Barabara ya Ujerumani kupewa jina la mwanaharakati wa Tanzania, Lucy Lameck. Alikuwa Waziri wa 1 mwanamke wa Tanzania

Mzee Mohamed Said, napenda kusoma michango yako! Ilhali elimu ya historia ni duni kiasi Tanzania nafurahi kuona yupo mzee anayetukumbusha tena na tena mambo yaliyopita na umuhimu wake kwa watu wa leo hii!
Ila hapa kuhusu Wissmann unirihusu nisahihishe kidogo na kuongeza machache.
Wissmann hakuenda Afrika Kusini kutafuta Wazulu.
Hermann von Wissmann aliyezaliwa 4 Septemba 1853 kwa jina kamili Hermann Wilhelm Leopold Ludwig Wissmann mjini Frankfurt (Oder) na kufariki 15 Juni 1905 katika Austria) alikuwa Mjerumani aliyejulikana kama mpelelezi wa Afrika, mwanajeshi na gavana wa pili wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kati ya 26 Aprili 1895 hadi 3 Desemba 1896. Aliongoza jeshi la Kijerumani lililokandamiza vita ya Abushiri mwaka 1889.
Baada ya kumaliza shule ya sekondari akajiunga na jeshi la Prussia (wakati ule dola kubwa ndani ya Ujerumani iliyoendelea kuwa nchi moja mwaka 1871), baadaye na jeshi la utemi wa Mecklenburg (Ujerumani ya kaskazini). 1874 alipata cheo cha luteni.

Mwaka 1881 aliomba likizo akajiunga na safari ya upelelezi wa Afrika na kupitia Luanda (Angola) alivuka beseni ya mto Kongo. Alikutana na mfanyabiashara Tippu Tip akajiunga naye na kuendelea hadi pwani la Bahari Hindi na 15 Novemba 1881 alifika Saadani. Pale Saadani alikutana na Bwana Heri, mtawala wa Saadani, na mkutano huu ulikuwa muhimu baadaye. Maana aliporudi mwaka 1889 kupigana na Abushiri alikuwa tayari kufanya mkataba wa amani na Bwana Heri (aliyekuwa kiongozi wa vita dhidi ya Wajerumani pamoja na Abushiri) hivyo Bwana Heri waliweza kurudi Saadani ilhali Abushiri alikamatwa na kunyongwa.
Safari ile ilimpatia sifa ya kuwa mzungu wa wanza aliyefaulu kuvuka Afrika kutoka magharibi hadi mashariki.

Baada ya kurudi Ujerumani kupitia Zanzibar na Misri aliajiriwa na mfalme Leopold II wa Ubelgiji kwa safari nyingine ya upelelezi katika sehemu za kusini ya beseni ya Kongo. Kupitia Malanje (Angola) alipita kwenye njia ya mto Lulua hadi kufikia mto Kasai. Njiani aliunda kituo cha kijeshi cha Luluaburg (Kananga). Kwa njia ya maboti waliingia katika mto Kongo na baada ya siku 50 walifika Leopoldville (leo: Kinshasa). Baadaye alirudi tena kwa safari nyingine alipeleleza njia nyingine kutoka Atlantiki hadi Msumbiji kupitia ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.

1888 alirudi tena Ujerumani. Wakati huohuo vita ya Abushiri ilikuwa ilianza tayari ambako wenyeji wa pwani la Afrika ya Mashariki walipinga majaribio ya Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki kushika utawala juu ya miji ya Waswahili kati ya Tanga na Lindi. Maafisa wa shirika waliuawa au walipaswa kukimbia na vituo vya Bagamoyo na Dar es Salaam pekee vilifaulu kujitetea kwa msaada wa wanajeshi wa manowari za Kijerumani. Hapo ilitokea azimio la serikali ya Ujerumani kuingilia kati (maana hadi wakati ule mradi wa Kijerumani katika Afrika ya Mashariki ulikuwa mradi wa kampuni ya kibinafsi tu iliyoanzishwa na Karl Peters. Chansella Bismark kiasili hakutaka kuanzisha koloni za serikali, ila kushindwa kwa kampuni ya Kijerumani ilitazamiwa kama aibu kubwa Ujerumani na kutokana na propaganda ya kisiasa Bismarck aliamua kujihusisha na mambo yale).

Wissmann (aliyejulikana kama Mjerumani aliyejua maeneo yale) aliombwa na serikali ya chansella Bismarck kuunda jeshi la kukandamiza upinzani wa wenyeji wa pwani.
Wissmann alipandishwa cheo kuwa kapteni akapewa cheo cha Mwakilishi wa Kaisari katika Afrika ya Mashariki. Bunge la Ujerumani liliambiwa ya kwamba upinzani ulisababishwa na wafanyabiashara ya watumwa likakubali kiasi cha mark milioni 2 kwa "vita ya kukomesha utumwa". Wissman aliajiri maafisa 21 na maafande 40 kutoka Ujerumani akaelekea Afrika. Njiani alipumzika kifupi Misri akawaajiri askari Wasudan 600 kutoka jeshi la Misri (walioachishwa kazi wakati ule kutokana na kupungukiwa kwa jeshi la Misri baada ya vita ya Mahdi). Baadaye askari 150 Wazulu waliajiriwa katika Msumbiji kama nyongeza. Jeshi hili lilijulikana kama "Wissmanntruppe" (kikosi cha Wissmann). Walipewa usaidizi na manowari za Kijerumani zilizokaa kwenye Bahari Hindi mbele ya pwani la Afrika ya Mashariki.

Hivyo si Wissmann aliyeenda kuwatafuta Wazulu, alimtuma afisa mmoja aliyeenda kule na kuwaajiri, pamoja na Babu wa Sykes.

Baada ya vita ya Abushiri serikali ya Ujerumani iliona kampuni ilishindwa kabisa ikaamua kuchukua maeneo yaliyodaiwa na kampuni ya Peters na kuifanya Koloni ya serikali.

Wissmann alirudi Ujerumani alipoandika kitabu na kuzunguka nchi akihotubia mikutano ya kusambaza wazo la kupanusha koloni za Ujerumani. Pia alikusanya pesa kwa ajili ya meli iliyokusudiwa kupelekwa Ziwa Viktoria Nyanza. 1893 alisafiri tena Afrika akaipeleka meli kwenda Ziwa Nyassa kwa sababu upinzani wa Wahehe chini ya Mkwawa ulizuia safari katika Tanganyika ya kati.

1895 (baada ya mapigano ya Lugalo ambako Jeshi la Kijerumani -iliyokuwa bado kwa asilimia kubwa jeshi liliowahi kuanzishwa na Wissmann, chini ya viongozi Wajerumani- iliangamizwa na Wahehe, hivyo serikali iliona kumtuma gavana mpya) aliitwa na serikali kuwa gavana wa pili wa koloni lakini Desemba 1896 alipaswa kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya akawa mtumishi wa wizara ya koloni huko Berlin.

1899 alipumzika akaishi Austria alipokufa tarehe 15 Juni 1905.

Hayo ni habari za Wissmann, nimechukua kutoka Hermann von Wissmann - Wikipedia, kamusi elezo huru ambako kuna pia vyanzo vinavyotajwa.

Hapo Dar es Salaam iko Lucy Lameck Road, ambayo ni mtaa mdogo wa dead end mwenye urefu wa mita 100 hivi, pale Msasani, inayotoka Mwai Kibaki Road.

Nasikia kule Berlin kulikuwa na mapendekezo mbalimbali kutafuta jina mbadala kwa Wissmann, pamoja na "Funmilayo Ransome-Kuti" (mama mwanaharakati wa Nigeria) na pia "Nangoiyastraße". Sina uhakika lakini nahisi walipendelea walienda mwishowe kwa "Lucy Lameck" kwa sababu majina mengine ni magumu sana kutamka kwa Wajerumani... (tukumbuke kule Ujerumani kila mtu anapata anwani yake kwenye kitambulisho pamoja na jina la barabara, hivyo kuweza kutamka kuna maana kwa wakazi wenyewe...)
 
Mwana...
Usiwe na hofu ya kunisahihisha kwani kila kazi ya mikono ya binadamu haikosi kasoro.

Mimi nimesoma nyaraka za Sykes na katika historia hii ya Hermann von Wissman nimetegemea mswada alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki dunia mwaka wa 1949 na historia hii yeye aliipokea kutoka kwa Affande Plantan.

Hebo tupa jicho hapo chini niliyoandika na ndiyo yapo katika kitabu cha Abdul Sykes (1989):
''Effendi Plantan came to Tanganyika together with Sykes Mbuwane on board a Germany warship which landed in Pangani in the late 1800s.

Sykes Mbuwane came from Inhambane, Kwa Likunyi, a village in Portuguese Territory of Mozambique.

He was part of a mercenary force of Zulu warriors recruited and led by the German soldier and explorer, Harmine von Wissman.

The legacy passed down by the Zulu warriors to their children is that:
Germans made an agreement with Mohosh, the Chief of Inhambane in Mozambique, that his people would go with the Germans to Tanganyika, and that any land they conquered would be shared equally between the Zulu and the Germans.

The Germans then put the Zulu on a ship which landed them at Pangani under the leadership of Mohosh and a warrior who was to become known as Effendi Plantan. [1]
This was the story passed down to Kleist who in turn passed it on to his son Abdulwahid.

After more than half a century since the Zulu landed at Pangani, Abdulwahid passed it on to his daughter Aisha Daisy, an undergraduate student of history at the University of Dar es Salaam.

Iliffe gives a more plausible explanation on the Zulu recruitment into the German army based on colonial records.

In the quest to create a German colony in East Africa, and faced with opposition from Arabs along the coast and well as resistance from African chiefs in the interior, the Imperial Chancellor Otto von Bismarck chose Harmine von Wissman [2] to quell resistance and restore order:

[1]Buruku, op. cit. p.96.
[2]Harmine von Wissman was an explorer and soldier. He led the suppression of the resistance of 1888-1889 and was Governor of German East Africa in 1895-1896.

Mwana...
Juu ya haya yote kwangu mimi kuandika kitabu cha Sykes ilikuwa na changamoto kubwa sana.

Wakati nafanya utafiti miaka ya 1980 mswada wa Kleist Sykes tayari ulikuwa ushachapwa kama ''seminar paper,'' na mjukuu wake Aisha Daisy Buruku, bint ya Abdul Sykes na unaweza kupata hii paper Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, ''The Life of Kleist Sykes,'' (1968).

Seminar paper hii ikachapwa kitabu na John Iliffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Hii haikunizuia mimi kufanya utafiti mpya nikutumia vyanzo vilevile alivyovipitia Daisy na Iliffe lakini mimi nikaongeza na mahojiano na Ally Sykes mtoto wa pili wa Kleist Sykes na vyanzo vingine.

Nilipata mengi ambayo hawa waandishi wawili Daisy na mwalimu wake Iliffe hawakuyapata kwa hiyo hayapo katika machapisho yao.

Daisy alimwita babu yake katika kitabu cha Iliffe, ''Kleist Sykes The Townsman,'' mimi katika kitabu changu nimemwita, ''Kleist Sykes Man of Ideas.''

Yako mengi.
Nimeupenda mchango wako.
 
Mwana...
Usiwe na hofu ya kunisahihisha kwani kila kazi ya mikono ya binadamu haikosi kasoro.

Mimi nimesoma nyaraka za Sykes na katika historia hii ya Hermann von Wissman nimetegemea mswada alioandika Kleist Sykes kabla hajafariki dunia mwaka wa 1949 na historia hii yeye aliipokea kutoka kwa Affande Plantan.

Hebo tupa jicho hapo chini niliyoandika na ndiyo yapo katika kitabu cha Abdul Sykes (1989):
''Effendi Plantan came to Tanganyika together with Sykes Mbuwane on board a Germany warship which landed in Pangani in the late 1800s.

Sykes Mbuwane came from Inhambane, Kwa Likunyi, a village in Portuguese Territory of Mozambique.

He was part of a mercenary force of Zulu warriors recruited and led by the German soldier and explorer, Harmine von Wissman.

The legacy passed down by the Zulu warriors to their children is that:
Germans made an agreement with Mohosh, the Chief of Inhambane in Mozambique, that his people would go with the Germans to Tanganyika, and that any land they conquered would be shared equally between the Zulu and the Germans.

The Germans then put the Zulu on a ship which landed them at Pangani under the leadership of Mohosh and a warrior who was to become known as Effendi Plantan. [1]
This was the story passed down to Kleist who in turn passed it on to his son Abdulwahid.

After more than half a century since the Zulu landed at Pangani, Abdulwahid passed it on to his daughter Aisha Daisy, an undergraduate student of history at the University of Dar es Salaam.

Iliffe gives a more plausible explanation on the Zulu recruitment into the German army based on colonial records.

In the quest to create a German colony in East Africa, and faced with opposition from Arabs along the coast and well as resistance from African chiefs in the interior, the Imperial Chancellor Otto von Bismarck chose Harmine von Wissman [2] to quell resistance and restore order:

[1]Buruku, op. cit. p.96.
[2]Harmine von Wissman was an explorer and soldier. He led the suppression of the resistance of 1888-1889 and was Governor of German East Africa in 1895-1896.

Mwana...
Juu ya haya yote kwangu mimi kuandika kitabu cha Sykes ilikuwa na changamoto kubwa sana.

Wakati nafanya utafiti miaka ya 1980 mswada wa Kleist Sykes tayari ulikuwa ushachapwa kama ''seminar paper,'' na mjukuu wake Aisha Daisy Buruku, bint ya Abdul Sykes na unaweza kupata hii paper Maktaba ya Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, East Africana ''The Life of Kleist Sykes,'' (1968).

Seminar paper hii ikachapwa kitabu alichohariri John Iliffe, ''Modern Tanzanians,'' (1973).

Hii haikunizuia mimi kufanya utafiti mpya nikutumia vyanzo vilevile alivyovipitia Daisy na Iliffe lakini mimi nikaongeza na mahojiano na Ally Sykes mtoto wa pili wa Kleist Sykes na vyanzo vingine.

Nilipata mengi ambayo hawa waandishi wawili Daisy na mwalimu wake Iliffe hawakuyapata kwa hiyo hayapo katika machapisho yao.

Daisy alimwita babu yake katika kitabu cha Iliffe, ''Kleist Sykes the Townsman,'' mimi katika kitabu changu nimemwita, ''Kleist Sykes Man of Ideas.''

Yako mengi.
Nimeupenda mchango wako.
Naona tofauti yetu ni kuhusu sentensi hiyo : "Sykes Mbuwane came from Inhambane, Kwa Likunyi, a village in Portuguese Territory of Mozambique. He was part of a mercenary force of Zulu warriors recruited and led by the German soldier and explorer, Harmine von Wissman. "
Kutokana na yale ninayoona katika vyanzo vya Kijerumani ingekuwa sahihi tukitafsiri:
"sykes alikuwa sehemu ya jeshi la mamluki wa Kizulu walioajiriwa kwa niaba ya mwanejeshi na mpelelezi Wissmann wakahudumia chini yake"

Maana afisa aliyetumwa Hori ya Inhambane kutafuta mamluki alikuwa Hans von Ramsay (1862 - 1838, luteni wa jeshi la Prussia aliyewahi kuchukua likizo akisafiri Lamu na Witu kuwasindikiza akina Deinhardt (walioanzisha kwa miaka michache koloni ndogo pale Witu na kufanya mkataba na Sultani Ahmad ibn Fumo Bakari -aliyetafuta ulinzi wa Ujerumani dhidi ya Sultani wa Zanzibar) . Februari 1891 alichukua nafasi ya kuajiriwa na kikosi cha Wissmann. Alitumwa Msumbiji, yaani eneo la Kireno kutafuta mamluki wa nyongeza (labda pia kwa bei nafuu kuliko Wasudani wa Wissmann) kwa kibali cha serikali ya Kireno. Nimeona maelezo kuwa alilenga Inhambane kwa sababu wakati ule gharama za mahari zilikuwa zilipanda sana na hivyo vijana walitafuta ajira ili waweze kugharamia mahari.
Ilhali Wareno walimruhusu kuingia na kutafuta mamluki (walioruhusu mkataba wa miaka 3 pekee), naona uwezekano kabisa hali halisi alipaswa kuwasiliana na chifu wa wenyewe (maana utawala wa Wareno ulikuwa mdhaifu), inawezekana ni kweli kwamba alimwahidi yale yanayokumbukwa katika kumbukumbu ya familia ya Sykes.
 
Mwanamkiwi,
Iwe iwavyo mimi kiongozi changu kama nilivyokueleza ni Nyaraka za Sykes mswada alioandika Kleist Sykes kabla kufariki 1949 na Abdul Sykes alihifadhi mswada huu hadi ulipowekwa hadharani kama ''seminar paper'' ya Daisy Sykes Department of History Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, University of East Africa mwaka wa 1968.

Affande Plantan ndiyo chanzo cha historia hii kwa Kleist na Plantan alifariki mwaka wa ----1914.

Ama kwa binadamu kukosea kwa ama mpewaji habari ama mpokeaji ni jambo linalowezekana.

John Iliffe aliyetumia amefanya ''book review,'' ya kitabu changu, ''review'' iliyochapwa katika Cambridge Journal of African History na hakusema lolote kuhusu hili.

Lakini na yeye anaweza pia kuwa kakosea kwa kutegemea taarifa zilizoko katika Nyaraka za Sykes.

Taarifa ulizotoa zinabeba mambo mengi ambayo yanaboresha taarifa katika Nyaraka za Sykes kwa kiwango kikubwa sana.

Siwezi kabisa kukataa kuwa pengine aliyekwenda Kwa Likunyi kuwachukua Sykes Mbuwane na Affande Plantan kuwaleta Pangani ni Hans von Ramsay kwa kutumwa na Hermann von Wissman.

Inawezekana hapa katika Wajerumani hawa wawili na majina yao ndipo paliposababisha tatizo hili.

Ningependa kukufahamisha kuwa nimekutana tena na Wissmann mwaka huu katika utafiti wa kitabu nilichoandika ambacho kimechapwa mwaka huu - ''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam.''

Mwaka wa 1890 Wissman baada ya kumaliza vita na Abushiri alikwenda na jeshi lake Kilimanjaro kumshambulia Mangi Sina wa Kibosho.

Jeshi la Sina lilionyesha uhodari mkubwa wa mapambano.

Vita hivi vilinyanyua haiba ya Sina na Wajerumani wakanyoosha mkono wa urafiki na huo ndiyo ukawa mwisho wa uhasama baina ya Mangi Sina na Wajerumani.

Juu ya haya Rindi aliungana na Hermann von Wisssmann dhidi ya Sina na na hii ikapelekea kwa Sina kushindwa vita mwaka wa 1891.

Naamini katika haya kuna mengi hapa ya kutufikirisha.

1606621565438.png
 
Huyo muuza duka naye alikuwa mbumbumbu kiwango cha sgr!

Mwenyeji wa Afrika ashindwe kuijua Nchi mojawapo ya bara hili hadi agoogle!

Mbona ni jiografia ya 'primary' kabisa hiyo, aliishia kusoma vidudu

Huyo muuza duka naye alikuwa mbumbumbu kiwango cha sgr!

Mwenyeji wa Afrika ashindwe kuijua Nchi mojawapo ya bara hili hadi agoogle!

Mbona ni jiografia ya 'primary' kabisa hiyo, aliishia kusoma vidudu?
Itakuwa jamaa alikuwa South Africa, maana wao ndio wengi wao wana vidudu kichwani.
 
Thomas,
Natafuta picha ya Bi. Halima Selengia.

Mimi nimekulia Moshi na Mzee Yusuf Olotu nikmfahamu na mwanae Ahmed tumekuwa sote Mtaa wa Chini.
Mzee wangu Mohamed Said
Naam nimefurahi kuwa nawe uliishi mtaa wa chini na ukiwamfahamu
Marehemu Mzee Yusuph Olotu(Yusuph Ngozi) tukiishi nae Mtaa wa Somali hadi mauti yake 1997 akiishi nyumba ya nne kutoka kwetu.

Bi Halima Selengia "shangazi" kama ambavyo amekuwa akizoewa kuitwa na wazazi wangu na jamaa zangu akiishi mtaa wapili Mtaa wa Liwali moshi Mjini.
Ameishi hapo hadi mauti yake 20 June 2013.

Kama nilivyosema Hawa wote ni katika wazee wangu wakishuhudia kuzaliwa na kukua kwa wazazi wangu na baadae mimi hadi kuwa kijana barobaro.

Nimeambatanisha picha ya Marehemu Bi Halima Selengia "Shangazi"
IMG_20201129_065202.jpeg
 
Mwanamkiwi,
Iwe iwavyo mimi kiongozi changu kama nilivyokueleza ni Nyaraka za Sykes mswada alioandika Kleist Sykes kabla kufariki 1949 na Abdul Sykes alihifadhi mswada huu hadi ulipowekwa hadharani kama ''seminar paper'' ya Daisy Sykes Department of History Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam, University of East Africa mwaka wa 1968.

Affande Plantan ndiyo chanzo cha historia hii kwa Kleist na Plantan alifariki mwaka wa ----1914.

Ama kwa binadamu kukosea kwa ama mpewaji habari ama mpokeaji ni jambo linalowezekana.

John Iliffe aliyetumia amefanya ''book review,'' ya kitabu changu, ''review'' iliyochapwa katika Cambridge Journal of African History na hakusema lolote kuhusu hili.

Lakini na yeye anaweza pia kuwa kakosea kwa kutegemea taarifa zilizoko katika Nyaraka za Sykes.

Taarifa ulizotoa zinabeba mambo mengi ambayo yanaboresha taarifa katika Nyaraka za Sykes kwa kiwango kikubwa sana.

Siwezi kabisa kukataa kuwa pengine aliyekwenda Kwa Likunyi kuwachukua Sykes Mbuwane na Affande Plantan kuwaleta Pangani ni Hans von Ramsay kwa kutumwa na Hermann von Wissman.

Inawezekana hapa katika Wajerumani hawa wawili na majina yao ndipo paliposababisha tatizo hili.

Ningependa kukufahamisha kuwa nimekutana tena na Wissmann mwaka huu katika utafiti wa kitabu nilichoandika ambacho kimechapwa mwaka huu - ''Maisha ya Rajabu Ibrahim Kirama Jemadari wa Vita Kuwa Jemadari wa Uislam.''

Mwaka wa 1890 Wissman baada ya kumaliza vita na Abushiri alikwenda na jeshi lake Kilimanjaro kumshambulia Mangi Sina wa Kibosho.

Jeshi la Sina lilionyesha uhodari mkubwa wa mapambano.

Vita hivi vilinyanyua haiba ya Sina na Wajerumani wakanyoosha mkono wa urafiki na huo ndiyo ukawa mwisho wa uhasama baina ya Mangi Sina na Wajerumani.

Juu ya haya Rindi aliungana na Hermann von Wisssmann dhidi ya Sina na na hii ikapelekea kwa Sina kushindwa vita mwaka wa 1891.

Naamini katika haya kuna mengi hapa ya kutufikirisha.

View attachment 1637270
Mwana...
Chukulia haya nikuwekeayo hapo chini kama post mpya.

Haya yanatoka katika mswada ''Under the Shadow of British Colonialism The Life of Ally Kleist Sykes:''

''I left Dar es Salaam on board a ship known as Karanja and reached Laurenco Marques a few days later.

As fate would have it my wife was heavy with a child when I set my foot in the land where my forefathers had come from and settled half a century ago.

In Laurenco Marques Said Saleh, a Comorian received us.

In 1930 my father had written to him to inquire and try to trace his relatives but up to the time of his death in 1949, he did not receive any meaningful information of the whereabouts of his relatives.

Somehow Said Saleh years later, after my father had passed away, was able to locate my father’s sister, my aunt, Maria Mbuwane, one of the daughters of Sykes Mbuwane left behind in Imhambane in late 1800s.

It is my belief that my father did not know of the existence of his sister because nowhere in the records he left behind was her name mentioned nor did he mention her in his talks.

My aunt came to see me.

When I narrated the family history she broke down in tears. My aunt took us to Kwa Likunyi, a village where my uncle Kattini Mbuwane lived, this village was some few miles from Nyambani where Sykes Mbuwane had originally settled when the clan trekked north from South Africa.

There I was informed that my uncle had died only some few months back.

All that was left me to do was to go and pay respect to his grave, as is the custom for Muslims.

My uncle had left behind three children, my cousins, Abdallah, Ahmed and Asya.

The family was well to do.

Abdallah the eldest child had his own fishing boat and was therefore financially independent.

Somehow my cousins were not too happy to see me, they thought I had gone there to claim property left behind by uncle Kattini.

They did not believe that after fifty years I, the child of a Zulu who had settled in Tanganyika many years ago would spend so much money to travel all the way from Tanganyika to Mozambique just to visit and get to know an uncle I had not even seen.

Aunt Maria took it upon herself to alley that fear from them.

I had spent sometime with her back in Laurenco Marques and it did not take her very long to realise that her brother Kleist who she never saw had been a man of means and had left the family relatively well off.

I assured my cousins of my sincerity and purpose of the visit.

This settled I had a good time with my cousins only to be spoiled by the dreaded Portuguese Police who paid me a visit one fine day and asked me to leave the country immediately because my passport was temporary and my visa had expired.

Before I left Laurenco Marques I gave my cousins 1,000 escudos, which was not a small amount in 1952.''
 
Mitaala ya shule zetu inatukuza mizungu iliyoleta utumwa na kututawala kuliko mashujaa wetu. Kila mtu anamjua na kaandika countless essays kuhusu Livingstone, Stanley, Bismarck n.k. huku watu wetu waliofanya makubwa wakisahaulika. Smh.
 
Kulikua na kampuni za kuuza magari ya Peugeot , maduka ya Wahindi yalikuwa na mahitaji yote. Ukitaka viatu kutoka London, Rome na hata Bata ya Kenya. Ajira ndiyo usiseme, vijana walipata ajira bandarini, mahotelini. Nk
Tanga wachawi mliloga kila kitu hadi wahindi na mashamba ya mikonge vyote vikafa havipo tena
 
Mitaala ya shule zetu inatukuza mizungu iliyoleta utumwa na kututawala kuliko mashujaa wetu. Kila mtu anamjua na kaandika countless essays kuhusu Livingstone, Stanley, Bismarck n.k. huku watu wetu waliofanya makubwa wakisahaulika. Smh.
Lisu PIA ana mengi ya kuandika kuhusu AMSTERDAM kuliko Magufuli
 
Tanga wachawi mliloga kila kitu hadi wahindi na mashamba ya mikonge vyote vikafa havipo tena
Uchumi hutegemea siasa na amani ya nchi. Baada ya serikali kuanzisha mfumo wa chama kimoja na siasa za kijamaa, wazungu walinyang’anywa mashamba ya chai na mkonge. Hawa wazungu waliwekeza sana katika kilimo cha biashara, waliletwa na Waingereza baada ya WWII uchumi wa Uingereza ulianguka na ilitumia ardhi yote ya makoloni kuzalisha. Walizalisha chai na katani na bandari ya Tanga ilisafirisha mizigo ya chai, kahawa na katani ilikua busy mno. Ajira zilikuwepo kuanzia mashambani, bandarini, mahotelini nk.

Mashamba yalipoendeshwa na serikali, yalikufa yote. Boss anaingia ofisini saa nne asubuhi kwakua yeye ndiye boss na hakuna wa kumuuliza.
 
Mzee wangu Mohamed Said
Naam nimefurahi kuwa nawe uliishi mtaa wa chini na ukiwamfahamu
Marehemu Mzee Yusuph Olotu(Yusuph Ngozi) tukiishi nae Mtaa wa Somali hadi mauti yake 1997 akiishi nyumba ya nne kutoka kwetu.

Bi Halima Selengia "shangazi" kama ambavyo amekuwa akizoewa kuitwa na wazazi wangu na jamaa zangu akiishi mtaa wapili Mtaa wa Liwali moshi Mjini.
Ameishi hapo hadi mauti yake 20 June 2013.

Kama nilivyosema Hawa wote ni katika wazee wangu wakishuhudia kuzaliwa na kukua kwa wazazi wangu na baadae mimi hadi kuwa kijana barobaro.

Nimeambatanisha picha ya Marehemu Bi Halima Selengia "Shangazi" View attachment 1637271

Ndugu yangu,
Furaha yangu haisemeki.

Ahsante sana.
 
@mrangi yeye ni database ya matukio yote ya nchi nzima.
barafu huyu ni wa taasisi ya serikali hawezi onekana.
Chige naye historia ya nchi hii anaijua

Hawa ni wa kuwawahi kabla 'hawajapotea'. Hatujui siku wala saa
Hapa JF kuna vichwa vina mengi ya kuongea ni hazina ya maarifa
 
Back
Top Bottom