GE2025 Balozi Polepole: Rais Samia anahujumiwa, kazungukwa na Wana Mtandao (Kikwete na Rostam)

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Ujasiri wa kuachia ubalozi na kuamua kuongea mambo haya sinwa kawaida. Inafikirisha
Ujasiri unaotokana na uwepo wa kundi linalogharamia maisha yake nje ya yale manufaa ya ubalozi.

Hicho ni kipaza sauti cha watu fulani waliokaa sehemu fulani wakiangalia yatakayotokea. CCM ipo madarakani tangu 1977 wakati huo pengine Pole Pole alikuwa akinyonya ziwa la mama yake huko kijijini.
 
Naam, huyu ni kivuli tu
 
Mmoja kashajitokeza tayari.Amesema Polepole siyo kada wa CCM
 
Aiseee alisema hivyo !? Yaani anadhihirisha kabisa kuwa Yuko under influence
 
Akiendelea kurudiarudia hii mada atapoteza ushawishi. Hili la kusema wanaomzunga wanaomzunguka kila siku inakuwa hamna jipya.

1. Watekaji ni kina nani

2. Nani alimuua mjomba wa chato

3. Kwanini Mpango na Majaliwa wamestep down?
Kama hapo kwa kutulia, hadi kufika 78% ya presentation ya HP maswali yako yatakuwa yamejibiwa.
 
Utabiri wa marehemu shekhe Yahya unasema Rais mwanamke atatawala muhula mmoja tu au wanaweza kumwacha aingie tena lakini wakafanya yao kisha makamu akawa Rais au pia wanaweza kumwekea shinikizo abadili mawazo wamwengue na mchakato uanze upya
Kwa maelezo ya Polepole,Nchimbi ni mwanamtandao.Kwa hiyo,inawezekana kabisa baada ya uchaguzi wanamtandao wakataka kumuweka Mwenzao.Mama akae chonjo.
 
Kuna mwana mtandao mmoja wakati anataka kupitisha mambo yake bila kufuata utaratibu alisema wachawi walishakufa.
 
Kujitokeza kwa Rostam Aziz "kujibu" hoja za Polepole kumenikumbusha jamaa aliyedakwa na begi kubwa la fedha za kuwahonha wajumbe wakati WA kumpotisha mgombea urais Dodoma
 
Ni uzembe wa jamuhuri yetu!haiwezekani jamuhuri inashindwa na mtandao!
 
Kwani hujui bila Kikwete asingetoka Zanzibar kuja hapa? Kama Magufuli alivyokuwa akimshukuru Mkapa wacha na Samia afanye
 
Lissu, mnyika na Lema walisema wanajua ufisadi wa Lowassa lakini wakawa sehemu ya kumpokea kwenye chama na kumsafisha kwenye kampeni je vipi hawa unawaamini?
Aliyemleta Lowassa ni Mbowe ambaye amekuja kubainika kumbe hakuwa mpinzani halisi. Ndiyo maana kwa sasa chama kinasafisha wale wote waliokuwa wanafiki baada ya Mh Lissu kushika uenyekiti.
 
Samia aahirishe kugombea urais,asigombee ili taifa libaki salama.


Mpaka anasema hadharani kwamba boss wake ni kikwete inaonekana Samia hana upeo wa kuona mambo na ku-reason sawa sawa,yupo yupo tu hajui thamani ya kiti alichokikalia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…