Watoa mada wengine wanaleta michango yao as if wanaishi nje ya nchi.
Kwa uchaguzi upi mpaka ukawasumbue wananchi kupanga foleni eti wapige kura wakati watu tayali wanayo matokeo,
Kwa kuenguliwa kote kwa watia nia as if kuna shule za wana ssm peke yao na za wanachadema peke yao,
Kwa uchaguzi upi wa wananchi kutekwa na kuuwawa na wasiojulikana na hakuna kesi yoyote na badala yake watu wanapandishwa vyeo,
Kwa uchaguzi upi usiokua hata na takwimu sahihi za wapiga kura,
Kwa uchaguzi upi watu wanapigwa risasi mbele za familia zao na hawakamatwi,
Kwa tume ipi ya kutenda haki,
Ni mjinga tu ndio anaweza kwenda kupanga foleni ya kupiga kura kutokana na upeo wake wa kufikiri,
MTOA MADA NYAKATI ZINGINE KABLA YA KUANDIKA MADA MTANGULIZENI MUNGU KWANZA, UNAFIKI NA UCHAWA VIACHWE NYUMA KWANZA. TUANGALIE MASLAHI YA TAIFA KWANZA NA SIO NJAA ZETU.
MIMI BINAFSI SINTAKWENDA KUPIGA KURA SIO KWA SABABU YA CHADEMA WAMESUSIA LA HASHA, SIENDI KUPIGA KURA KUTOKANA NA MFUMO WA UCHAGUZI ULIOPO