Bomu lalipuka kwenye mkutano wa CHADEMA Arusha, watu kadhaa wahofiwa kupoteza maisha!

Je mrusha bomu amejulikana na kukamatwa au bado policcm wamelala??????????
 
INASIKITISHA SANA

....bomu lilirushwa baada ya viongozi kushuka jukwaani na lililenga viongozi wa Chadema...
.....polisi kufika na kurusha risasi za moto.....

HAPA CCM HAMTAKWEPA....HIII DAMU MLIYOMWAGA ITAWAGHARIMU NINYI NA VIZAZI VYENU....
 
Poleni sana watu wa arusha. Mungu awayie nguvu.
 
Afadhali naona mshaanza kuelewa somo, nimepima mawazo yenu naona udini haupo tena.
Ila nna swali.!

Mbona hili kwa haraka hamjaliita kuwa ni tukio la kigaidi? Wala hakuna hata mmoja aliyelihusisha na uislamu? KUNANI?


Nyeupe itabakia kuwa nyeupe ,vivyo hivyo kwa rangi nyengine.Jitahidi sana kueneza amani na upendo kuliko chuki dhidi ya wananchi.
 

Mwigulu alisema amefuata ushindi arusha iwe kwa damu au usaha.isije kuwa ni mbinu ya kuchakachua leo usiku kucha na ukichukulia kwamba watu wameshaogopa wanaweza wasiende kupiga kura ikawa adavantage kwa akina mwigulu kufanya mambo yao.WHy kila anapoenda mwigulu kupiga kampeni vifo hutokea???? Hili jamaa lina hulka ya kifasishisti kama akina idd amini ndo maana limeanza kuvaa kama nduli.
 
Tuna habari kamili: Usalama wa taifa unahusika ili kuwaogopesha watu. Hata lile bomu la kanisani ni hao hao!
Ni fikra mgando tu ndizo zitakazo ungo unga mkono hisia zako. Jiulize kwanini yasitokee kwenye mikutano ya CUF ama CCM? Kwanini kilasiku ni CDM? Hapo utajua kunakitu nyuma ya panzia.
 
Hivi wewe mwenye alama zote za Werema(anayejiita eti naye ni mwanasheria) kwenye ubongo wakounabwabwaja nini hapa! Hujui hii ni kazi ya usalama wa taifa chini ya maagizo ya CCM?

wewe akili yako inakuambia kwamba hiyo ndiyo kazi yao؛au unaongea kwa sabu mungu amekupa uwezo wa kuongea wewe hujui kuwa ni mipango ya wanasiasa wa ajabu unaowaramba miguu mungu atawalaani tu.
 
Mkuu hapo nakupinga,kama ni magaidi basi wanatekeleza kazi ya ccm,shekhee kamwagiwa tindikali,makanisa yamepigwa mabomu na kuuwawa kwa viongozi na sasa mkutano wa chadema,no big NO hawa ni CCM TU
 


Mkuu JK
anaachia nchi kwenye machafuko mabaya akiambiwa hasikii
hii kama imetokea kwa mkutano wa chadema iweje kesho Jk anahutubia huko sumbawanga au mtwara bomu lisitupwe.



Kila mara huwa yanapigwa akiwa nje........Mtikila atabaki kuwa hero.
 

you must be very very intelligent_huwa sitokez kuchangia ingawa nashinda jf mpaka nipate kuona hoja yenye akili kama ya kwako, tatizo siasa, udini na ukanda na uroho wa kutawala vinawanyima fikra ya kufikir mambo kwa mapana_habar ya Zanzibar( padri na shekh), waandishi wa habar na Arusha(kanisan na leo kwenye kampeni)_watu hawaonekan_sio suala jepes kuwa na such vitual army, hawa ni kundi makin, well trained and organised_tunapokurupuka kwa kunyoosheana vidole, wanafurah hasa wakiamin kamwe hatuwez kuwapata_ni kweli watafanikiwa
 
Hii ni kazi ya chadema, kwa mtu mwenye akili timamu ataelewa kuwa hii itawaathiri sana ccm sasa kwanini wafanye haya maovu. Hii ni mbinu za kupata sympathy za wananchi

Mkuu nakubaliana na wewe 100% sidhani kama CCm wapo na akili ndogo namna hiyo kufanya jambo ambalo wao watakua watuhumiwa wa kwanza???
 
Mkuu,
Kumbuka bomu la kanisani, watu waliwaingiza Waislam lakini kumbe ukweli ni tofauti kabisa.

Sijui na kwenyewe ungeuliza kwanini mabomu hayalipuki kwenye misikiti?

Hili suala la mabomu ni janga la nchi nzima. Ni muhimu wote tushirikiane kuhakikisha wahusika wanakamatwa. Lakini tukiingiza itikadi za siasa au dini, kweli Tanzania yetu itaangamia.

 
Mtatupiga na kutuua, lakini watakaobaki kesho asubuhi watakwenda kupiga kura.
Huu ni uchaguzi wa diwani, kuna chaguzi zingine zinakuja, ikiwamo kura ya maoni ya katiba na uchaguzi mkuu wa 2015.
Mtaua wangapi? Kama uchaguzi wa diwani mnaanza kuua, je hizo chaguzi zingine itakuwaje?
Eleweni ya kwamba Watanzania tuko zaidi ya milioni 44, hamtatumaliza kamwe.

Tumeonewa kiasi cha kutosha,
Tumepuuzwa kiasi cha kutosha,
Tumedhalilishwa kiasi cha kutosha,
Sasa tunataka mapinduzi ili tusionewe tena!
Tusinyonywe tena!
Tusidhalilishwe tena!
Na tusipuuzwe tena!

Nendeni wapambanaji mkapige kura zenu, na mkazilinde!
 
Sasa nimeamini pasipo shaka, mauaji yote kuanzia kule Zanzibar, kanisani kule Arusha, kule Igunga, n.k. Ni CCM kwa kumtumia Mwigulu na kundi lake la wauaji ndiyo wanaohusika. CCM wanafanya mauaji na kisha kuwasingizia waislam wenye msimamo mkali.

Njia ya kukabiliana na CCM hata watudanganye namna gani, tusikubali. Ni lazima tuwaambie wazi kuwa CCM ndiyo wauaji.wakuu wa nchi hii. Hakuna cha magaidi, hakuna cha waislam.wa msimamo mkali. Magaidi na wenye msimamo mkali ni CCM. Sasa inaonekana GREEN GUARD kimekuwa rasmi kikundi cha kigaidi.

CHADEMA ITUMIE UWEZO.WAKE WOTE ILI KUIFANYA GREEN GUARD ITAMBULIWE RASMI KIMATAIFA KUWA NI KIKUNDI CHA KIGAIDI KINACHOFADHILIWA NA CCM.

Wakuu nitawapa updates soon
=====
Updates:

Mkutano ulishaisha, Mbowe akaanza kukusanya michango kama ilivyo kawaida kwa mikutano ya CHADEMA, ndipo ghafla kijana mmoja aliyekuwa amevaa kaptula ya jeans iliyoraruka kidogo akarusha bomu wakafa watatu
 
Mbunge wa iramba magharibi mwigulu nchemba amekuwa akifanya siasa chafu zenye mwelekeo wa kigaidi. Alipoongoza kampeni igunga siasa zake chafu zilisababisha mauaji. Kule arumeru akaua,ndago iramba akaua. Tangu arudi china amekuja na mbinu mpya ya kukusanya vijana wahuni kwenye makambi na kuwapa mafunzo ya kijeshi. Makambi hayo yamegundulika mbeya,arusha nk,nakuripotiwa polisi. Licha ya kupewa taarifa hizo polisi hawajachukua hatua zozote. Uzembe huu wa polisi wa kutomchukulia hatua mwigulu nchemba,ndio uliopelekea mauaji ya leo mjini arusha. Taarifa za uhakika zinathibitisha kuwa kijana alierusha bomu lililojeruhi na kuua leo arusha,ALITUMWA NA MWIGULU NCHEMBA. Tangu kuwasili kwa mwigulu mjini arusha matukio ya kujeruhiwa kwa wananchi yamekuwa yakiripotiwa. Mwigulu ni mtu hatari kwa amani ya nchi yetu. Ni vema polisi wakamkamata mwigulu awe mshitakiwa wa kwanza kwa mauaji ya arusha.
 

Kamanda mbona unawagawa wananchi unavyosema wakiristo serikalini wanawasaliti unamaanisha waamie Chadema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…