Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Waziri wa kwanzaAnaweza kuwa naibu waziri wa kwanza mwanamke Tz, sina uhakika nalo kwani ni yeye na Bibi Titi Mohamed ndio walikuwa na vyeo hivyo kwa wakati mmoja.
Waziri mwanamke wa kwanza ni Julie Manning (wa sheria).
Huyo muuza duka naye alikuwa mbumbumbu kiwango cha sgr!Tanzania hasa Tanga ina historia kubwa sana Ki dunia sema ndio hivyo we are a sleeping Giant.
Rais wa Mwisho wa South Africa ya Makaburu alizaliwa Tanga.
Malkia Elizabeth alitangazwa kuwa Malkia wa Uingereza baada ya kifo cha Baba yake 1952 akiwa anazuru Ziwa Victoria.
Viongozi kadhaa wa Kitaifa wa Ujeruman wamezaliwa Tanganyika.
Viongozi kadhaa wa Kiafrica wana historia kubwa sana na Nchi yetu. Mf Watoto wa kwanza wa 3 wa Museven wote wamezaliwa Tanzania
Lakin cha kusikitisha Nchi yetu hasa miaka ya karibuni imejizika kabisa.
Kuna Mwaka nilikuwa Nchi moja ya Kusini mwa Jangwa la Sahara sasa tukaingia mitaani tukawa tunafanya shopping huku tunapiga story na wenzangu, yule Muuza Duka akawa interested na lugha yetu akatuuliza lugha gani hii na ya wapi tukamjibu, cha kushangaza eti haijui Tz hadi alipo google akajijibu ooh its Ngorongoro.
Publicity yetu tunaifanyia Tandale na Hadi Nyakanazi si zaid ya hapo.
Hatutaki bla bla, tunataka mjusi wetu tutengeneze pesa.
Pamoja sana, tunashukuru kwa historia hiiMJI WA BERLIN UNAFUTA BARABARA YA HERMANN VON WISSMAN NA KUIITA LUCY LAMECK
Jana jioni mwandishi wa BBC kannipigia simu kutaka tufanye mahojiano kuhusu Bi. Lucy Lameck akanifahamisha kuwa mji wa Berlin uko katika mchakato wa kubadili jina la Barabara ya Wissman na kuiita Lucy Lameck.
Sababu ya kufanya hivyo ni kuwa huyu Hermann Von Wissman alikuwa mtu katili na amefanya mengi mabaya Afrika wakati wa utawala wa Wajerumani.
Mimi nilikutana na Hermann von Wissman kwa mara ya kwanza katika mswada alioandika Kleist Sykes kabla ya kufariki mwaka wa 1949.
Wakati huo nilikuwa nafanya utafiti wa kitabu cha maisha ya Abdul Sykes.
Kleist Sykes katika mswada huu anaeleza kuwa Herman von Wissman ndiye aliyekwenda Kwa Likunyi kijijini kwa baba yake mkoa wa Imhambane Mozambique, kufunga mkataba na Chief wa Imhambane Mohosh ili atoe jeshi kuja Tanganyika kupigana na wananchi wanaopinga utawala wa Wajerumani.
Wissmann na hawa mamluki wa Kizulu wakasafiri kwenda Luarenco Marques wakapanda manowari hadi Pangani.
Hili ndilo jeshi lililopigana na Abushiri bin Salim Al Harith Pangani na Chief Mkwawa Iringa.
Wissman alifanya ukatili mkubwa wakati wa vita hivi akiua, kuchoma moto vijiji na kuharibu mazao mashamabani ili kusababisha njaa.
Katika jeshi hili la mamluki wa Kizulu pamoja na Chief Mohosh ambae baadae alikuja kujulikana Tanganyika kama Affande Plantan alikuwapo Sykes Mbuwane.
Uzao wa askari hawa wawili, Sykes na Plantan walikuja kuwa Waafrika mashuhuri katika mji wa Dar es Salaam wakati wa ukoloni wa Muingereza na wakawa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya ukoloni na kupigania uhuru wa Tanganyika ingawa Schneider Abdillah Plantan na Kleist Sykes na walikuja kupigana ndani ya jeshi la Wajerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow Vorbeck dhidi ya Waingereza katika Vita Vya Kwanza Vya Dunia (1914 - 1918).
Katika Vita Vya Pili Vya Dunia (1939 - 1945) wajukuu wa hawa Sykes Mbuwane wakapigana katika vita hivi lakini safari hii wakapigana upande wa Waingereza dhidi Wajerumani waliokuwa washirika wa babu na baba zao.
Turudi kwa Wissmann.
Hivi ndivyo Ujerumani na jina hili la Wissmann linavyogusa historia ya koo hizi mbili na baada ya Ujerumani kushinda vita dhidi ya wananchi wa Tanganyika alifanywa kuwa Gavana mwaka wa 1895.
Mji wa Dar es Salaam ulikuwa na sanamu za Wissman katikati ya mji ambazo zilikuja kuondolewa baada ya Vita Kuu Vya Kwanza Waingereza walipokuja kuwa watawala wapya wa Tanganyika.
Hatua ya Ujerumani na mji wa Berlin kufuta jina la raia wao aliyewapigania kuwezesha Ujerumani kuitawala Tanganyika kama koloni lao ni hatua inayoonyesha mabadiliko makubwa ya fikra.
Ingetosha tu kwa Ujerumani kufuta jina la barabara na kuipa jina lingine la Mjerumani yoyote wamtakae lakini kwa kitendo hiki cha kufuta jina la Wissman na kuweka jina la Lucy Lameck hili ni jambo ambalo wao wenyewe tu ndiyo wanaweza wakalieleza vizuri zaidi.
Wajerumani wanasema kuwa wameamua kumpa heshima hii Lucy Lameck kwa ajili ya mchango wake wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.
Hakika Lucy Lameck anastahili heshima hii.
Historia ya Lucy Lameck mzaliwa wa Kilimanjaro inaanza na kuundwa kwa chama cha TANU Moshi mjini kiongozi akiwa Yusuf Olotu, wakati huo Lucy Lameck akiwa msichana mdogo wa miaka 20.
Yusuf Olotu anasema Lucy Lameck alimuunga mkono katika mapambano yake na Joseph Kimalando ambae ingawa alikuwa mmoja wa waasisi 17 wa TANU Dar es Salaam mwaka wa 1954, lakini aliporudi Moshi yeye ndiye akawa ndiyo kikwazo kikubwa cha kuisajili TANU na mwishowe akajiunga na UTP chama cha Wazungu kuipiga vita TANU.
Lucy Lameck alishiriki katika vita hivi pamoja na wanawake wengine ambao yeye walimzidi umri kama Mama bint Maalim, Amina Kinabo, Halima Selengia kwa kuwataja akina mama wachache.
Baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 Lucy Lameck akawa mwanamke wa kwanza kuteuliwa na Mwalimu Nyerere kuwa waziri wa serikali.
Inatia furuha kusikia kuwa Ujerumani imemuadhimisha mzalendo mama yetu huyu aliyepigania uhuru wa Tanganyika.
Picha: Lucy Lameck, Mtaa utakaopewa jina lake, Hermann von Wissmann, Sanamu ya Wissman Dar es Salaam 1906.View attachment 1636559View attachment 1636560View attachment 1636561
Thomas,Umewataja Wazee wawili mashuhuri ambao kwangu nawajua personal ni katika jamaa zangu(Family)
1.Marehemu Mzee Yusuph Olotu
2.Marehemu Bi Halima Selengia
Hawa ni miongoni mwa wazee wangu
Tangu nikiwa kijana mdogo nikiwaona wakija nyumbani na mimi nikienda kwao kuwaamkua mara kadhaa.
Allah azirehemu Nafsi zao na kuwapa pepo.




Picha:Hivi JF hakuna wanaofanya podcasts tafuteni hawa watu muongee nao.. Kuna contents nyingi sana katika hawa viumbe
1. Mohamed Said
2. Infantry Soldier
3. CONTROLA
4. GLOBAL CITIZEN
5. Sky Eclat
6. Mla Bata