Mbuli yaza
JF-Expert Member
- May 30, 2023
- 711
- 683
kama alikataa wangemfanya Nini? ukikubali ndiyo unafanyiwa hivi,RIP mwamba MAGU.Wamewaone TU,,mbona hukonhakuna shida kabisa,,Mbona wakati wajiwe alikataa fedha za elimu za masharti ya ushoga
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
kama alikataa wangemfanya Nini? ukikubali ndiyo unafanyiwa hivi,RIP mwamba MAGU.Wamewaone TU,,mbona hukonhakuna shida kabisa,,Mbona wakati wajiwe alikataa fedha za elimu za masharti ya ushoga
kama alikataa wangemfanya Nini? ukikubali ndiyo unafanyiwa hivi,RIP mwamba MAGU.Wamewaone TU,,mbona hukonhakuna shida kabisa,,Mbona wakati wajiwe alikataa fedha za elimu za masharti ya ushoga
watu weus mmelaaniwa , nyinyi ndo wakusanya mapato ya kwenye hizo maliasili ila mkitaka kupalinda au kupaendelza bas mnataka pesa za walipa kodi za ulaya zije kama msaada kujenga nchi yenu na huko ndo mmewekeza macho yenu kuliko kulinda makusanyo ya ndani yasiishie mifukoni mwa watu , hata hii habar ni aibu kuendelea kuwepoBenki ya Dunia imesitisha ufadhili wa mradi mkubwa wa utalii nchini Tanzania kwa madai kuwa umesababisha mateso miongoni mwa maelfu ya wanakijiji kama ilivyokuwa katika kuwahamisha jamii ya maasai kutoka Ngorongoro.
Hii ni baada ya kundi moja la kutetea haki nchini Marekani kwa muda mrefu kumtaka mkopeshaji huyo wa kimataifa kuchukua hatua hiyo.
Benki ya Dunia imechukua hatua ya kusitisha mradi huo wa dola milioni 150, ambao unalenga kuboresha usimamizi wa maliasili na utalii katika vijijini vya kusini mwa Tanzania.
Katika taarifa iliyotolewa leo Jumanne, Taasisi ya Oakland iliyokuwa ikiendesha kampeni hiyo imedai kwamba "kushindwa kuchukua hatua za haraka kulisababisha madhara makubwa kwa jamii."
Angalau dola milioni 100 zilikuwa tayari zimetolewa kwa mradi huo, ambao ulianza mwaka 2017 na hatua ya kusimamishwa kwake imeanza rasmi Aprili 18.
Taasisi ya Oakland, shirika la kutetea haki za binadamu lenye makao yake mjini California ambalo linaangazia jamii zilizotengwa, kwa miaka mingi imekuwa ikitoa wito kwa Benki ya Dunia kusitisha ufadhili wa mradi unaojulikanao kwa kifupi REGROW, kwa kwa madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki miongoni mwa wenyeji katika eneo hilo.
Kundi hilo katika ripoti iliyotolewa mwezi Novemba liliishutumu Benki ya Dunia kwa kushindwa kuziwajibisha mamlaka za Tanzania kwa kile ilichokiita "mauaji ya watu wengi na unyanyasaji wa kijinsia" wakati wa upanuzi wa Mbuga ya Wanyama ya Ruaha.
Ripoti hiyo ilisema mbinu za serikali ya Tanzania kulazimisha jamii kuondoka ili kuongeza utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, kama lengo la mradi wa REGROW, "zilisababishwa moja kwa moja na ufadhili wa Benki ya Dunia."
Benki ya Dunia ilisema wakati huo kwamba "haivumilii vurugu katika miradi inayoifadhili," na iliunda jopo la wakaguzi kupitia malalamiko yanayohusiana na mradi huo ili "kuamua kama maswala yaliyoibuliwa ni halali."
Katika mawasiliano ya hivi majuzi kati ya Benki ya Dunia na Taasisi ya Oakland yaliyoonekana na shirika la habari la The Associated Press, mkopeshaji huyo alithibitisha kusimamishwa kwa malipo zaidi kwa mradi wa REGROW "hadi kuwe na uhakika kwamba mradi unazingatia viwango vya kijamii na kimazingira."
Anuradha Mittal, mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Oakland, alisema uamuzi wa Benki ya Dunia kusitisha ufadhili ni ushindi kwa jamii zilizotengwa katika taifa hilo la Afrika Mashariki. Mital ameongeza kuwa uamuzi huo unatuma ujumbe mzito kwa serikali ya Tanzania kwamba kuna matokeo kwa ukiukwaji mkubwa wa haki unaofanyika kote nchini humo wakati ikiendeleza biashara ya utalii. Hata hivyo, mamlaka ya Tanzania haikutoa maoni kuhusiana na taarifa hii.
Acha kuwa mpumbavu kutetea waarabu kupewa ardhi yetu na wananchi kufukuzwa ardhi yao yWakazi wa Ngorongo hawajatendewa ubaya unless wale wabishi ambao walikuwa na ratiba zao binafsiView attachment 2971728.
Ila mkichunguza sana, unaweza kuta Kenya wanataka huo ufadhili, kwahiyo wanaleta hizo figisu
Mnamo Aprili 18, 2024, Benki ya Dunia imesitisha mara moja utoaji wa fedha kutekeleza mradi wa REGROW nchini Tanzania kuanzia mara moja. Hatua hii ni baada ya taasisi ya Oakland Institute kufanya advocacy kwa niaba ya niaba ya wakazi wa maeneo ambayo wataathiriwa na mradi huo...
Ngoja tuone, huenda pia Wazungu wako kazini wanafanya utafiti. Maana hiyo report imeanza kufanyiwa utafiti toka 2017 hadi hiyo jana 23/04/2024 ndo majibu yametoka.Kule ngorongoro wao sio kuvunja haki za binadamu? Kwa nini watu wakalazimishwe kuishi wasikokupenda
Mimi hii habari nimeiona kwenye The citizen.. Ni vyombo gani vya habari vya Tz unavyovizungumzia?!Juma hili benki ya dunia imezuia ufadhilii wa mabilioni ya shilingi kwenye sekta ya utalii na uhifadhi kwa Tanzania kutokana na madai ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na serikali ya Samia.
Habari hizi imetangazwa kwenye vyombo vya habari vya kimataifa, ila kwa vyombo vya ndani haikupewa nafasi hata kidogo.
Swali ninalojiuliza ni nani anayedhibiti uhuru wa habari huko serikalini? Ni Nape au Samia?
Fursa za watu kupiga pesa tu!