Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania, Lucy Lameck. Alikuwa Waziri wa 1 mwanamke wa Tanzania

Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania, Lucy Lameck. Alikuwa Waziri wa 1 mwanamke wa Tanzania

Hioy ndiyo shida na hasara ya kuwa na majina ya Kizungu, fikiria kama huyo Mbongo angeitwa labda Neema Majuto, huo Mtaa ungekuwa na maana zaidi, sasa Mtaa unaitwa Lucy halafu mnasema ni Mtanzania, WTF, ...
Barabarosa ni Mtanzania?

Jinga kabisa.
 
Tanzania hasa Tanga ina historia kubwa sana Ki dunia sema ndio hivyo we are a sleeping Giant

Rais wa Mwisho wa South Africa ya Makaburu alizaliwa Tanga

Malkia Elizabeth alitangazwa kuwa Malkia wa Uingereza baada ya kifo cha Baba yake 1952 akiwa anazuru Ziwa Victoria

Viongozi kadhaa wa Kitaifa wa Ujeruman wamezaliwa Tanganyika

Viongozi kadhaa wa Kiafrica wana historia kubwa sana na Nchi yetu
Mf Watoto wa kwanza wa 3 wa Museven wote wamezaliwa Tanzania

Lakin cha kusikitisha Nchi yetu hasa miaka ya karibuni imejizika kabisa

Kuna Mwaka nilikuwa Nchi moja ya Kusini mwa Jangwa la Sahara sasa tukaingia mitaani tukawa tunafanya shopping huku tunapiga story na wenzangu, yule Muuza Duka akawa interested na lugha yetu akatuuliza lugha gani hii na ya wapi tukamjibu, cha kushangaza eti haijui Tz hadi alipo google akajijibu ooh its Ngorongoro

Publicity yetu tunaifanyia Tandale na Hadi Nyakanazi si zaid ya hapo
We are in the laiti traki. We are dona kantre now.
 
Haitatusaidia, sisi tunataka CCM ipigwe nyundo
CCM imetuletea shida kubwa sana. Wananchi wanatawaliwa bila ridhaa yao ni sawa na kubaka. Tutake tusitake lazima tutawaliwe na watu ambao hawajachaguliwa kwa matakwa ya wananchi waliowengi. Ni bahati mbaya sana kwa kweli!
 
Tanzania hasa Tanga ina historia kubwa sana Ki dunia sema ndio hivyo we are a sleeping Giant

Rais wa Mwisho wa South Africa ya Makaburu alizaliwa Tanga

Malkia Elizabeth alitangazwa kuwa Malkia wa Uingereza baada ya kifo cha Baba yake 1952 akiwa anazuru Ziwa Victoria

Viongozi kadhaa wa Kitaifa wa Ujeruman wamezaliwa Tanganyika

Viongozi kadhaa wa Kiafrica wana historia kubwa sana na Nchi yetu
Mf Watoto wa kwanza wa 3 wa Museven wote wamezaliwa Tanzania

Lakin cha kusikitisha Nchi yetu hasa miaka ya karibuni imejizika kabisa

Kuna Mwaka nilikuwa Nchi moja ya Kusini mwa Jangwa la Sahara sasa tukaingia mitaani tukawa tunafanya shopping huku tunapiga story na wenzangu, yule Muuza Duka akawa interested na lugha yetu akatuuliza lugha gani hii na ya wapi tukamjibu, cha kushangaza eti haijui Tz hadi alipo google akajijibu ooh its Ngorongoro

Publicity yetu tunaifanyia Tandale na Hadi Nyakanazi si zaid ya hapo
Tanga ni mji ambao Wajerumani walipanga ufanane na Bonnie mji wao. Miaka hiyo Tanga ilikua kama Ulaya, Raskazone yalikua makazi yao na jioni walistarehe Yatch Club, Mkonge Hotel, Tanga Hotel, .

Kulikua na kampuni za kuuza magari ya Peugeot , maduka ya Wahindi yalikuwa na mahitaji yote. Ukitaka viatu kutoka London, Rome na hata Bata ya Kenya. Ajira ndiyo usiseme, vijana walipata ajira bandarini, mahotelini. Nk

Muingereza hakuipenda Tanga kwakua ilimkumbusha maisha ya Mjerumani.
 
Mji wa Berlin kuupatia mtaa mmoja jina la Mtanzania

Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani, Berlin, wamepiga kura kukubali kuubadilisha mtaa mmoja wa mji huo kuwa na jina la Mwanaharakati Mwanamke wa Tanzania, kuchukua nafasi ya jina la Mtaa wa Wissmannstraße, ambalo linatokana na jina Hermann von Wissmann aliyekuwa Gavana wa koloni la Afrika Mashariki anayetuhumiwa kuamuru mauaji na mmoja wa Wanaharakati wa Kike wa Uhuru wa Tanzania.

Lucy Lameck mzaliwa wa Kilimanjaro alikuwa Waziri wa kwanza wa Mwanamke wa Baraza la Mawaziri nchini Tanzania na pia kama kiongozi wa harakati za uhuru. Von Wissman alikuwa Gavana wa Afrika Mashariki ya Ujerumani (sasa ni Tanzania, Burundi na Rwanda) mwishoni mwa karne ya 19. Gazeti la Ujerumani la Der Tagesspiegel limeripoti kuwa Gavana huyo anaaminika kuhusika mauaji ya umati ya watu wa eneo hilo.

Kutokana na hali hiyo kulikuwa na kampeni iliyozuia "kuheshimiwa zaidi" kwa Von Wissmann na badala yake kuweka "Mwanamke wa Kitanzania ambaye alipinga kikamilifu ukoloni na ubaguzi wa rangi". Mtaa huo sasa utaitwa Lucy-Lameck-Straße.

Chanzo cha Habari CRI Kiswahili


Lucy Lameck alitoa mchango mkubwa katika kupigania uhuru wa Tanganyika ajabu kubwa hadi hakuna barabara au mtaa uliopewa jina lake.

Wazee wetu wanefifishwa na utawala wa Mwl Nyerere kila kitu kajipachika yeye huku wengine wakiwekwa kando.

Nakala Mohamed Said
 
CCM imetuletea shida kubwa sana. Wananchi wanatawaliwa bila ridhaa yao ni sawa na kubaka. Tutake tusitake lazima tutawaliwe na watu ambao hawajachaguliwa kwa matakwa ya wananchi waliowengi. Ni bahati mbaya sana kwa kweli!
Sure mkuu
 
Tanzania hasa Tanga ina historia kubwa sana Ki dunia sema ndio hivyo we are a sleeping Giant.

Rais wa Mwisho wa South Africa ya Makaburu alizaliwa Tanga.

Malkia Elizabeth alitangazwa kuwa Malkia wa Uingereza baada ya kifo cha Baba yake 1952 akiwa anazuru Ziwa Victoria.

Viongozi kadhaa wa Kitaifa wa Ujeruman wamezaliwa Tanganyika.

Viongozi kadhaa wa Kiafrica wana historia kubwa sana na Nchi yetu. Mf Watoto wa kwanza wa 3 wa Museven wote wamezaliwa Tanzania

Lakin cha kusikitisha Nchi yetu hasa miaka ya karibuni imejizika kabisa.

Kuna Mwaka nilikuwa Nchi moja ya Kusini mwa Jangwa la Sahara sasa tukaingia mitaani tukawa tunafanya shopping huku tunapiga story na wenzangu, yule Muuza Duka akawa interested na lugha yetu akatuuliza lugha gani hii na ya wapi tukamjibu, cha kushangaza eti haijui Tz hadi alipo google akajijibu ooh its Ngorongoro.

Publicity yetu tunaifanyia Tandale na Hadi Nyakanazi si zaid ya hapo.
Umetoa historia nzuri sana mkuu. Nafikiri kuna haja ya wenye dhamana kuwa na strategy nzuri zaidi ya kuitangaza nchi yetu. Lakini pia na sisi mmoja mmoja tunapopata fursa ya kutembea ni lazima tuwe mabalozi wazuri wa nchi yetu.
 
Barabara hiyo inatarajiwa kubadilishwa jina mwaka ujao

Madiwani katika mji mkuu wa Ujerumani , Berlin wamepiga kura ya kuondoa jina la barabara moja linalompatia heshima gavana mmoja wa nyakati za ukoloni katika eneo la Afrika mashariki aliyeshutumiwa kwa kuagiza mauaji na kuweka jina la mmoja wa wanaharakati wa kupigania uhuru nchini Tanzania.

Barabara ya Wissmannstraße, iliopatiwa jina la Hermann von Wissmann, sasa itaitwa Lucy-Lameck-Straße.

Alikuwa waziri wa kwanza mwanamke nchini Tanzania pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi maarufu katika vuguvugu lililopigania uhuru wa taifa hilo.

Lameck alikuwa naibu waziri wa maendeleo ya kijamii na Afya na alifanya kazi kuimarisha nafasi ya mwanamke.

Von Wissman alikuwa gavana wa taifa la Ujerumani Afrika mashariki ambayo kwasasa ndio mataifa ya Tanzania , Burundi na Rwanda katika mwisho wa karne ya 19 na anadaiwa kuwa chanzo cha mauaji ya wakaazi wengi limetangaza gazeti la Ujerumani, Der Tagesspiegel .

Kundi la Berlin Postkolonial, mojawapo ya kundi lililohusika na mabadiliko liliunga mkono hatua ya serikali hiyo ya mtaa.

Katika taarifa lilisema kwamba kampeni hiyo ilizuia kuheshimiwa kwa ''Von Wissmann na mahala pake kuchukuliwa na mwanamke Mtanzania ambaye alipinga ukoloni na ubaguzi wa rangi''.

"Wissmann alikuwa mbaguzi na muhalifu wa kivita . Lucy Lameck anawakilisha mchango ulioshushwa thamani wa wanawake wa Tanzania waliopigania uhuru wa taifa hilo'', alinukuliwa akisema mwanaharakati wa Tanzania Mnyaka Sururu Mboro.

Je Lucy Lameck ni nani?
Alizaliwa mnamo 1934 Moshi mjini iliyokuwa wakati ule sehemu ya Tanganyika ya Kiingereza.

Alizaliwa katika familia ya wakulima, akajifunza kazi ya uuguzi kabla ya kuingia katika shughuli za siasa.

Baada ya mafunzo ya kazi ya muuguzi mnamo 1950, hakutaka kushiriki katika mfumo wa matibabu wa kikoloni wa Uingereza, na kwa hiyo alianza kufanya kazi ya karani.

Lucy Lameck alikuwa mwanasiasa wa Kitanzania, na mwanamke Mtanzania wa kwanza kuwahi kushika wadhifa wa uwaziri kwenye serikali ya kitaifa.

Alisoma baadaye kwenye Chuo cha Ruskin, huko Oxford, Uingereza.

Mwaka 1960 aliingia mara ya kwanza katika Bunge la Tanganyika kabla ya kuchaguliwa katika Bunge la Kitaifa la Tanzania mnamo 1965.

Anakumbukwa kama kielelezo cha kuigwa, akiwa amefanya kazi katika maisha yake yote kuboresha hali ya wanawake nchini Tanzania.


View attachment 1636310View attachment 1636311
 
Back
Top Bottom