Utajuaje mwanaume kajitunza?Waulize wao wana bikra kwanza au wameshajitibu gono mara 100 kwa uzinzi et leo anadai apate binti aliejitunza
Binti aliejitunza anastahili mwanaume aina yake tu si vinginevyo
Sasa kwa mfano wale madogo wa juzi, waliojipost na kujinadi "ficheni mabwana zenu ndo tushavamia" hao nao utawalaumu wanaume?Hapa hakuna wakutipiwa lawama
Kinachoshangaza ni wanaume kujitoa kwenye hili swala kama vile vile hawahusiki
WANAUME, NAWAITA NJOOENI KWENYE JAMVI
ANGALIZO: Hapa ukija, njoo na hoja, usije na hisia zako
UTANGULIZI :Kumekuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wanaume wakisema mwanamke asiye na bikra hastahili kuolewa hastahili kutolewa mahari, abebwe mzobe mzobe mpaka ndoani
Ila nina swali moja kwa hawa wanaume wenye mtazamo huu: Kwani nani anayeondoa bikra ya mwanamke?
Si mwanaume naye anashiriki katika tendo hilo?
Sasa kwanini baadhi yenu mna nguvu nyingi za kuwananga wanawake wasio na bikra, lakini hamna nguvu hizo hizo za kuzungumzia wajibu wa wanaume wanaowashawishi na kuwatumia wasichana wadogo kingono?
Nasema hivyo kwa sababu kuna wasichana wanaoingia kwenye mahusiano ya kingono wakiwa bado wadogo, hawajakomaa vya kutosha kiakili na kihisia
Baadhi yao hudanganywa, hushawishiwa kwa ahadi mbalimbali au hutumiwa na watu wazima wanaotambua vizuri wanachokifanya
Mwisho hujikuta wamepoteza usichana wao
Cha kushangaza ni kwamba, mwanaume anaweza kushiriki katika mazingira yaliyosababisha mwanamke kupoteza bikra halafu baadaye akageuka na kumdharau mwanamke huyo kwa sababu hiyohiyo
Yaani wewe mwanaume ambae hukujitunza ambae unajua kila sample ya kei za wanawake
Unapata wapi nguvu ya kusema nataka mwanamke bikra?
Kwa usafi upi hasa ulionao?
Hao uliwachezea unataka nani ale makombo yako wewe unatafuta fresh?
Nimeingia mtandaoni kutafuta hali ya ukatili kingono kwa wasichani wenye umri mdogo
Kwa mujibu wa utafiti wa kitaifa wa Tanzania wa mwaka 2024 kuhusu ukatili dhidi ya watoto na vijana (VACS) asilimia 8.4 ya wanawake waliohojiwa wenye umri wa miaka 18β24 waliripoti kufanyiwa ukatili wa kingono kabla ya kufikisha miaka 18
Huu ni utafiti tu ambao wanawake wengine huogopa kufunguka
Lakini naamini wapo wengi zaidi na tunaona kesi nyingi hata hazipelekwi kwenye madawati huishia kumalizwa kwa ngazi ya familia
Wote tunajua haya mambo yapo tena hufanywa na watu wakaribu sana kwenye familia wale wa kuaminiwa na sio watu tu ni Wanaume wenzenu au hata nyinyi wenyewe π
Naomba nieleweke sio kwamba wanaume wote wako hivi. La hasha!
Kuna wanaume wanaoheshimu wanawake, wanaolinda watoto na wanaopinga kabisa vitendo hivi
Hoja yangu ni kwa wale wanaume wanaotaka mwanamke awe bikra wakati wa ndoa, lakini hawataki kuzungumzia wajibu wa mwanaume katika kulinda heshima na usalama wa wasichana
Hakuna bikra itatoka bila mwanaume au tuseme baiskeli?
Wanaume kwanini msianze kuhamasishana wenyewe kwa wenyewe kufunga zipu zenu na kuacha kurubuni wasichana kwenye umri mdogo?
Hivi hamuoni kua nyie ndio chanzo kikubwa?
Mwisho; Kama bikra ni kigezo cha thamani ya mwanamke, je thamani ya mwanaume anayeshiriki katika tendo hilo inapimwaje?
Kama mwanamke anatakiwa kuwajibika kwa historia yake ya kimapenzi, je, mwanaume naye hapaswi kuwajibika kwa matendo yake?
Na kama kweli tunataka kupunguza tatizo hili, kwanini tusianze kwa kuhamasisha heshima, uwajibikaji, kutowadanganya wasichana na kutowatumia watoto kingono?
MWISHO WA SIKU, SI UNAWEZA KUMDHARAU MTU KWA JAMBO AMBALO WEWE MWENYEWE ULICHANGIA KULITOKEA?
ShesRise_1 βοΈ
Kwa akili ya kawaida tu hii mada ilitakiwa iishie hapa maana hakuna hata haja ya kuongeza hoja nyingine. Ila kwa sababu wanawake wanatafuta chaka la kujifichia na kuhalalisha tabia zao mbovu mada haitoisha hii.Hivi mada ungeiacha tu maana unachotafuta ni makasiriko, suala la kutunza bikra liko mikononi mwa Mwanamke mwenyewe halihusiani na mwanaume hata.
Kuna wanawake wameolewa na bikira zao, kwamba wao walikuwa hawatongizwi au kushawishiwa kwa namna yoyote na wanaume? Hapana waliamua kubana mapaja yao licha ya ushawishi walioupata, ukiwauliza wao unafikiri watapeleka lawama kwa mwanaume?
Umeanza kukua mdogo wanguHahahaha,
Umeongea ukweli Mchungu dada, wanaume tunaongea kujifurahisha tu.
Ukweli ulioko nje, hakuna bikira, period.
Bikra sio kipimo cha thamani ya mwanamkeSIWEZI KUMUHESHIMU WALA KUMUONEA WIVU MWANAMKE AMBAYE SIKUMKUTA BIKRA
Kurumbembe wanapenda kufarijiana sanaUmeanza kukua mdogo wangu
Mimi kurumbembe sawa!! lakini hao wanaojitunza mpka ndoa ni wao mimi bikra yao hainisaidii chochoteKurumbembe wanapenda kufarijiana sana
WAPO WANAWAKE WANAOJITUNZA MPAKA NDOA
Kwa akili ya kawaida sawa ila kwa akili kibwa hii mada haiwezi kuushia hapaKwa akili ya kawaida tu hii mada ilitakiwa iishie hapa maana hakuna hata haja ya kuongeza hoja nyingine. Ila kwa sababu wanawake wanatafuta chaka la kujifichia na kuhalalisha tabia zao mbovu mada haitoisha hii.
Usitumie akili mnemba kufikiriaππ Ngoja nikuulize swali moja. Je, ni kweli kwamba baadhi ya wanawake hupima thamani ya mwanaume kwa uwezo wake wa kifedha? Mwanaume akiwa hana pesa, anaweza kukosa nafasi ya kuoa hata kama ana tabia nzuri, heshima na uaminifu.
Sasa kama mwanaume anapimwa kwa uwezo wake wa kifedha, je, sisi wanaume hatuna haki ya kuwa na vigezo vyetu tunapochagua mwenza, kwa mfano kuzingatia bikra au historia yake ya kimapenzi (purity/no body count)?
Maanake hapa kuna mitazamo miwili ππ. Kuna wanaume wanaotanguliza bikra, wengine wanatanguliza tabia na uaminifu. Vivyo hivyo, kuna wanawake wanaotanguliza pesa, wengine wanatanguliza tabia na sifa nyingine za mwanaume.
We nae unani tag kwa lipi sasa hapa π π ππΌWewe ShesRise_1 inabidi ukubali kuwa jukumu la kujilinda ni lako peke yako. Ni nyege zenu ndo huwa zina watu a mpaka mnalala na wanaume na si vinginevyo.
Lakini pia, mwanaume kujitunza huwezi kujua kama kweli haja lala na wanawake. Kubali kuwa the burden is on you.
Nimeachana na drama, na kuongea kujifurahisha dada. Inabidi kukubali ukweli tu. Ndoa haiangalii huyu bikira au lah, na wanao wekwa ndani sio hawa tunaowapa kichwa humu na hawapo kabisaUmeanza kukua mdogo wangu
Nina Kutag ili dawa niweze kupenya zaidi mdogo wanguWe nae unani tag kwa lipi sasa hapa π π ππΌ
Huna hoja kacheze mdogo wanguNina Kutag ili dawa niweze kupenya zaidi mdogo wangu
Logically unaweza kudhani uko sawa, ila uhalisia unakupinga. Mwenye jukumu la kutunza bikira yako ni weweHuna hoja kacheze mdogo wangu
Kuna wanaume wapuuzi snJiulize na wewe mkuu π ππΌ
ukiua kwa upanga