CHADEMA yajibu hoja za Tundu Lissu: "Hakuna Serikali ya Nusu Mkate, Sio Sera Yetu"

Wakuu

CHADEMA wamemjibu Makamu Mwenyekiti wa chama chao, Tundu Lissu

=====
Hivi karibuni kumeibuka tena wimbi la hoja mbalimbali ambazo zilishawahi kuibuka siku za nyuma na ambazo zimesababisha wanachama, wapenzi wa Chadema na Wananchi kwa ujumla kutaka ufafanuzi rasmi wa Chama;

1. Chadema haijawahi kuletewa hoja ya kugawana madaraka kutoka Chama chochote au kutoka kwa Serikali wala hoja ya kupewa Majimbo ya Uchaguzi au kugawana nafasi za madaraka katika muundo wa Serikali.

Aidha, ieleweke kuwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo sasa nafasi ya Makamu wa Rais hugombewa na haitolewi mezani, vilevile nafasi ya Waziri Mkuu hutokana na Chama chenye wabunge wengi Bungeni.

2. Chadema katika vikao vyake vyote rasmi haijawahi kujadili, kutoa au kupokea mapendekezo yeyote ya kitu kinachoitwa "Serikali ya nusu mkate". Jambo hili kama linavyopotoshwa halijawahi kuwa Sera ya Chadema.

3. Chadema haijawahi kupokea wala kujadili au kubeba au kuwa na agenda na Serikali katika vikao vyote vya Chama au vile vya maridhiano kuhusu hoja hizo tajwa hapo juu.

4. Ikumbukwe kuwa vikao vyote vya maridhiano vilifanyika mwaka 2022 na vikahitimishwa 3 Januari 2023 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alizungumza na Taifa kupitia Vyama vya Siasa na Wadau mbalimbali kuondoa katazo haramu la shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano. Tarehe 30 na 31 May 2023 palifanyika vikao vya mwisho ambapo tulishindwana. Baada ya hapo hakuna kikao chochote cha siri au hadharani kimefanyika baina ya CCM na Chadema.

5. Kwa kipindi chote cha mwaka 2023 na 2024 hadi sasa, Chama kimekuwa kwenye program mbalimbali zenye lengo la kukiuhisha Chama kufuatia miaka 7 ya Chama kupitishwa kwenye "Bonde la Uvuli wa Mauti" na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mtandao na Uongozi wa Chama katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na ziara mbalimbali maeneo kadhaa ya nchi kwa ajili ya mikutano ya hadhara, maandamano, mafunzo, usajili wa wanachama kidigitali, chaguzi kuanzia ngazi za vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, Majimbo, Wilaya, Mikoa hadi Kanda. Chaguzi hizi za ndani zitahitimishwa na Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama.
Pia, Soma:
+ Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM
Inasemekana hiyo barua ya Mrema ni FEKI
 
Chama hakijapasuka aliyepasuka ni yule aliyejifanya TID.
 
Chadema wanasema " nusu mkate" maneno ambayo hayana maana yoyote isipokuwa kuonyesha kwamba hawataki Umoja katika Chama chao.
Siyo hivyo tu,yule Katibu kule Arusha anaulizwa,"Vipi jana usiku pale tuliona kama kuna vurugu kidogo", anasema,"Hakuna vurugu,ila wahuni wachaxhe walikuwa wanaleta fujo."
Sasa adui wao ni CCM , lakini sasa hivi sijui wanagombana na nani.
As I see it hapa,hakuna tatizo lolote. Hawa watu waungane wafanye hii kazi yao.
Wanabishana kuhusu nani atagombea urais. Why?
Anayefaa kugombea urais wataambiwa na TWAWEZA.
Lilian atawaambia.
 
Sheida yake ni nini? Ni kukalia kiti tu au kuna mengine zaidi?
Kwakwel siwez eleza kiundani lakin sasa kama ni wewe tu unalalmikiwa na ni wewe tu unagombana na watu kila siku, wao wakionekana ndio wenye makosa na wewe uko sahihi always, hii inaleta walakini kidogo mkuu!. Au wewe unaonaje?
 
Tamko hilo la Kigaila halina thamani yoyote zaidi ya karatasi lilipo chapishwa.
Maelezo yote hayo ya taratibu za chama na vikao, n.k., hayana maana yoyote katika enzi hizi za watawala kufanya lolote wanalo taka lifanyike.

Kwa mfano: Andiko hilo limezungumzia chochote kuhusu wabunge 19 toka CHADEMA walivyo ingia Bungeni na bado wanaendelea kutumika huko?

CHADEMA chini ya uongozi huu na wao sasa hawapishani sana na CCM kwenye udanganyifu.
 
Wakuu

CHADEMA wamemjibu Makamu Mwenyekiti wa chama chao, Tundu Lissu

=====
Hivi karibuni kumeibuka tena wimbi la hoja mbalimbali ambazo zilishawahi kuibuka siku za nyuma na ambazo zimesababisha wanachama, wapenzi wa Chadema na Wananchi kwa ujumla kutaka ufafanuzi rasmi wa Chama;

1. Chadema haijawahi kuletewa hoja ya kugawana madaraka kutoka Chama chochote au kutoka kwa Serikali wala hoja ya kupewa Majimbo ya Uchaguzi au kugawana nafasi za madaraka katika muundo wa Serikali.

Aidha, ieleweke kuwa kwa mujibu wa Katiba iliyopo sasa nafasi ya Makamu wa Rais hugombewa na haitolewi mezani, vilevile nafasi ya Waziri Mkuu hutokana na Chama chenye wabunge wengi Bungeni.

2. Chadema katika vikao vyake vyote rasmi haijawahi kujadili, kutoa au kupokea mapendekezo yeyote ya kitu kinachoitwa "Serikali ya nusu mkate". Jambo hili kama linavyopotoshwa halijawahi kuwa Sera ya Chadema.

3. Chadema haijawahi kupokea wala kujadili au kubeba au kuwa na agenda na Serikali katika vikao vyote vya Chama au vile vya maridhiano kuhusu hoja hizo tajwa hapo juu.

4. Ikumbukwe kuwa vikao vyote vya maridhiano vilifanyika mwaka 2022 na vikahitimishwa 3 Januari 2023 ambapo Rais Samia Suluhu Hassan alizungumza na Taifa kupitia Vyama vya Siasa na Wadau mbalimbali kuondoa katazo haramu la shughuli za kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano. Tarehe 30 na 31 May 2023 palifanyika vikao vya mwisho ambapo tulishindwana. Baada ya hapo hakuna kikao chochote cha siri au hadharani kimefanyika baina ya CCM na Chadema.

5. Kwa kipindi chote cha mwaka 2023 na 2024 hadi sasa, Chama kimekuwa kwenye program mbalimbali zenye lengo la kukiuhisha Chama kufuatia miaka 7 ya Chama kupitishwa kwenye "Bonde la Uvuli wa Mauti" na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mtandao na Uongozi wa Chama katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na ziara mbalimbali maeneo kadhaa ya nchi kwa ajili ya mikutano ya hadhara, maandamano, mafunzo, usajili wa wanachama kidigitali, chaguzi kuanzia ngazi za vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, Majimbo, Wilaya, Mikoa hadi Kanda. Chaguzi hizi za ndani zitahitimishwa na Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama.
Pia, Soma:
+ Benson Kigaila: Yeyote akisema hatukujiandaa na uchaguzi anafanya kazi ya CCM
Hawa uwezo wa kuongoza nchi hawana. Warndelee kujifunza kwanza.🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hoja Dhaifu sana chadema wameingia mtegoni:
-Suala la kuahidiwa Vyeo hilo halipingiki ata katiba isingefuatwa wangepewa kwani saizi katiba haifuatwi...
-Suala la Rushwa hilo lipo wazi kuna watu wana Ramba asali.
-Pia hawakujiandaa vizuri na uchaguzi ni kweli Wajipange Upya..

KIUFUPI MHE:TUNDU ANTIPHAS LISSU
Ameongea vizuri na yupo sahihi Kama vipi aanzishe chama chake nipo tayari kujiunga mapema sana..
 
Anaivuruga Chadema wala sio CCM. Anayeivuruga ni Kiongozi anaiongelea Chama chake vibaya nje ya vikao rasmi vya Chama. Kama harithiki na kinachofanyika chamani si aondoke kama wengine walivyofanya, kama harithiki na kundi ulilopo unaachana nalo na si kupiga kelele na upo nao. Narudia tena CCM Chini ya Mama Samia Suluhu Hassan ni waungwana sana. Wanasemwa vibaya tena kwa dharau na wamekuwa waungwana. Vile vile huwezi hata mara moja kuendesha Chama cha Siasa kiuharakati lazima ufuate miongozo ya Uongozi wa vyama vya siasa chini ya Msajili wa vyama vya siasa.
 
5. Kwa kipindi chote cha mwaka 2023 na 2024 hadi sasa, Chama kimekuwa kwenye program mbalimbali zenye lengo la kukiuhisha Chama kufuatia miaka 7 ya Chama kupitishwa kwenye "Bonde la Uvuli wa Mauti" na hivyo kuathiri kwa kiasi kikubwa mtandao na Uongozi wa Chama katika ngazi mbalimbali kuanzia kwenye Vitongoji, Mitaa na Vijiji. Shughuli zilizofanyika ni pamoja na ziara mbalimbali maeneo kadhaa ya nchi kwa ajili ya mikutano ya hadhara, maandamano, mafunzo, usajili wa wanachama kidigitali, chaguzi kuanzia ngazi za vitongoji, Mitaa, Vijiji, Kata, Majimbo, Wilaya, Mikoa hadi Kanda. Chaguzi hizi za ndani zitahitimishwa na Uchaguzi Mkuu ndani ya Chama.
Uongozi wa CHADEMA hapo Makao Makuu ya chama na hata Mwenyekiti wa chama; kitu mlicho fanikiwa kukiigiza toka CCM ni njia zao za udanganyifu na hadaa; lakini hamkujifunza kwa ukamilifu zaidi miundo na mbinu kama walizo nazo CCM kuendelea kuwa madarakani kama walivyo jipanga huko mitaani/vitongojini.

Mlicho jifunza ni kutumia njia za udanganyifu ndani ya chama ili muendelee kubaki madarakani ndani ya chama; kwa manufaa ya CCM.

Hovyo Kabisa!
 
Ndugu zangu wachaga Wana tabia ya kumiliki , Mbowe amaeona amiliki Chama Cha siasa kama private co.

Mrema na TLP
Mbatia na Nssr
Mbowe na Cdm
 
1. Chadema haijawahi kuletewa hoja ya kugawana madaraka kutoka Chama chochote au kutoka kwa Serikali wala hoja ya kupewa Majimbo ya Uchaguzi au kugawana nafasi za madaraka katika muundo wa Serikali.
Kachelewa sana kujibu hoja. Watu wameshaamini yaliyotolewa kinywani mwa kiongozi namba 2.
Sasa hivi tunahangaika na uchaguzi wa ndani huko kwa Godbless Lema. Longido Oyeeeee.
Lema kama katumwa au kafanya mwenyewe kitaeleweka tu. Moto hauzimiki kwa kumwaga petroli.
 
Inavyoonekana Kuna mvurugano ndani ya Chadema. Kiini cha kuwepo kwa mvurugano huu huko Chadema kwa maoni yangu ni kutokana na namna Mwenyekiti wa Chama chao hicho Freeman Mbowe kukosa misimamo inayoeleweka kuhusiana na Siasa za nchi hii kwa sasa. Siyo siri hata kidogo, Mbowe akiwa Kama Kiongozi wa Chama Chao hicho, amekuwa ni mtu ambaye Hana msimamo unaoeleweka hali hii imesababisha mkwamo na kuyumba kwa Wanachama wa chama hicho.

Mbowe amekuwa ni mtu asiyeaminika tena kwa sasa ndani ya Chama Chao hicho, watu wengi kwanza wanamchukulia kama ni Mamluki wa Chama tawala ambaye amejipachika kwenye Vyama vya upinzani kwa 'kazi maalumu ya kuvuruga vyama vya upinzani' ili kukinufaisha chama tawala.

'Engine' ya treni ikiharibika mabehewa yote ya treni nayo huyumba na kusimama!
Bora mabehewa yayumbe na treni isimame kuliko kumuachia usukani mropokaji Lissu, atapindua treni moja kwa moja na itakuwa ndio mwisho wa safar.
 
Back
Top Bottom