Bei ya chakula ipo juu halafu mtu anasema Mama anaupiga mwingi

Umeandika kama mtu asiye na elimu.
Kaandika uhalisia, TZ tuna ardhi kubwa mno Tena Ina rutuba ya kutosha kuzalisha mazao ya Kila aina, Kwa kifupi tuna uwezo wa kuzalisha chakula Cha kulisha Afrika nzima.

Tatizo letu ni uzembe na uvivu tuambiane tu ukweli ndugu zangu, haiwezekani tunapata soko la nje badala tuchangamkie fursa tunabaki kulialia eti tufunge mipaka serious?

Angalia nchi zilizotuzunguka DRC Burundi Rwanda Kenya Yaani tulipaswa kufanya biashara ya chakula mpaka Somalia Sudani kusini n.k

Badala yake tunalialia tu na kuilalamikia serikali kweli?

Kwa ujinga ujinga huu hii nchi kusonga mbele tutasubiri sana

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Wala hakuna mkulima mwenye kuweza kusafirisha chakula shida ya Biashara ya chakula imeingiliwa na walanguzi ndio wanao miliki soko na sio mkulima.
Wananunua mali ikiwa shambani haswa mchele
Kumbe unajua suluhisho! Nenda na wewe ukanunue huku huko shambani
 
Wewe ni taahira!

Hakuna mkulima anafaidika na hizi bei hakuna! Kwanza hawana mazao sasa hivi.

Sisi tulioko huku field tunajua.
Mimi natokea jamii ya wafugaji na tunalima vile vile. Kwa kifupi gu sasa hivi angalau kidogo tunapata tija ya tunachozalisha

Kama unaishi hapo Dar au mji mwingine beba gharama za kuishi mjini acha kelele

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Acha uongo dogo!

Muulize mamako kule kijijini kama ana hata unga sasa hivi
 
Unambiwa mbowe anahaha mvua zinavyonyesha nchi nzima eti alitaka iwe ajenda
 
Rejea kumbukumbu wakati wa huyo unayemuona kuwa ana akili kuliko watu wote duniani,

Wakati wake mazao yalipanda bei wazembe mkanung'unika kama kawaida yenu aliwaambia nenda kauze hata ng'ombe 10 ununue ndio 1 ya mahindi wapumbavu nyie

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nenda kalime kama ajira hailipi.Mkulima hawezi kupangiwa bei au mahali pa kuuzia mazao yake,kwa kuwa yeye ni mfanyibiashara kama wengine.Mbona wafanyibiashara wengine hawapangiwi mahali pa kuuzia biashara zao wala bei za kuuzia?
 
Unategemea mtu kama DC au RC atasema bei ipo juu na wakati kila kitu anapata bure?
 
Kwa hiyo ni kosa nikinunua nikahifadhi wakati natafuta soko? Jamani tufanye kazi acheni uzembe

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Nawapa experience yangu. Mimi ni Mhadhiri kwenye Chuo Kikuu kimoja Dar es Salaam. Mwaka 2016-2017 kama mnakumbuka vyakula vilipanda bei sana. Nikaamua ntakuwa nalima kila mwaka nikaaza na ekari 10 kule Naberera Simanjiro mpaka mwaka jana nililima ekari 150 pamoja na hali mbaya ya hewa. Kuanzia hapo sijapungukiwa chakula na kila January nauza mazao napata ada na matumizi mengine ya familia. Sasa nasema endeleeni kukaa kwenye keyboards kupiga domo. Mtakula maafi. Yes twendeni tukalime tutengeneze vikundi vya uzalishaji nawaambia mtaacha malalamiko. Tatizo vijana wengi niliojaribu kwenda nao hawana uvumilivu kukaa shambani .maharage ni miezi mitatu lakini kijana wiki mbili tu amekumbuka club,uzinzi mjini, kubet etc. Mtabaki mnabeti mpaka mfe. Pili wanasiasa na viongozi hawasemi ukweli na kuongoza vyema wananchi .wanapenda kuwapambapamba wanachi kwa matumaini yasiyo ya kweli. Kiufupi hakuina serikali itakupwa wewe chakula hakuna labda kwa walemavu na dharura tuu. hakuna kula bure duniani tufanye kazi. Period.
 
Kwa akili yako mkuu unajua mkulima ananufaika na lolote kaka mkulima atabak kua grade ya Mwisho kimaisha apa Tanzania
Unataka kuniambia kuwa kwenye hii price hike Middleman anamlipa Mkulima kwa bei ya mwaka 2016-21?

Tuwe serious na arguments zetu, tusiwasemee wakulima kwa assumptions. Hakuna mkulima ambaye hajui kuwa Bei za mazao zimepanda.

Halafu hayo mawazo mgando ya kudharau kilimo ndiyo yanafanya vijana wote mnaishia kuwa wamachinga na wasusi wa nywele mijini.
 
Acha uongo dogo!

Muulize mamako kule kijijini kama ana hata unga sasa hivi
Kwani Niko wapi sasa hivi? Ndio nimetoka kuwatengea kuku msosi sahivi naingia Kwa nguruwe, maziwa yameshachukuliwa Toka saa 12 alfajiri, nikitoka hapa Banda la nguruwe naenda kuangalia matikitimaji yanaendeleaje.

Akiba ya Chakula ipo inatutosha mpaka msimu wa mavuno mwezi wa 6 huko. Endelea kuzurura mjini na kulialia mitandaoni

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu amini huyo mkulima unae msemea sahivi nae analia njaa maana Alisha uza kwa mfanyabiasha Kama huamini nenda singida vijijin sahivi wanasubiria maidi ya msaada watakayo uziwa kwa nusu Bei
 
Dogo! Usifikiri kila mtu kajaza mavi badala ya ubongo hapa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…