika ,kumdhalilisha humu ,umekupa yeye,akili amekugaia

Bado huoni ni urithi tosha ,

Acha malalamiko ,Dunia iko wazi sana ikufanye nawewe utafute zakoo.

Ni aibu Sanaa na unataibisha wanaume

Umetukosea Sanaa, unamdhalilisha sana baba yakoo.

Nakuambia utateseka Sanaa, njia pekee rudi kamuombe radhi baba yako kwa hichi ulichokufanya hapo njia zako zitafunguka .

Ushauri tuuu Mkuu ,najua utachukulia kichanyaa.
 
Hana lolote alikuwa mshenzi kama wengine
Mkuu kwa majibu kama haya acha unyimwe urithi,umeshaambiwa huko juu na wadau inawezekana wewe siyo mtoto wa huyo mzee ongea vizuri na Mama anajua ukweli..
 
Mimi ni mtu ambaye kwenye familia ndiye niliyeonewa nimewekwa fungu la kukosa haya nayolalamikia nikweli nimetendewa ndugu yangu unazaliwa familia ambayo wao ndio wanastahili mimi sistahili
Ni kweli inauma!

Jitahidi kubadilisha akili yako kuhusu jambo hilo.
Tafuta mali yako, utakuwa huru zaidi! mara nyingi mali za kurithi huwa ni kama zunamfanya mtu kubweteka, akili inakoma katika utafutaji.

I swear, jipe muda wa kutafuta, utakuwa mbali zaidi ya hao walio achiwa mali!.
 
Hana lolote alikuwa mshenzi kama wengine
Yaani inasikitisha kuwa:
Umeona hilo karatasi ukapata mawazo
Ukajiuliza mwenyewe
Ukajijibu mwenyewe
Umeshaamua uamuzi ujitenge
Maana yake umeichukia familia nzima hata wasio husika.
Hukutakq kulijua vizuri jambo hilo na umeshafikiri vibaya na una chuki already!!!
Halafu ghafla tu umeamini mamemo ya mother ako bila kuyatafakari vizuri ati mzee alikuwa katili!! Kama alikuwa katili mbona amegawa urithi kwa wengine!! Mama yako amekwepa hoja kakutwika kitu kingine ili kupotezea.
Uliza vizuri wakubwa na hasa huyo mama yako kuwa kwanini wewe hukuwekwa,au uliza kaka mkubwa.Baba km yupo unaweza kutafuta muda kuongea nsye lkn yote hayo yafanyike kwa nidhamu na heshima kubwa,utapata jibu tu.Ukiendq kwa mikwqla umeharibu.
Mwisho km ushauri huu haufai na umeamua kweli kuondoka,basi wakusanye familia yenu waage kwa upendo kabisa ukiwaeleza hiyo sababu.Litakaa vizuri tu na hata ukienda bado upendo na nduguzo utakuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…