S.M.P2503
JF-Expert Member
- Nov 25, 2008
- 2,421
- 4,344
Asante mkuu, lakini hata kama ni za kwao, ingefaa sasa kila kijiji cha nchi hii kifungue shauri la kupinga mambo yote ya ajabu ajabu humu nchini- ni suala la uratibu tu na malipo kwa wanasheria ndio issue.Umejenga hoja vyema sana mkuu.
Lakini msingi wa swali ni kuwa mahakama na tume ni za kwao, kutegemea matokeo kuwa kwa upande wetu sisi wafuata taratibu inakua ngumu sana.
Majaji wapewe kazi ya zaida zaidi toka kila kijiji cha nchi hii. Wakichoka kusilikiza mashauri ya namna hii ndipo waatanza kutenda haki. yaanai kesi za kupinga kila corner kijiji.
Ningefurahi sana iwapo CDM wangeweka katika kila kijiji/kata/ tarafa mwanasheria wa kufungua kesi mbali mbali nyingi sana, hadi majaji wachoke na waanze kutenda haki. Hapa ndipo tulipo kwama maana hawa majaji wakipewa kashi kashi, hakutakuwa tena na delaying techinics. Ningependa sana mwanasheria ajaye wa CDM aanze na mpango huu kabla ya October. yaana ni kesi kwenda mbele hadi wachoke wenyewe na watoe kile wananchi wanachi taka- haki tupu. wakichelewa kutenda haki, kesi zitarundikana na wataoneka ni kauzi na watu kuwaambia kama wamechoka kazi waache. ifike mahali mahakama zifanye kazi 24/7 hadi weekend, wanasheria wapo wa kutosha, hakuna haja ya kukalia kesi wakati watu wa kufanya kazi hizo wapo.
sijui ni kwa nini kupata haki humu nchini ni kazi kama kutafuta kazi?