Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hao wanaomba msamaha kiaina baada ya kumpiga TUNDU Lissu.

Yaani mtu atume watu wakupige Kisha anakupoza ml 5🤔!!
 
Kwa nini ukubali pesa ya laana?
View attachment 3071048
Binafsi sioni shida. Kuna mambo unaweza kukataa, lakini kuna mambo mengine ukubali au ukatae hayana effect yoyote. Ila yakikufanya ulainike, na kuanza kuimba mapambio labda. Otherwise, mchango kama mchango sioni shida. Ni kama sadaka za kanisani zinatoka kwa watu wa makundi mbalimbali, wema na wabaya. Na hapa sina maana kwamba CCM ni wabaya na mkundi mengine ni wema, ila kwamba hatuna njia ya kumpima mtu kwamba huyu atoe sadaka na huyu asitoe. Kwa mfano, hata hizo fedha zingine zilizochangwa, kama kuna wana-CCM waliochangia Tundu Lissu atawajuaje ili awarudishie? Unaona ilivyo ngumu? Anyway, ni maoni yangu.
 
Na Lissu alisema apokee tu , watamuingiza kwenye mtego ambao kutoka ni ngumu. Maana wao target yao ni Lissu wakishampata kazi kwisha.
 
Naona doa hapa tayari, ilikuwa simple tu Lissu aseme ahsanteni kwa moyo wenu ila hizo pesa pelekeni kuweka madawati kwa watoto wanaokaa chini, hapa angekuwa amejibu vizuri sana na kupata wafuasi.

Lakini hawa CCM, ambao juzi tu wametoka kuwacharaza virungu viongozi wa Chadema kupitia polisi wao, virungu vilivyomhusisha Lissu mwenyewe, leo kutoa mchango kwa Lissu na kupokewa, hii kwangu automatically wameshajinasua kwenye ule ujinga wao waliofanya juzi kule Mbeya.

Now wakiulizwa simply watajibu Chadema ni marafiki zetu kwenye siasa, ndio maana juzi tumemchangia Lissu apate gari mpya!.

Waongo, wanalazimisha 4R kwa Lissu wakati Samia mwanzilishi ameshazipiga teke, huu mtego Lissu na Chadema wamenasa!.
 
Hii nimeipenda,na hivi ndivyo siasa inatakiwa iwe🤣🤣🤣
 
Nchimbi anataka kulazimisha urafiki wa CCM na CDM.

Awaambie Serikali waache kuwanyanyasa wanachama na viongozi kwanza. kila mtu afuate sheria.

Afu si michango tu, watueleze nani alitaka kumuia Lissu? Akamatwe na ashitakiwe kwa mujibu wa sheria.

Urafiki wa kinafiki si mzuri.
 
Vile virungu vya polisi juzi kule Mbeya kwa viongozi wa Chadema akiwemo Lissu mwenyewe ndio "urafiki" unaozungumzia hapa?!

Usituimbie ngonjera hapa wakati kule field matendo ya CCM kwa Chadema ni complete opposite.
 
Mtoa hoja, jifunze siasa. Siasa ni pana saana. Kuna watu walisema Mbowe kala asali afu leo wanajutia maneno yao.
 
Kweli kabisa, kutoka Mbeya ilibidi apate lifti ya Polisi
 
Ninakubaliana nawe sehemu kubwa.
Lakini hapo hapo elewa kwamba huko CCM siyo wote ni akina .... eeerrr-eerrr-eh, nani yule polisi anaitwa yule?

Huko ndani ya CCM sasa hivi kuna mashetani kweli kweli, wasioona kitu kingine zaidi ya kumpambania 'Chura Kiziwi'; lakini pia kuna watu wanaoweza kuaminika na kuheshimika; kama huyo Nchimbi.

Hivi kwa maoni yako, hii pesa iliyo changwa ni sawa na ile ya Abdul, ambayo Lissu amekuwa akiipigia kelele? Mimi naona tofauti kubwa.

Kiukweli, milioni tano si pesa ya kudhalilishwa nayo; kama lengo ni kufanya hivyo, Tundu Lissu aachane nayo.
 
Hongereni CCM, katika kila mkutano mumchangie, Chadema wameshindwa
 
Lissu kategwa na CCM na kapitakana kizeeeembe kwelikweli.

Kuchangiwa na CCM ni tofauti na kuchangiwa na wanaCCM mmoja mmoja!.

Poor Lissu, kaingizwa kingi kilaini. Yaani ananyang'anywa mtaji wake wa Kisiasa hivihivi.

Kama kuna mtu yupo karibu na Lissu mwambieni aache, CCM wanaenda kuitumia hiyo incidence kisiasa na itademoralize watu wenye imani naye kisiasa sana!
 
Pesa hizo hazikutoka CCM zimetoka kwa watanzania ambao hawskufurahishwa na kitendo cha serikali ya Magufuli.
 
Kuachana nayo si sahihi, hiyo pesa haijatoka kwenye mfuko wa CCM, kwani Lissu hana ndugu wanachama wa CCM, nao awakatae! Hapana.
 
Kukoswa akili bora ukose nguo.

Lisu si mpinzani uchwara kama wewe.

Hana hoja ya kubagua wa kumchangia ikiwa pesa inayotolewa si Pesa ya serkali

Siasa si uadui, ila ugomvi wetu unakuja pale mmoja anapotaka kuhalalisha haramu na kuhujumu nchi.

Dunia bado inazunguka hii tumia ubongo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…