Pre GE2025 CCM wamchangia Lissu Milioni 5 atengeneze gari lake. Lissu azipokea
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Manunuzi yapo ya siri na ya wazi

Hili la Lissu ni manunuzi ya wazi!

Hicho chama cha CCM mbona hakikuitisha harambee ya wazi kuchangia matibabu yake?
Lissu anadai bungeni mahela kibao stahiki za matibabu yake kama mbunge mbona CCM haiiagizi serikali yake kumlipa stahiki zake?

Wakati serikali ya CCM imewashushia viongozi wenzio mkong'oto na vijana kibao wa chama bado wako ndani hazijapita hata siku tatu CCM kupitia uombezi wa msaliti wa chama wanakupa hela ukanunue gari na unazipokea hizo hiyo kama siyo kukosa umakini wa kisiasa ni kitu gani?

..zoezi zima limefanyika kama KEJELI kwa Tundu Lissu.

..Lissu apokee tu huo mchango kwasababu hawezi kuzuia wana-Ccm waliokosa hoja kumkejeli.
 
CCM wanajua kucheza na mindset za watu aisee kongole! kipindi cha uchaguzi wanaona 4R Awadh kazitibua lazima juhudi zifanyike kurejesha imani

..hakuna mtu anaweza kuamini huo mchango ni kuenzi 4R.

..Ccm wamekosa hoja za kuwashawishi wananchi.
 
20240815_212711.jpg
 
Hatuzitaki lissu asipokee hii politiki ya kinafiki kinachofwata watamuuliza zile walizochangia wananchi zimeenda wapi huo ni mtego.
Chadema ni chama cha udini na ukabila

Lissu aondoke haraka aende ccm au act au cuf
 
CCM wanatamani sana kukamilisha usajili basi wa kwanza ni TL..
Dah!

Haya yatakuwa ni matamanio kama ya yule fisi aliyekuwa akifuatilia mkono wa mtu udondoke!

Labda ianzishwe CCM nyingine ambayo inaweza kumvuta Tundu Lissu, siyo hii iliyooza kiasi hiki.

Mtu anaye simamia anayo yaamini kama alivyo Tundu Lissu akijiunga na hii CCM ya 'Chura KIziwi' huo utakuwa ni muujiza wa kipekee.
 
Pokea hata kama hazitoshi hata tairi. Haujawaomba pokea na mahakamani kama kawa. Watajipendekeza sana! Hata kama mama Abdul kapitisha mlango wa nyuma chukua. Ila onyo wasitumie mchango huo kutamka kashfa tunawarudishia ndani ya masaa 6. Yule mtoto aliyechoma picha alichangiwa ndani ya masaa machache
 
Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.
Hongera lisu kwa kukubali na kupokea pesa toka ccm. Ningeshangaa kama ungezikataa, japo ingeonyesha msimamo wako wa kuichukia ccm!
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.

Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.

"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.

Mwananchi
Magazeti yaandike hivi "Walioshiriki kumuumiza LISSU, Sasa kukarabti gari lake"
 
Lissu apokee tu ila kumziba mdomo wasahau mama abdul atapashwa tu!

Lisu hajui kukaa na jambo wasidhani wamefanya la maana kwa Lissu
 
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amewaongoza wajumbe wa NEC alioongoza nao ziarani mkoani Mwanza na wanachama wa chama hicho mkoani humo wamemchangia Shilingi Milioni Tano Makamu Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu ili kufanyia matengenezo gari yake.

Kada wa CCM, Mchungaji Peter Msigwa akiwa kwenye mkutano wa chama hicho kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza alimuomba Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Nchimbi kuhamasisha wanachama wa CCM kumchangia Lissu ili gari hilo limuwezeshe kufanya shughuli za siasa.

Kwa upande wake, Dkt Emmanuel Nchimbi amesema siasa si uadui hivyo ni vyema kushikana mkono pale panapobidi kwani wanasiasa wote wanaijenga Tanzania.
Alipotafutwa kuzungumzia kitendo hicho kilichofanywa na CCM, Lissu amewashukuru CCM kwa mchango na kwamba atazipokea fedha hizo kama ambayo amekuwa akipokea kutoka kwa makundi tofauti ya watu.

"Nawashukuru, kama nilivyosema...hatukusema tunachangiwa na wanaChadema peke yao, kama nilivyotibiwa, sikutibiwa na wanaChadema peke yao. Kwa hiyo, wakichangia nitazipokea, sina sababu ya kukataa," amesema Lissu.

Mwananchi
Kiburi siku zote ni mali ya shetani lakini Mungu hukomesha kiburi
 
Mnafikiri yupo kwenye siasa kwa ajili ya kipato cha nani?
 
Back
Top Bottom