Kihistoria, eneo lote la ilipo Israel, Gaza na sehemu ya kusini mwa Lebanon, sehemu ya Misri, sehemu ya Syria na sehemu ya Jordan, mpaka mwaka 2,500 BCE ilikuwa ni nchi moja iliyoitwa Canaan.
Wayahudi waliingia katika nchi hii kwa vita, na kuwapiga wenyeji wa maeneo hayo, canaanites, na kutengeneza tawala mbili: ISRAEL KINGDOM na JUDAH KINGDOM.
Kutokana na vita vya daima, kuanzia mwanzoni mwa karne 10, walihamia maeneo mbalimbali ya mediteranian, wengi wakiingia nchi za Ulaya, huku jamii ndogo ya Wayahudi na waarabu wakibakia kwenye maeneo yao ya asili. Wakati Wayahudi wengi waliyahama maeneo haya, waarabu waliendelea kuishi sehemu hizo hizo. Kabla ya vita kuu ya pili ya Dunia, kulikuwa na wayahudi wapatao 450,000 na waarabu wapatao 1.1m kwenye eneo ambalo leo ni Israel, Gaza na West Bank. Wakati huo eneo lote likiwa chini ya mamlaka ya Uingereza.
Baada ya vita kuu ya pili ya Dunia, idadi ya wayahudi katika eneo hili iliongezeka hadi kufikia takribani 760,000, na waarabu wakiwa 1.2m.
Kwa ufupi ni kwamba, hili eneo la Israel, Gaza na Westbank, toka kale ziliishi jamii mbalimbali pamoja, huku wayahudi wakiwa wengi, na ndio walikuwa watawala. Migration kubwa ya wayahudi ilibadilisha demography ya eneo, na kuwafanya waarabu kuwa wengi zaidi kuliko wayahudi.
Katika uhalisia, na hekima ingekuwepo, kama walivyopendekeza wayahudi mwaka ule 1947, eneo lote lilitakiwa kuwa nchi moja yenye jamii tofauti tofauti. Kwa bahati mbaya, waarabu walikosa hekima, wakaona kuwa Wayahudi hawana haki yoyote, na hawa hawakuwa waarabu wa pale Palestine, walikuwa waarabu wa mataifa ya Misri, Iraq, Jordan, Syria na Lebanon, ambao tayari walikuwa wamelimega eneo la ufalme wa zamani wa Israel na Judah.
Kwa kuzingatia mazingira ya baada ya vita vikuu vya pili vya Dunia, jibu rahisi ni kwamba, hakuna mvamizi. Waisrael ni eneo lao, na wapalestina pia. Lakini kwa vile waarabu waliukataa mgawanyo wa 1948, waliipoteza haki ya eneo walilopewa. Kwa sasa ni vyema ikawa nchi moja inayozingatia haki ya jamii zote.