Watanzania hasa wale wapenda maendeleo ya kweli ambao Magufuli haya ndio mambo ambayo hakuwa na muda nayo.
Hivi Lissu alijianzia tu kuongelea maswala ya ‘nusu mkate’ au aliulizwa swali na mwandishi wa habari baada ya kumaliza press conference yake je CDM ikipewa nafasi ya kufanya kazi na serikali kwa utaratibu kama Zanzibar itakaa. Ndio akaanza kutoa ufafanuzi wa sheria hilo haliwezekani kwa katiba ya Tanzania na kuanza kutoa elimu ya sheria.
Huu ndio upuuzi ambao Magufuli hakuwa na muda nao, unasema ‘A’ wananchi wanasema uliongea ‘B’ huo muda wa kutoa maelezo alikuwa hana; utaelewa siku akikutumbua alimaanisha nini hasa.
Aliyoongea Lissu na tafsiri ya jamii ni tofauti kabisa na wengine wamesikiliza press conference nzima.
Ndio maana wengine tunadhani anahitajika Magufuli 2.0, lazima apatikane mtu wa kuziweka akili za watanzania zikae sawa. Huwezi kuwa na jamii ya namna hii.
Mimi binafsi uwa simkubali Lissu sehemu moja tu, pale ambapo nchi inakuwa na migogoro na watu wa nje; halafu muda huo-huo yeye analeta majungu yake dhidi ya serikali. Lakini alichoongea juzi ni kwa ajili ya kuijenga CDM hakuna sehemu aliyolenga kubomoa, labda kama watu huko Mikocheni sijui Ufipa wanajistukia tu.