Samia kakaripia watu kuanza kampeni kabla ya wakati, halafu yeye kaenda kuanza kampeni bila kufuata wakati.
Kikao kimevunja katiba ya CCM ya 1977, tileo la Disemba 2022, 8bara ya 100, kifungu cha 5 c.
Kama kuna watu wanataka kupinga jambo hili, wanaweza.
Mkuu Watu hawajasoma Katiba ya CCM 1977 toleo 2022.
Kuna ukiukwaji wa Katiba. Tuangalie kwa uchache
Tuanze na Fungu VII Vikao vya Taifa.
Fungu VII 99 (4) Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa (Zanzibar).
Fungu VII, 110 (7)(b) Kamati Maalumu itapendekeza majina KWA Kamati kuu CCM kwa Wanachama wanaoomba kuteuliwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Ubunge
Hoja: Wanachama waliotaka kuomba nafasi wamenyimwa haki yao kikatiba hakuna mchakato uliopendekeza majina na kuchujwa na Kamati kuu ya CCM Taifa. Jina la H.A Mwinyi lilipatikanaje?
Kamati Kuu ya CCM.
Fungu VII M 104 (1)(7)(b) Kamati Kuu itapendekeza kwa Halmashauri kuu majina
yasiyozidi matano ya Wanaoomba kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano.
Fungu VII ,104 (1)(7)(d) kufikiria na kupendekeza majina yasiyozidi
matatu ya Wanachama wanaotaka kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar
Hoja: Nafasi ya majina 5 au 3 ingepatikanaje ikiwa hakukuwa na uombaji na mchakato ?
Halmashauri kuu
Fungu VII, 103(12) (b na c) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa Taifa majina
yasiyozidi matatu kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano , na
jina mmoja kwa nafasi ya Rais wa
Zanzibar
Hoja: Halmashuri kuu haikufanya kazi kwasababu haikupokea majina kutoka Kamati kuu.
Wanachama waliotakiwa kuwa 5 Kamati kuu kisha 3 Halamshauri kuu kwa Jmahuri ya Muungano, na Wanachama 3 Kamati maalum Zanzibar kisha jina moja Kamati kuu hawakupewa nafasi.
Mkutano Mkuu
Fungu VII, 101 (5)(c)
Kuchagua jina moja kwa atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.
Hoja: Jina moja kutoka matatu yaliyopendekezwa na Halmashuri Kuu kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano.
Kwa Upande wa Zanzibar, katiba haijasema chochote. Maana yake Halamshauri kuu ndio kikao cha mwisho cha uteuzi wa Rais wa Zanzibar. Mwinyi alithibitishwaje Dodoma?
Rais Mstaafu Kikwete anasema, limeshatoka azimio la Mkutano Mkuu, akina ''Emanuel' kwa maana ya KM wa CCM waangalie taratibu za kisheria. Katiba ya CCM inakataa .
Fungu VII, 101 (7) linatoa Uhuru wa Mkutano Mkuu Kukasimu shughuli zake kwa Halamshauri kuu ya CCM
isipokuwa kifungu (c) kinachokataza Mkutano Mkuu kukasimu madaraka ya
uteuzi wa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano, na (d)Kuthibitisha mgombea Urais wa Zanzibar.
Rais Mstaafu anatueleza, CCM imeweka mkokoteni mbele ya Farasi halafu zitafutwe njia za kuhalalisha hilo
Yote haya yapo wazi kwenye Katiba ya CCM, Watu wasome waje tujadiliane kama kuna makosa ya tafsiri
JokaKuu