CHADEMA yajibu hoja za Tundu Lissu: "Hakuna Serikali ya Nusu Mkate, Sio Sera Yetu"

CHADEMA yajibu hoja za Tundu Lissu: "Hakuna Serikali ya Nusu Mkate, Sio Sera Yetu"

Ni yeye
 

Attachments

  • LISSU.jpg
    LISSU.jpg
    338.4 KB · Views: 3
Mkuu 'Al Watani', naomba kupitia kwako nieleze kinacho nishangaza na mjadala huu wa kulaumiana, na hasa kumlaumu Tundu Lissu kama baadhi ya watu wanavyo fanya.

Kwani Tundu Lissu anafanya kosa gani hasa kukumbushia tu ulaghai na uongo mwingi ambao sasa inajulikana Rais Samia ni kinara wa mambo hayo ya kusema uongo!
Kwani Mwenyekiti Mbowe, yeye hakuweza kulaghaiwa kwa muda alio shiriki kwenye hayo yaliyo itwa "mazungumzo ya Maridhiano"? Kuna lipi la ajabu hapa.

Samia kaahidi jambo gani na lini, na kweli akafanya kama alivyo ahidi; unaweza kunipa mfano hata mmoja? Mwenyekiti Mbowe sasa hivi bado hajui kuwa zile hadaa za Mazungumzo zilikuwa na lengo maalum, badala ya kutafuta utatuzi wa maswala ya kisiasa yanayo tukabili?

Sasa Lissu akikumbushia haya, ndiyo yeye alaumiwe; badala ya chama (CHADEMA) kukiri jinsi kilivyo taka kupelekwa kwenye shimo?

Bado Mwenyekiti Mbowe na wanao muunga mkono ndani ya chama, bado wanayo matumaini ya kufikia makubaliano na Samia na chama chake? Kama sivyo, malalamiko juu ya yaliyo semwa na Tundu Lissu ni ya nini na yana faida kwa nani? Siyo CCM anaye faidika sasa hivi?
Mimi binafsi sikuamini maridhiano kama yataleta tija na sikuwa na Imani na Samia kuwa yuko genuine na alichokuwa akikisema.
Samia ana upole wa kizanzibar, Kiburi cha mwambao lakini ana ulaghai wa kiccm na ana mamlaka ya kufanya chochote anachotaka.

Mbowe na wenzake walitakiwa walisome hilo mapema kabla ya kujiingiza kwenye mazungumzo ya aina yoyote na ccm.

Turudi kwa Lissu kukikumbusha Chama chake kuwa tulipotoka kwenda kwenye meza ya mazungumzo si kosa na Wala Sina tatizo nalo.

Tatizo langu na Lissu ni yeye kuishia kuwa mlalamikaji kwa ulalamishi unaojenga taswira kuwa wenzake ndani ya Chama hawana akili na maono na kwamba wanafanya wanachofanya kwa sababu wamekula hela za Samia.

Hoja nyingine ni Lissu kutosoma mazingira ya kipi akizungumze kiimarishe taswira ya chama na kipi akiache.

Lissu tunatarajia atuuzie, maono, misimamo na mwelekeo wa Chama chake siyo kutulalamikia tu. Akumbuke kuwa nje ya chama anakuwa ni mwanaharakati tu na hawezi kufika popote.

Asikijengee taswira mbovu Chama chake wakati yeye anataka kukitumia kwenda ikulu labda Kama Hana nia hiyo.
 
Back
Top Bottom