Bilioni 1.6 imeibiwa ndani ya miezi miwili na Waziri wa Fedha Mwigulu yupo!

Bilioni 1.6 imeibiwa ndani ya miezi miwili na Waziri wa Fedha Mwigulu yupo!

Cheo cha uwaziri ni cha kisiasa hakiangalii taaluma. Wizarani kuna watendaji ndo wataalam, kumbuka Hussein Mwinyi alikuwa waziri wa ulinzi na hakuwa mwanajeshi.
 
Waziri wa Fedha hii ni kashfa nzito mno, hutakiw kuitolea maelezo. Unachotakiwa ni kuwaomba radhi watanzania na kujiuzuru kiungwana kabisa na kama huwezi basi usubir rungu la mama Samia ambalo ni aibu na linakutolea credit kama mgombea urais 2025.
Mwigulu Nchemba njoo huku wanakusagia kunguni
 
Hapo ndo mam anapofeli kwenye kuchukua hatua ngumu
 
Mwigulu ni mwizi mno. Sijui Samia alidanganywa na nani kumuweka mtu huyu kwenye Wizara hii nyeti. Hopeless kabisa.

Harafu unawaachaje nje wezi eti kupisha uchunguzi?
 
Vipi wale wanaofanya usifadi kupitia biashara ya korona? kulazimisha matumizi ya fedha za walipa kodi kununua madawa ya nchajo ya korona ambayo wanajua kabisa si ya muhimu kwa taifa letu kwa namna watu wamekuwa wakiishi nayo kama vile magonjwa mengine ya kawaida?

Vipi wale weanaotaka kuidhinisha mradi wa ujenzi wa bandari ya bagamoyo mradi ambao unatekeleza kwa masharti ya azma ya china kupata maeneo ya ku ocupy katika bara la Africa?

Vipi yule mtu aliyekwenda China kuokoa mtoto wake asiuawe kwa kukutwa namadawa ya kulevya na badala yake akaweka rehani nchi yetu kwa wachina?

Hao wewe unawasemaje?
Acha nchi isonge kama ukujenga ukiamini mwendazake atatawala milele imekula kwenu
 
Ndo tunaambiwa wachaga ni wezi? Kila siku.. hawa ni wa wasamaria wema sio?
 
We vipi hiyo order alisoma PM bila wasaidizi angejua? Mama yuko good ndio maana hatembei na machuma.vijana wapo kazini wengine utawalipa posho
 
Na yule aliyekuwa katibu mkuu wa wizara hiyo kaopo mabilioni vipi?mwacheni mwigulu nyie sukuma gang.
 
Mhe Rais wangu, ninakusalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Kazi iendelee!

Najua Mhe Rais pengine utasema huu ni ushauri wa mitandaoni na huwezi kufanyia kazi maoni ya mitandaoni,lakini haya ndio majukwaa huru kwa 100% yanaweza kukupa ushauri mzuri kuliko wale wanaokutazazma ana kwa ana wengine waoga hawakuambii ukweli. Sasa huu ndio ukweli! Nakuomba mhe Rais pokea maoni yangu kwa mikono yote ni muhimu sana. Hii ni njia yangu sahihi maana siwezi kuja IKULU kukushauri.

Nirudi kwenye hoja,Mama tunajua ulishauriwa wakati unafanya mabadiliko ya baraza la mawaziri kuhusu uteuzi wa Ndg Dkt Mwigulu Nchemba lakini Watanzania walio wengi walikushauri kua huyu usimamizi wa Wizara hii kwake ni mgumu kutokana na kutokua makini na pia anaendekeza sana siasa, huyu ni typical politician hawezi kua msimamizi wa wizara ya fedha. Mwigulu ni tofauti na Dkt Mpango, Mpango hakuwa mwanasiasa ni mtendaji,aliteuliwa kutoka kwenye kazi za kiutendaji.

Haiwezekani kati ya miezi ambayo yeye yupo ofisini pesa zinaliwa kiasi kile asijue mpaka waziri mkuu akabaini.Waziri anafanya nini? Kuna wanaomtetea kua eti hakua waziri, yaani pesa zinapigwa mpaka mwezi huu wa May Mwigulu akiwabofisini wizarani halafu kuna watu wanatetea eti hakuwa waziri. Huu ni udhaifu mkubwa sana wa waziri na ni lazima tuwe na uchungu na taifa hili badala ya kutazama usoni.

Hivyo basi, Mhe Rais tunakuomba shughulika na hili mapema kabla halijakuletea shida, wapo watanzania wachache wenye umakini na kazi zao, siyo lazima watoke kwa wabunge waliopo, unaweza kuteua mbunge toka nafasi 2 za Rais zilizosalia. Hii wizara ni roho ya taifa, ikikwama na taifa litakwama.

Mwisho, Mhe Rais nakutakia majukumu mema sisi tupo pamoja nawe na tutaendelea kukuunga mkono na kukutia moyo kiongozi wetu.
Wewe ni msukuma.msikie Mh Mbowe mlikuwa hamuwataki wachaga na makabila mengine.mbona katibu mkuu aliyehamishiwa wizara ya viwanda na biashara kaopoa mabilioni.hatukumwona kiongozi yoyote akikemea au kuunda tume eti kwa kuwa ni mpwa wa hayati magufuli.
 
Sasa ukisema Dr. Mwingulu ndio anahusika moja kwa moja utakuwa unamwonea tuu na una chuki binafsi wewe ulitakiwa uonyeshe jinsi zilivyochukuliwa kwa kuwataja wahusika ambapo ni kosa la jinai yeye atawajibika tuu kama alijua na alihusika. Mtoto wako kukomba sukari jikoni baba anahusika vp! Labda kimalezi
 
Walioiba billion moja mnawatoa kafala , vipi walioiba bilioni 96 na bilioni 180 wakasingizia za kumtibu marehemu Jiwe , mbona mmewateua katibu mkuu na mwingine kuwa mbunge ?
 
Jamani nendeni polepole. Munaweza kupendekeza munaemuhitaji bado akashindwa kazi. Twende taratibu jaman
 
Back
Top Bottom