Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Bashe: Kuna kikundi ndani ya Idara ya Usalama (TISS) kinahusika na utekaji. Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa

Swali la kizushi kuna mihimili 3 Bunge, Serikali, na Mahakama kiutendaji hii mihimili inategemeana japo hakuna muhimili unaouingilia muhimili mwingine, Inakuwaje bunge likikosolewa na mihimili mingine inaonekana Bunge limedharauliwa? lakini Wabunge kutuhumu na kukashifu mihimili mingine ni sawa?!
 
FB_IMG_1491815675895.jpg
 
Kweli sasa ndiyo naanza kumuelewa rais awamu ya 4, Dr. JK , alisema hivi " ukitaka nchi itikisike wewe wataje au waguse wauza unga, maana wamo wanasiasa wakubwa na serikalini, viongozi wa dini..."

Sasa , hivi mizengwe mingi anafanyiwa JPM, kwa sababu , tu serikali anayoiongoza imetangaza vita dhidi ya wahusika wa unga wa sembe / sumu.

Dr. J Kikwete, pumzika baba popote ulipo, ila sasa ukweli unaonekana wa ulichokisema.

JPM, kaza tena, ili tuzidi kuwatambua aliowasema JK kuwa wako kila mahala.

RC wa dar, jiandae tu, kila anaye inua kichwa wewe pasua / piga kichwa tu.

Pia, na sisi wazalendo tunazidi kuandika majina yao mmoja baada ya mwingine!
Wakat anaingia madarakani JPM mambo yalikua mabaya mkasema 'Tumpe muda hata mwaka bado!'
Leo hii mambo yameendelea kuwa.magumu zaidi mnasema nchi inatikiswa na WAUZA DAWA ZA KULEVYA.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyu Bashe anajistukia tu, kwanini asijilipue kabsa kwa kutaja wahusika maana anajijua kabsa hayupo CCM tokea kipindi kile lowassa amekatwa hivyo nafsi yake haina amani kabsa kuendelea kuwepo CCM ila tu anajilazimisha, kujilazimisha huko kuna mkuta anazungumza mambo ya ajabu kabsa ya kumchafua Rais. Chunguzeni kwanini wale team Lowassa wote kama bashe,msukuma,malima ndio wapiga kelele kila siku? Kwanini Wao tu?

Hivi usalama gani wa taifa ukawa na kikundi cha utekaji na tena utekaji wa kipuuzi kabsa kama tunaouona sasa? System ikitaka kukuua inakuondoa tu haisubiri kukuteka.

Hizi ni chuki tu za baadhi wa wabaya wa Magufuli maana kama kuyabana majizi ni kweli kayabana kwa hiyo tusitegemee mteremko kwa Magufuli hata siku moja.Watu wenye pesa chafu watahonga sana hawa whistleblower kumchafua Magufuli.

Watamsingizia mengi mno huyu mzee na ndio kwanza picha inaanza.
kuna MAJITU MENGINE HUMU wao chuki zao ni mbele tu HATA KWENYE UWONGO YANAKUBALI TU.....utasikia mtu anasema ETI MAGUFULI nchi imemshinda....SASA hao ambao nchi haikuwashinda walitufikisha wapi???mbna still mlikuwa mna piga kelele???
Afadhali ya huyu amabaye mnasema nchi imemshinda lakini pesa za walipa kodi zipo salama si kwenye mikono ya wachache.......
ACHA TU atunyooshe HII MIAKA 10 AKILI ZIKAE vizuri kichwani......
Non sense! i hope you are not a Tanzanian representative sample.
 
sijui kwanini Tanzania tunachagua wabunge wajing.a kama huyu yaani mtu unatumiwa tu Sms unakimbia bungeni kuropoka? mtu wa ajabu kabisa huyu.
 
Kusipo chukuliwa hatua yoyote. Dawa ni kila mtu kujihami kwa chochote. Wenye uwezo milikini pisto, wasio kuwa na uwezo watu wasioeleweka wakikufuatilia piga yowe la majambazi, kwenye gari tubebe hata sime kama wamasai au majambia kama ISS. Tunaojua martial arts mpe mtu yokogel ya chembe au mfanyie rocking kabla hajatoa pisto. Kiufupi iwe timing kwa timing mpaka kama taifa tuachane kufanyiana unyama kama wanyama pori. Ni kweli wote tutakufa lakini hii ya kuteswa na kikundi ambacho hata mamlaka za usalama hazikitambui utakua ni unga wa kijinga
 
Haya, waambie basi wawakilishe wananchi , na kama wameshindwa basi waachie ngazi siyo kupeleka kelele bungeni.

Kama hakuna hela, usalama wao unatishiwa basi, wakalime kwani mapori si yapo yakutosha??
bashe hana njaa kama wwe ndugu yangu, tafuta file lake ndio ujue,
 
Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe, ameomba mwongozo kuahirishwa kwa Bunge ili kutoa nafasi ya Wabunge wote kujadili matukio ya utekaji watu yanayoendelea.
Akiomba Mwongozo kwa Naibu Spika, Hussein Bashe amedai kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu. Amedai kuwa kuna Wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai. Mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie

"Kuna watu wamenitumia ujumbe kwamba mimi ni kati ya watu 11 tuliopo hatarini kufanyiwa vitu vibaya popote pale nijiangalie. Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana".

​


Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka.Kuna hali ya tahayari katika Taifa.

Jana nimeongea na Askofu mmoja wa Kikatoliki, nimeona dalili ya uhusiano wa JPM na Kanisa kudorora kwa namna anavyoendesha mambo ya Nchi.

Hatuwezi kulifumbia macho jambo hili, Watanzania wanatekwa na watu wasiojulikana'

Wasalaam

This is powerful massage ... siamini kitengo kina fanya mambo ya ajabu kiasi hiki ... naamini kuna watu wanatumia jina la kitengo kutekeleza ajenda zao ...
 
Ha ha ha haaaaaa

Ameambiwa eeeeh

Na hakwenda polisi kuripoti!!!

Asa bungeni ndio pa kutafuta kuichafua serikali, hawa wabunge wengin njaa inawauma kweli kweli.

Watanyooka tu

Wachafuzi wa serikali hii

Inabidi huyo akamatwe aojiwe zaidi, mchochezi tu
Sasa kma watekaji ni watu wa usalama, na polisi ndo hao hao wana usalama, utakuwa unafanya nini sasa..??

Alichofanyiwa Nape kilifanywa na mtu wa usalama, ila tukaambiwa HAKUWA POLISI, na wala hajakamatwa mpk sasa na hakuna chochote kinachoendelea. So who was that..??

Nways, tufanye alikuw anaongea na familia yake kama Gwajima. Tatizo liko wapi..??

Nia yke ni kutoa angalizo tu. Isije ikatokea mkasema kwamba kwanini hukusema..??
 
Bashite alianza kwa kuhakiki silaha mkoa mzima, ili akianza utekaji awe salama zaidi. Maana anakuwa anajua nani na nani wana silaha.
 
Ha ha ha haaaaaa

Ameambiwa eeeeh

Na hakwenda polisi kuripoti!!!

Asa bungeni ndio pa kutafuta kuichafua serikali, hawa wabunge wengin njaa inawauma kweli kweli.

Watanyooka tu

Wachafuzi wa serikali hii

Inabidi huyo akamatwe aojiwe zaidi, mchochezi tu

Ben saanane ali ripoti polisi saiv yuko wap sasa au mpaka babako au ndugu zako watekwe ndo itakuuma
 
Anayekataa hakuna utekaji,vitisho huyo ni kumuangalia kwa jicho la tatu,wachumia tumbo..hakika tupo pabaya...
 
Hii ni staili ya utawala ambao rais wa Rwanda anaitumia Sana, mtu anayeingia kwenye rada za rais lazima aazidhibiwe na mkono wa chuma....
Chondechonde TZ tusifike huko...

Hizi taarifa sio za kupuuza Kabisa!!
Mungu atulinde na hili janga jipya.
 
Nadhani wiki ijayo atakaye tekwa ni Harmorapa, sababu hii ndio Kiki ya mwezi. Bashe na Nape kuweni makini sana, hao wanaowachekea na kuwapumbaza kuna siku watawaua kabisa ili kupata kiki kamili, kama waliweza kumuondoa Chacha Wangwe nyie ni mbwa tu kwao.
Hata wakoloni waliua ndugu zetu wengi tu lakini fikra ya ukombozi ilisonga mbele mpaka
 
bashe hana njaa kama wwe ndugu yangu, tafuta file lake ndio ujue,

Haya, jiaminishe kuwa Mimi ni njaaa. Ila Dr. JK ameishatuwekea mambo yote wazi JPM kaja tu kutupa jiwe gizani, sasa tunawaona bila chengachenga wote aliowasema Dr. JK.
 
Back
Top Bottom