Mwanamkiwi
JF-Expert Member
- Mar 7, 2019
- 2,023
- 2,402
Mzee Mohamed Said, napenda kusoma michango yako! Ilhali elimu ya historia ni duni kiasi Tanzania nafurahi kuona yupo mzee anayetukumbusha tena na tena mambo yaliyopita na umuhimu wake kwa watu wa leo hii!
Ila hapa kuhusu Wissmann unirihusu nisahihishe kidogo na kuongeza machache.
Wissmann hakuenda Afrika Kusini kutafuta Wazulu.
Hermann von Wissmann aliyezaliwa 4 Septemba 1853 kwa jina kamili Hermann Wilhelm Leopold Ludwig Wissmann mjini Frankfurt (Oder) na kufariki 15 Juni 1905 katika Austria) alikuwa Mjerumani aliyejulikana kama mpelelezi wa Afrika, mwanajeshi na gavana wa pili wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani kati ya 26 Aprili 1895 hadi 3 Desemba 1896. Aliongoza jeshi la Kijerumani lililokandamiza vita ya Abushiri mwaka 1889.
Baada ya kumaliza shule ya sekondari akajiunga na jeshi la Prussia (wakati ule dola kubwa ndani ya Ujerumani iliyoendelea kuwa nchi moja mwaka 1871), baadaye na jeshi la utemi wa Mecklenburg (Ujerumani ya kaskazini). 1874 alipata cheo cha luteni.
Mwaka 1881 aliomba likizo akajiunga na safari ya upelelezi wa Afrika na kupitia Luanda (Angola) alivuka beseni ya mto Kongo. Alikutana na mfanyabiashara Tippu Tip akajiunga naye na kuendelea hadi pwani la Bahari Hindi na 15 Novemba 1881 alifika Saadani. Pale Saadani alikutana na Bwana Heri, mtawala wa Saadani, na mkutano huu ulikuwa muhimu baadaye. Maana aliporudi mwaka 1889 kupigana na Abushiri alikuwa tayari kufanya mkataba wa amani na Bwana Heri (aliyekuwa kiongozi wa vita dhidi ya Wajerumani pamoja na Abushiri) hivyo Bwana Heri waliweza kurudi Saadani ilhali Abushiri alikamatwa na kunyongwa.
Safari ile ilimpatia sifa ya kuwa mzungu wa wanza aliyefaulu kuvuka Afrika kutoka magharibi hadi mashariki.
Baada ya kurudi Ujerumani kupitia Zanzibar na Misri aliajiriwa na mfalme Leopold II wa Ubelgiji kwa safari nyingine ya upelelezi katika sehemu za kusini ya beseni ya Kongo. Kupitia Malanje (Angola) alipita kwenye njia ya mto Lulua hadi kufikia mto Kasai. Njiani aliunda kituo cha kijeshi cha Luluaburg (Kananga). Kwa njia ya maboti waliingia katika mto Kongo na baada ya siku 50 walifika Leopoldville (leo: Kinshasa). Baadaye alirudi tena kwa safari nyingine alipeleleza njia nyingine kutoka Atlantiki hadi Msumbiji kupitia ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.
1888 alirudi tena Ujerumani. Wakati huohuo vita ya Abushiri ilikuwa ilianza tayari ambako wenyeji wa pwani la Afrika ya Mashariki walipinga majaribio ya Shirika la Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki kushika utawala juu ya miji ya Waswahili kati ya Tanga na Lindi. Maafisa wa shirika waliuawa au walipaswa kukimbia na vituo vya Bagamoyo na Dar es Salaam pekee vilifaulu kujitetea kwa msaada wa wanajeshi wa manowari za Kijerumani. Hapo ilitokea azimio la serikali ya Ujerumani kuingilia kati (maana hadi wakati ule mradi wa Kijerumani katika Afrika ya Mashariki ulikuwa mradi wa kampuni ya kibinafsi tu iliyoanzishwa na Karl Peters. Chansella Bismark kiasili hakutaka kuanzisha koloni za serikali, ila kushindwa kwa kampuni ya Kijerumani ilitazamiwa kama aibu kubwa Ujerumani na kutokana na propaganda ya kisiasa Bismarck aliamua kujihusisha na mambo yale).
Wissmann (aliyejulikana kama Mjerumani aliyejua maeneo yale) aliombwa na serikali ya chansella Bismarck kuunda jeshi la kukandamiza upinzani wa wenyeji wa pwani.
Wissmann alipandishwa cheo kuwa kapteni akapewa cheo cha Mwakilishi wa Kaisari katika Afrika ya Mashariki. Bunge la Ujerumani liliambiwa ya kwamba upinzani ulisababishwa na wafanyabiashara ya watumwa likakubali kiasi cha mark milioni 2 kwa "vita ya kukomesha utumwa". Wissman aliajiri maafisa 21 na maafande 40 kutoka Ujerumani akaelekea Afrika. Njiani alipumzika kifupi Misri akawaajiri askari Wasudan 600 kutoka jeshi la Misri (walioachishwa kazi wakati ule kutokana na kupungukiwa kwa jeshi la Misri baada ya vita ya Mahdi). Baadaye askari 150 Wazulu waliajiriwa katika Msumbiji kama nyongeza. Jeshi hili lilijulikana kama "Wissmanntruppe" (kikosi cha Wissmann). Walipewa usaidizi na manowari za Kijerumani zilizokaa kwenye Bahari Hindi mbele ya pwani la Afrika ya Mashariki.
Hivyo si Wissmann aliyeenda kuwatafuta Wazulu, alimtuma afisa mmoja aliyeenda kule na kuwaajiri, pamoja na Babu wa Sykes.
Baada ya vita ya Abushiri serikali ya Ujerumani iliona kampuni ilishindwa kabisa ikaamua kuchukua maeneo yaliyodaiwa na kampuni ya Peters na kuifanya Koloni ya serikali.
Wissmann alirudi Ujerumani alipoandika kitabu na kuzunguka nchi akihotubia mikutano ya kusambaza wazo la kupanusha koloni za Ujerumani. Pia alikusanya pesa kwa ajili ya meli iliyokusudiwa kupelekwa Ziwa Viktoria Nyanza. 1893 alisafiri tena Afrika akaipeleka meli kwenda Ziwa Nyassa kwa sababu upinzani wa Wahehe chini ya Mkwawa ulizuia safari katika Tanganyika ya kati.
1895 (baada ya mapigano ya Lugalo ambako Jeshi la Kijerumani -iliyokuwa bado kwa asilimia kubwa jeshi liliowahi kuanzishwa na Wissmann, chini ya viongozi Wajerumani- iliangamizwa na Wahehe, hivyo serikali iliona kumtuma gavana mpya) aliitwa na serikali kuwa gavana wa pili wa koloni lakini Desemba 1896 alipaswa kujiuzulu kutokana na matatizo ya kiafya akawa mtumishi wa wizara ya koloni huko Berlin.
1899 alipumzika akaishi Austria alipokufa tarehe 15 Juni 1905.
Hayo ni habari za Wissmann, nimechukua kutoka Hermann von Wissmann - Wikipedia, kamusi elezo huru ambako kuna pia vyanzo vinavyotajwa.
Hapo Dar es Salaam iko Lucy Lameck Road, ambayo ni mtaa mdogo wa dead end mwenye urefu wa mita 100 hivi, pale Msasani, inayotoka Mwai Kibaki Road.
Nasikia kule Berlin kulikuwa na mapendekezo mbalimbali kutafuta jina mbadala kwa Wissmann, pamoja na "Funmilayo Ransome-Kuti" (mama mwanaharakati wa Nigeria) na pia "Nangoiyastraße". Sina uhakika lakini nahisi walipendelea walienda mwishowe kwa "Lucy Lameck" kwa sababu majina mengine ni magumu sana kutamka kwa Wajerumani... (tukumbuke kule Ujerumani kila mtu anapata anwani yake kwenye kitambulisho pamoja na jina la barabara, hivyo kuweza kutamka kuna maana kwa wakazi wenyewe...)