Bilioni 1.6 imeibiwa ndani ya miezi miwili na Waziri wa Fedha Mwigulu yupo!

Bilioni 1.6 imeibiwa ndani ya miezi miwili na Waziri wa Fedha Mwigulu yupo!

Tunasubiri mabadiliko saa 8 usiku....Meigulu hayupo team Mama yeye ni Mataga....hakumkubali Mama kama Mwana Kamati kuu mmoja ambae amepewa RC ili kumtoa ndani CC...maana aliubgana na Bashiru kumkataa Mama....hadharani...

Mnaweza kufanya lolote. Lakini, msema kweli nauliza, nmamtoa kwa visasi hivyo ama kwa maslahi ya taifa? Bado mnataka watu wote wawe na utashi mmoja? Ni lini mlisema kutofautiana mitazamo ni uharifu? Uhuru wa watu kufanya uchaguzi na kutoa maoni yao mmeufuta kwa katiba gani?
Hapa mnajenga taifa la aina gani?
Kwamba muwe na watu wanafiki wanaosema ndiyo hata pale hawaoni ni sahihi?
Mnapeleka wapi hii nchi?

Kwa hiyo mnataka kumpoteza na weledi wake kwa sababu ya visasi binafsi?

Mwogopeni Mungu enyi binadamu msio na hisia.
 
Wizi huu umeanza kutekelezwa zaidi ya siku 50 zilizopita. Mfumo wa ulipaji serikalini hasa kwa viwango vya mamilioni kama hivi ni computerised/electronic. Kwa hivyo ni mfumo ulio wazi kwa viongozi wote wizarani kuona kinachoendelea 24x7 na kuchukua hatua proactively. Tunahitaji mawaziri wakakamavu style ya kalemani na siyo wanasiasa kama mwigulu ambao kazi yao kubwa kupiga vijembe wapinzani bungeni. The buck must stop at the minister - mwigulu nchemba.
Wangapi kati ya hao waamuzi wanapenda watu kama kalemani?
Ninaona baada ya hayati mambo ya awamu ya nne yanarudi kwa kasi na watu wote wako kumsimanga hayati. Mwogopeni Mungu mtende haki.
 
Vipi wale wanaofanya usifadi kupitia biashara ya korona? kulazimisha matumizi ya fedha za walipa kodi kununua madawa ya nchajo ya korona ambayo wanajua kabisa si ya muhimu kwa taifa letu kwa namna watu wamekuwa wakiishi nayo kama vile magonjwa mengine ya kawaida?

Vipi wale weanaotaka kuidhinisha mradi wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo mradi ambao unatekeleza kwa masharti ya azma ya china kupata maeneo ya ku ocupy katika bara la Africa?

Vipi yule mtu aliyekwenda China kuokoa mtoto wake asiuawe kwa kukutwa namadawa ya kulevya na badala yake akaweka rehani nchi yetu kwa wachina?

Hao wewe unawasemaje?
Mkuu umetumia hisia sana licha ni mawazo yako
 
Acheni kampeni za kipumbavu.
Haya madudu ndiyo yanayowafanya waandike kwamba sasa hivi wana furaha zamani hawakuwa na furaha.

Lakini sauti ya Majaliwa ina mamlaka ndani yake ndiyo maana wako bize kumfundisha rais Samia kuwa amtoe kwenye uwaziri mkuu kwa sababu eti ni masalia ya JPM!

Kwani SAMIA ni masalia ya nani?
 
Vipi wale wanaofanya usifadi kupitia biashara ya korona? kulazimisha matumizi ya fedha za walipa kodi kununua madawa ya nchajo ya korona ambayo wanajua kabisa si ya muhimu kwa taifa letu kwa namna watu wamekuwa wakiishi nayo kama vile magonjwa mengine ya kawaida?

Vipi wale weanaotaka kuidhinisha mradi wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo mradi ambao unatekeleza kwa masharti ya azma ya china kupata maeneo ya ku ocupy katika bara la Africa?

Vipi yule mtu aliyekwenda China kuokoa mtoto wake asiuawe kwa kukutwa namadawa ya kulevya na badala yake akaweka rehani nchi yetu kwa wachina?

Hao wewe unawasemaje?
huo ni uzi mwingine, Kwanza hii, miez miwili, bilioni 1.6,hii imezidi aisee,ndio maana mwendazake alikuwa anatumbua usiku wa manane.
 
Yule mama ni hopeless nishaanza kumtoa manyota. Narudia nchi hii haijawahi kuwa na viongozi wenye maono.
 
Mwigulu ni moja ya wateule hatari kwa awamu ya 6. Huyu nia yake ni ovu kwa Mh. Samia. Mwigulu Ana nguvu za majukwaani na siyo za kiutendaji. Mwigulu ni sehemu ya Sukuma gang ambayo ni kuhakikisha Mheshimiwa Rais hasongi mbele. Mwigulu target yake ni kugombea Urais 2025 na yuko busy kwa ajili hiyo tu na ili afanikiwe ni lazima kutuonyesha Mheshimiwa Rais Samia S. Hassan kuwa hawezi kitu. Mheshimiwa Rais kama una nia ya kufanikiwa tafadhali sana zingatia haya ambayo pia wengi wameshasema kwako kupitia platforms kama JF au individual:
1. Unda Serikali yako. Hao ulioazima kwa awamu ya 5 ni waimba mapambiyo na hawako kukusaidia kwa walio wengi. Ondoa wengi wao su wote na weka wa kwako. Vunja anza upya Serikali. Wanaokuzunguka kukusaidia tafakari sana.
2. Ondoa Mwigulu Nchemba Wizara ya Fedha. Wizara haiwezi na taasisi zake ni nyeti ikiwemo TRA. Hapa utashindwa vibaya mno usipokuwa makini.
3. Mawaziri wenye uzembe timua haraka mno.
4. Tumia Wanausalama waaminifu kwako wakusaidie kufuatilia kwa siri mienendo ya watendaji na wasaidizi wako. Narudia unda tume yako ya watiifu kwako kwa siri pia wakufanyie kazi. Yapo mengi utajifunza baada ya taarifa yao na kukuwezesha kufanya maamuzi haraka sana.

Tunakuombea mno Mh. Rais kwa kuwa nia yako ni njema na Mwanga tumeanza kuuona.
Mungu Ibariki Tanzania.
 
Waziri wa Fedha hii ni kashfa nzito mno, hutakiw kuitolea maelezo. Unachotakiwa ni kuwaomba radhi watanzania na kujiuzuru kiungwana kabisa na kama huwezi basi usubir rungu la mama Samia ambalo ni aibu na linakutolea credit kama mgombea urais 2025.
Kama sielewi vile, lakini waziri anatakkwa awe"eyes on hands off"ila wakulaumiwa ni Katibu Mkuu! yeye ni"Afisa Mashuhuli "
 
Hoja ni wizi ama hoja ni Mwigulu?

Wapinzani wa mwigulu naona mmepata kijisababu cha kuropokea.

Mwigulu bado yupo sana. Mind you Mwigulu atakuja kua prime minister wa nchi hii ama Rais.
Labda PM wa familia yako
 
Waziri wa Fedha hii ni kashfa nzito mno, hutakiw kuitolea maelezo. Unachotakiwa ni kuwaomba radhi watanzania na kujiuzuru kiungwana kabisa na kama huwezi basi usubir rungu la mama Samia ambalo ni aibu na linakutolea credit kama mgombea urais 2025.

Ajiuzuru ili watoto wale mawe, hili neno "KUJIUZURU" halipo kwenye kamusi ya viongozi wengi wa Tanzania.
 
Kwa uelewa wangu, na ninavyo fahamu tamaa za Mwigulu, hili jambo ana lijua, na huenda haya makundi anayonyafadhili kumpinga Mh. Rais, baadhi ya hizo pesa zime elekezwa huko. Direct or indirect.

Mwigulu anatakiwa aondoke hapo wizara ya fedha asap.

Mh. Rais watu walikutonya mapa sana kuhusu huyu mtu. He is a Snitcher.

View attachment 1801097
Mwigulu ni mtu wa blah blah tu, na nimpigaji aliyetukuka,ana kashfa nyingi sana hata kwenye biashara zake,ni kwa nini aendelee kukalia kiti nyeti mpaka sasa?
 
Wizi huu mkubwa uliofanyika Katiba Mkuu wa wizara ya fedha akiwa Doto James. Ninashauri Doto James akamatwe na afukuzwe kazi huko aliko hamishiwa soon.
Sio kweli, wizi umefanyika Hadi mwezi wa 5, na makatibu wakuu walitoka tarehe 4 April, hivyo hapo akamatwe huyu mpya
 
Mwigulu tusimchukie tuwe wawazi huyu jamaa hakuwepo wakati pesa hizi zinachotwa alikuwa hajakabidhiwa ofisi

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.
Si kweli
Mawaziri wapya wameanza kazi April 2 na wizi umeendelea Hadi mwezi wa 5
 
Kwenye mawizara na idara mbalimbali wataalamu wameshajikatia tamaa kukaa vikao vya kikazi na kitaaluma kwa kukosa facilitation ya posho, hapo wizara ya fedha watu wanakula pesa daily kwa mgongo wa posho.....tutaishia kuua nchi kwa ulafi na ubinafsi.
 
Hoja ni wizi ama hoja ni Mwigulu?

Wapinzani wa mwigulu naona mmepata kijisababu cha kuropokea.

Mwigulu bado yupo sana. Mind you Mwigulu atakuja kua prime minister wa nchi hii ama Rais.
Kama Jiwe na ukilaza wake wote alikuwa rais,sioni chochote kikishindikana ndani ya Tanzania yetu.
 
Back
Top Bottom