Benki Kuu ya Tanzania (BoT) yaanika Application 69 zilizofungiwa kwa utoaji mikopo kidijitali bila leseni
 
Inawezekana,kuna jamaa aliwahi kunipa stori sijui kama ilikuwa na ukweli au ilikuwa chai wajuzi watatia neno, ni muda kidogo ilikuwa 2016 PBZ ilikuwa inakopesha kwa riba ndogo sana, wafanyakazi wakaanza kumiminika huko sasa sijui Benk nyingine wakaweka figisu masuala ya ushindani PBZ wakafuatiliwa wakakutwa vibali vyao havipo sawa wakafungiwa kukopesha, jamaa waliokopa walijikuta tu ghafla mshahara uneingia bila makato na paysleep imekuja nyeupe haina deni
Subiri kwanza nikojoe nakuja
 
Wafunge na betting kampuni zimekua nyingi sana halafu uchwara

Betting ni Michezo ambayo inatambulika rasmi na Gaming Board ipo enzi na enzi tangia kina Jackpot Bingo late 90s ,biashara yeyote inatakiwa iendeshwe kisheria na ndiyo maana hata kipindi cha Magu kuna Bank zilifungiwa.

Betting inatambulika kiserikali na hata mikopo online nayo inatambulika kosa kuendesha bila leseni na hata ukifungua Bank ukaendesha bila leseni utafungiwa tu ,hata hiyo NBC au CRDB leseni yao ikiisha wasiporenew inafungiwa vile vile.
 
Nawasanua Sasa apps zilizosajiliwa ni hizi hapa
1. Flexi cash jina la kampuni ni sharp financial services.
2. Kili loan jina la kampuni ni puissant Microfinance.
3. Pesa Yako Hawa wapo Mbeya na Wanamilikiwa na kampuni ya Nchimika Microfinance limited
Wengine watazidi kuja kwa update
 
Binafsi naona walishamaliza kazi yao, kama ni kutakatisha fedha zimetakata haswa labda wakamatwe.
 
Hivi hakuna app ambazo hawahitaji picha za vitambulisho!?
 
Back
Top Bottom