Wanajanvi.
Leo ni siku ya wanwake duniani, matamko mengi yametolewa na viongozi mbalimbali. Yapo yaliyoandikwa na kutangazwa na mengine yamepotelea pasipo julikana.
Hofu ya watawala siku ya leo ilikuwa je chadema na Lisu watajadili kipi na jamii itakipokeaje kwa leo. Hasa ikizingatiwa mkuu wa nchi angezungumza.
Wahafidhina wa ccm wakishirikiana na TISS Wakafikiria ili ujumbe wa Chadema usifike kwa wanancchi na kujadiliwa ipasavyo wafanyeje?? Wakaona waahirishe mechi ili kuhamisha tension kwa umma.
Wakaona waahirishe mechi ili watu wapate vya kujadili na ujumbe wa chadema usisikike. Kweli wamefanikiwa kwa kiasi kidogo japo siyo sana. Dr. Sllaa ameongea leo hakuna haija trend kivile.
Ni hivi, watawala wa ccm wanawajua watz, wanajua pia kwamba wengi ni machizi moira ( sicilia namba ya vipindi vya michezo na magazeti utagundua hilo) stories kwenye vijiwe na maongezi ya kawaida.
Kipindi cha JPM CHADEMA walitangaza maandamano ya UKUTA, Kulikuwa na mechi ya Simba na yanga. Siku ya maandamano ndo ilikuwa siku ya mechi, mball na JWTS kuamriwa wafanye usafi lakini mechi iliahirishwa kubadili upepo.
Mechi ile iliahirishwa ikachezwa siku nyingine na siku ya mechi mh. Mbowe na Mwigulu walikaa jukwaa moja na walionekana kupeaba tano wakati mechi inaendelea.
Ulishawahi kujiuliza wanaoingia uwanjani na jezi na mabango ni kina nani ?
Ukwei mchungu ila ndo hivyo dola inaogopa chadema kuliko inavyojitapa.
Tukutane mechi ya marudiano,