Bado kuna Fukuto la kwanini Samia hajapitishwa kwenye Chujio !!!

Ni shida
 
Mkuu Watu hawajasoma Katiba ya CCM 1977 toleo 2022.
Kuna ukiukwaji wa Katiba. Tuangalie kwa uchache

Tuanze na Fungu VII Vikao vya Taifa.
Fungu VII 99 (4) Kamati maalumu ya Halmashauri kuu ya CCM Taifa (Zanzibar).

Fungu VII, 110 (7)(b) Kamati Maalumu itapendekeza majina KWA Kamati kuu CCM kwa Wanachama wanaoomba kuteuliwa nafasi ya Urais, Uwakilishi na Ubunge

Hoja: Wanachama waliotaka kuomba nafasi wamenyimwa haki yao kikatiba hakuna mchakato uliopendekeza majina na kuchujwa na Kamati kuu ya CCM Taifa. Jina la H.A Mwinyi lilipatikanaje?

Kamati Kuu ya CCM.
Fungu VII M 104 (1)(7)(b) Kamati Kuu itapendekeza kwa Halmashauri kuu majina yasiyozidi matano ya Wanaoomba kugombea kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano.
Fungu VII ,104 (1)(7)(d) kufikiria na kupendekeza majina yasiyozidi matatu ya Wanachama wanaotaka kugombea kiti cha Rais wa Zanzibar

Hoja: Nafasi ya majina 5 au 3 ingepatikanaje ikiwa hakukuwa na uombaji na mchakato ?

Halmashauri kuu
Fungu VII, 103(12) (b na c) Kupendekeza kwa Mkutano Mkuu wa Taifa majina yasiyozidi matatu kwa nafasi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano , na jina mmoja kwa nafasi ya Rais wa Zanzibar

Hoja: Halmashuri kuu haikufanya kazi kwasababu haikupokea majina kutoka Kamati kuu.

Wanachama waliotakiwa kuwa 5 Kamati kuu kisha 3 Halamshauri kuu kwa Jmahuri ya Muungano, na Wanachama 3 Kamati maalum Zanzibar kisha jina moja Kamati kuu hawakupewa nafasi.

Mkutano Mkuu
Fungu VII, 101 (5)(c) Kuchagua jina moja kwa atakayesimama katika uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.

Hoja: Jina moja kutoka matatu yaliyopendekezwa na Halmashuri Kuu kwa Urais wa Jamhuri ya Muungano.
Kwa Upande wa Zanzibar, katiba haijasema chochote. Maana yake Halamshauri kuu ndio kikao cha mwisho cha uteuzi wa Rais wa Zanzibar. Mwinyi alithibitishwaje Dodoma?

Rais Mstaafu Kikwete anasema, limeshatoka azimio la Mkutano Mkuu, akina ''Emanuel' kwa maana ya KM wa CCM waangalie taratibu za kisheria. Katiba ya CCM inakataa .

Fungu VII, 101 (7) linatoa Uhuru wa Mkutano Mkuu Kukasimu shughuli zake kwa Halamshauri kuu ya CCM isipokuwa kifungu (c) kinachokataza Mkutano Mkuu kukasimu madaraka ya uteuzi wa mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano, na (d)Kuthibitisha mgombea Urais wa Zanzibar.

Rais Mstaafu anatueleza, CCM imeweka mkokoteni mbele ya Farasi halafu zitafutwe njia za kuhalalisha hilo

Yote haya yapo wazi kwenye Katiba ya CCM, Watu wasome waje tujadiliane kama kuna makosa ya tafsiri

JokaKuu
 
Wakala nae ni binadamu. Unategemea gaidi mbowe ale pesa yote, mawakala hawalipwi, nani atakaa. Mbowe ameshindwa kupata support kutetea kiti kwa sababu hicho chama hela inabaki tu juu, haishuki chini. Mashinani kumepauka, njaa kali. Huwezi kukuza chama. CCm angalau wana vimradi mikoani, nyumba, fremu za maduka, shule, hospitali, viwanja vya mpira. Kila kitu mwisho wake ni maslahi
 
2020 kuna watu walivuruga uchaguzi maksudi wakasahau kwamba ajuaye kesho leo hii ni mwaka wa nne hawapo duniani vyote wameviacha

Huwezi shiba fedha ukipenda fedha kupita kiasi utadhalilisha utu wako
Watu wenye akili wanapigania wawe na legacy zuri lakini hii ni tofauti na jk mtu mzima hovyo
 
Mnyonyanyi mkubwa kwa ss ni ex president ndio maana wakati wa jiwe alikua kmy sn alibanwa sawa sawa ila kwa sasa yuko close na chura kiziwi ndio maana anatumia effort kubwa kumpambania ili aendelee kuwa kwny system
 
Maswala ya ugaidi wa mbowe yanatoka wapi kwenye uzi
Kama mbowe ni gaidi na yupo uraiani basi tuna-inch ya hovyo sana
 
Kikwete ameharibu sana utaratibu, na ametia doa urais wa Samia hata kama atakuja kushinda.

Kwa sababu watu wataangalia mchakato mzima wa Samia alivyokuwa rais, na kuona matatizo haya ya kikatiba.

Na zaidi, wameacha mwanya wa Samia kuwekewa pingamizi.
 
Ila hili taifa tunakwama sana huyu mama pamoja na underperformance hii lkn bado tunampa nafasi ya kuliongoza tena taifa. Wenzetu wa Malawi yule mama baada ya kuupata urais ndondokela kama huyu wa kwetu na akaperform chini ya kiwango uchaguzi uliofuata watu walipiga chini hawakuangalia usoni ila sisi sasa dah
 
Kikwete ameharibu sana utaratibu, na ametia doa urais wa Samia hata kama atakuja kushinda.
Hata ndani ya CCM wanasema wazi kilichofanyika hakikuwa sahihi. Nadhani walitaka kukwepa ushindani wa majina 5 kisha 3. Nashangaa wanaogopa nini? Kuna wakati alikuwepo Msuya, JK, na Mkapa!
Tuliona ushindani mkubwa sana! Hata wakati wa Magufuli. Nini kinaogopwa!
Kwa sababu watu wataangalia mchakato mzima wa Samia alivyokuwa rais, na kuona matatizo haya ya kikatiba.
Mchakato mzima umekosa uhalali hata kwa wasiojua sheria. Ukisoma katiba tu unajua kuna tatizo
Na zaidi, wameacha mwanya wa Samia kuwekewa pingamizi.
Nakuhakikishia ingelikuwa ni CDM au ACT leo Msajili wa Vyama ungemsikia kwa kila neno.
Kungekuwa na pingamizi kubwa mbele ya safari.

Ninasubiri kuona mazingaombwe ya kukwepa kikwazo hicho. Katiba ya CCM ipo wazi kabisa, Mgombea anaanza kupatika kwa vikao gani halafu ikasisitiza, Mkutano Mkuu hauwezi kukasimu shughuli za uteuzi kwa H/Kuu . JK anapata wapi nguvu za kusema '' warekebishe'' kisheria!

JokaKuu Pascal Mayalla
 
Underperformance gani so far aliyofanya. Kitu gani hakiendi. Shida ni nyie taliana mnaaminishana kuwa ndio kila kitu
 
Unajua nchi za wazungu viongozi baada ya kustaafu hasa maraisi walio save maximum terms. Na viongozi wengine wakuu wa idara nyeti ambao hawawezi tena kuwa viongozi (senior serikali au kwenye vyama) wanapewa power withdraw therapy pamoja na watoto ambao washazoea ulinzi how to be civilians.

Tanzania hatuna utaratibu huo, from 2016 wengine tumekuwa tunasema issue ya JK ni psychology ya kudhani bado ni mtu influential na kupambania kubaki relevant kwenye decision making za nchi (ni mental issue),

Kwa nafasi yake alikuwa na mamlaka gani ya kupitisha azomio la Dodoma, kwa nafasi gani aliyonayo CCM leo.

JK ni mental case, sema Tanzania atuelewi tu. Kilichotokea Dodoma hana mamlaka ya kichama wala serikali kuyaidhinisha yaliyofanyika Dodoma ni wazimu wake tu.
 
Kwamba ni mpango wa JK

Alihusishwa toka mwanzo, ingawa alijifanya ameshitushiwa pale.

Kwa jinsi Maza alivyojipanga kuitetea hiyo nafasi sitashangaa watu wakifa safari hii kwa sababu ya Urais. Anawekeza nguvu na mali nyingi.
 
CCM wanaogopa Samia kuchaguliwa na wanaCCM wenzake kuwa mgombea ila wana guts za kusema watashinda uchaguzi mkuu kwa kupitia mgombea ambaye hata chamani kapitishwa nyuma ya pazia. Kazi ipo.
 
Tanzania ma ex presidents wana tabia hii tangu Nyerere. Ambaye hakufanya mchezo huu ni Mwinyi tu. Tofauti hawakufanya wazi hivi.

Nyerere alimkata Kikwete kwa kubadilisha sheria za mchezo katikati ya mchezo.

Mkapa alitulazimishia Magufuli despite recommendations za security organs.

Kikwete ndiye huyu sasa.

Wamerithishana uhuni wa kujiona kingmakers.
 
Hata ndani ya CCM wanasema wazi kilichofanyika hakikuwa sahihi.

JokaKuu Pascal Mayalla
Its true hakikuwa sahihi, nimemwandikia barua Dada kumshauri hili lirekebishwe Dada Mkubwa tunakupenda na tunakukubali, kama ni wewe, ni wewe tu, hakuna mwingine! Usiruhusu uhuni huu, fuata Katiba na the due process, utabarikiwa

Mpanga wa awali ulikuwa ni CCM kutoa fomu moja na kupitishwa kwa mserereko, kwenye barua yako hiyo nimemweleza Dada hata huo mserereko ni kinyume cha katiba ya CCM na ya JMT.
P
 
Ni kweli kabisa ! πŸ˜…
Lakini je huoni kwamba hii yote ya sasa and and the worse to come inasababishwa na itaendelea kusababishwa na madaraka makubwa kupita maelezo aliyonayo mtu mkubwa kupita wote Nchini ??!
Ambaye sio kwamba eti labda anavunja Katiba ! Bali tu Katiba haijamzuwia kufanya lile analotaka kulifanya japo wengine mnaona kwamba sio sahihi !!
Je ni mikanganyiko kwenye Katiba sasa unajidhihirisha zaidi hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote ???!

Je watu waendelee kutoona u muhimu wa Katiba mpya kwa sababu zile zile za kuulinda utawala wetu wa Chama Chetu ???!!
Hilo swali ni swali fikirishi !

Na Mimi naendelea kusema watu wataendelea kuogopa kutoa misimamo yao huko Chamani kwa sababu wanajua kwamba itakuwa ni kujipalia mkaa πŸ™„!
Locuta causa finita ! πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘πŸ™
 
Lakini Katiba haijawakataza kufanya yale wayafanyayo ! Right ?
Je tatizo lipo kwa hao wakubwa au lipo kwa sababu Katiba haijazuwia watu kujifanya ma-King makers ??!
 
Kama kweli wapo wana CCM waliochukia tuwaone nao wakiipigania Katiba mpya ipatikane ambayo itapunguza madaraka makubwa kweri kweri aliyopewa Mkuu wa Nchi ambaye huyo huyo ndiye Mkuu wao wa Chama πŸ˜³πŸ˜³πŸ™„!
Je watakuwa na ubavu huo ???!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…