Bashiru Ally: Heshima ya nchi yetu imeshuka, tunadhalilika kwa njaa

Kipindi huyu mwamba akiwa Katibu Mkuu wa CCM chini ya himaya ya Mwendazake, Lissu aliibua hoja ya njaa kali kwa Taifa - aisee wakamshukia kama mwewe kwamba anapotosha umma.

What goes around...
Kwa hiyo kulikuwa na njaa alafu ikazimwa?
 
Kama vile yuko injeeee, unafiki ni unafiki tu, haijalishi unaungwa mkono au mguu
 
Huyu mpuuzi alitakiwa sasa hivi awe jera alifuja mabilioni ya walipa kodi kwenda kununua wapinzani kwa kushirikiana na jiwe.
Hana cha kumfundisha bashe atutolee unafiki.
Hakika, tena ni wa kiwango cha 555G
Wanazani watarudi tena?imetoka hiyo walinyanyasa sana hawa
 
Tunatafakari kwanza hawa wanasiasa maneno yao ukiyasikia lazima utafakari sana, huyu jamaa ndie aliyekuwa msaidizi mkubwa wa Jiwe na wakati wanatekeleza sera zao tulikuwa na tunawaambia wanapotupeleka wanakwenda kutuumiza, wakazuia watu wasiseme waseme wao tu, sasa maneno yetu yanatimia wao walioleta tabu yote hii ndio wanataka kugeuka kuwa wanatuonea huruma, hili linatupa hofu mno.

Bashiru ni mtu mbaya sana na badala ya kwenda kusaidia wakulima, unakuta raisi na waziri wake wanakuja na mpango kabambe wa kutoa ekari 10 kwa vijana wakalime, vijana ambao hawana ujuzi wa kilimo, hawakuchagua kilimo kama ndio shughuli yao ya uzalishaji mali na wameshatia pesa huko.

Sie tunawaambia tena kwanini wasiongeze nguvu kwa hawa wanaolima sasa wakaweka trekta katika kila kijiji ili kuwaongezea maeneo ya kulima, wakawakopesha mbegu, pembejeo na wakapima udongo ili stahiki ya mbolea ionekane. Hii ndio hofu ya watu kuchangia
 
Alishiriki moja kwa moja kwenye siasa za kishenzi za dhalimu. Ni mnafiki fulani anayekwenda na upepo.
Vip ushirika wa Dr samia aliekuwa makam wa rais?

Inabid ifike hatua kizur kifanyiwe kaz na kibaya kipingwe kwa nguvu zote bila kujal msemaji ni nan.

Yan tukatae ushaur mzuri kisa umetoka kwa mtu mbaya does it click into your mind [emoji2369].

Haijalishi ni mnafki, muovu and many stuff ila alichosema lazima kifanyiwe kaz LAZIMA SERIKAL IFAHAM NJAA SIO KITU KIZUR.Lazima uboreshwaji kweny kilimo uendelee bila kusahau demand ya watanzania kwanza.
 
Usitulazimishe kuamini kitu ambacho atukiona ila njaa na bei ya Michele tunaiyona,Dr badhiru ni sawa manyumbu wote
Kupinga WAZO DHAHABU alilosema bashiru kisa alikua alikua ni ishara ya wendawazim.
 
Achana na tindo!

Yeye ana maumivu sana alifanyiwa ukatili na magufuli!

Mimi kila siku huwa namshauri aende dawati la jinsia
 
Kufunga mipaka ni kumnyonya mkulima
Bashiru kazungumzia ubunifu. Kufunga mipaka hakuwez kumnyonya mkulima, wakulima wanauza mazao yao nje ya nchi sabab ya bei huko ni kubwa. Kama bei imewafany wakulima kupeleka mazao nje kwanin serikali isiangalie namna ya kuboresha maslah ya wakulima kwa kuuza bidhaa zao ndan ya nchi?

Lazima bei ziwe nzur ili mkulima afaidike na mnunuzi asilalamike.
 
Kwanza bashiru ajasema mipak ifungwe.Japo ni moja ya soln kwa sasa. Kufocus kweny uzalishaji hali ya kuwa wazalishaji wanalia njaa bei kupanda ni kukosa weled kweny maamuzi.

Kanuni anza nyumban kisha uende nje.Kulitokea ukame ukasababisha uzalishaji kupungua ilitakiwa mipaka iendelee kufungwa huku mikakati ya uboreshaji sekta ya kilimo ikiendelea,ili baada ya uzalishaji weny tija hapo badae wagen wapate chakula bila athari kwa wenyeji.
 
Changamoto yake ni moja tu, hivi sasa akubaliki na wahafidhina ndani ya chama, kosa lake linaoneka linatokana na zoezi alilolisimamia kwa uadilifu mkubwa wa kuhakiki mali za chama tawala. Ukweli wake umemponza, uongo na unafiki wake ungalimuokoa.
Kosa lake kubwa ni kujifunganisha na yule muuaji
 
Jibu swali wewe basha wa Bishiru,ni wapi na lini aliwahi sikia Tzn Kuna njaa Hadi heshima ya Nchi kushuka?

Kuwa Rais mpenda Haki sio kuwachekea wapumbavu kama wewe na Bashiru wanaotafuta umaarufu Kwa kupotosha.
Kwaio hizi kelele za bei kupanda watu kupunguza milo ya siku wew ujaiskia.ACHENI UJINGA WATANZANIA.
 
huyu ana gubu na hii serikali ana maumivu makubwa sana kuondolewa yale mavyeo makubwa amekuwa km mchochezi. Kuhusu njaa ukweli anaujua anajaribu kuihujumu serikali. Bila aibu eti heshima ya nchi imeshuka, hivi wanamvumilia wa nini huyu mchochezi na mzushi mwenye gubu na serikali hii? Wakamtupilie mbali arudi kufundisha. Nchi jirani kenya, somalia, Ethiopia wamekuwa na njaa kwa muda mrefu lakini hakuna mbunge wao alitoa matamshi mazito km haya eti heshima ya nchi imeshuka. Kwanza Tanzania kuna njaa wapi, hakuna anachojua amejaa uwongo bila kuona haya. Hakuna eneo nchi hii ina njaa pengine upungufu ambao serikali imejitahidi sana kuuziba. Hakuna njaa aache uwongo.
 
Huyu si ndiye alihusika pia kuvuruga uchaguzi wa 2020 akishirikiana na yule muuaji. Hana jema kwa wananchi huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…