CHADEMA yajibu hoja za Tundu Lissu: "Hakuna Serikali ya Nusu Mkate, Sio Sera Yetu"

Shida hiyo ya uelewa mdogo wa jamii ambao ndiyo wapiga kura wake anatakiwa aufahamu na aepuke kukiingiza Chama chake kuandikwa vibaya kwenye media.

Tundu Lissu anatakiwa aelewe kuwa media zote huwa zinaandika habari mbaya za CHADEMA hawajishughulishi na habari nzuri.

Lissu kama angeongelea Uchaguzi tu na Mambo mengine ya kitaifa hakuna chombo Cha habari kingeandika au kufuatilia ndiyo maana wametwist context ya kile alichokizungumzia.

Hata hili Lissu halielewi ?
 
Lissu atafute mshauri mzuri wa siasa.
 
Na ndicho alichoongelea uchaguzi tu, tena wa Ikungi kwa sehemu kubwa, huko inaonekana ndiko alipokuwa anajua nini kimejiri.

Hayo mengine yote yanayo trend msingi wake ni majibu ya maswali aliyoulizwa na media baada ya kumaliza kuongea alichowaitia kulikuwa na maswali matano. Baadhi ya maswali aliyoulizwa.

1. Vipi umesema serikali imecheza foul CDM mna mpango gani mtakubali hii hali au mna mpango mwingine?
Ndipo alipotoa majibu ya siku chache zilizobakia na changamoto za appeal yenyewe (akahitimisha) aoni njia nyingine ya kuwarudisa hao wagombea hasa upande wa Ikungi.

NB; Ndio maana Mchengerwa na Nchimbi wakajitokeza kijibu.

2. Wengine wakauliza nusu mkate ndio akatoa maelezo hilo linawezekana kwa katiba ya Zanzibar tu

3. Wengine wakauliza vipi rushwa, je watu wameharibu form makusudi. Ndipo alipoelezea hana ushahidi huo, ila possibility hiyo ipo
kama yeye alifuatwa seuse huko mtaani.

Press conference ipo YouTube hakuna sehemu Lissu alipokisema chama chake vibaya, hayo yote yanayo-trend msingi wake ni kwenye kujibu maswali aliyokuwa anaulizwa mwishoni. Ni watu tu wana twist hivyo vitu anavyoshutumiwa navyo wakati yeye alikuwa anaongea katika context nyingine kabisa. .

Hakuna sehemu kakisema vibaya CDM ni watu tu huko walipo wanajistukia.
 
Mmh!!ngoja tuone Kama Kuna ukweli utajulikana,lkn tuwaombee waendelee kudumu wawe na umoja,na wasitetereke Kwa namna yoyote ile,bado twawahitaji saana,hakuna mbadala wenu kwa Sasa.
 
Tindo brazaj ....

econonist
 
Mkuu 'Al Watani', naomba kupitia kwako nieleze kinacho nishangaza na mjadala huu wa kulaumiana, na hasa kumlaumu Tundu Lissu kama baadhi ya watu wanavyo fanya.

Kwani Tundu Lissu anafanya kosa gani hasa kukumbushia tu ulaghai na uongo mwingi ambao sasa inajulikana Rais Samia ni kinara wa mambo hayo ya kusema uongo!
Kwani Mwenyekiti Mbowe, yeye hakuweza kulaghaiwa kwa muda alio shiriki kwenye hayo yaliyo itwa "mazungumzo ya Maridhiano"? Kuna lipi la ajabu hapa.

Samia kaahidi jambo gani na lini, na kweli akafanya kama alivyo ahidi; unaweza kunipa mfano hata mmoja? Mwenyekiti Mbowe sasa hivi bado hajui kuwa zile hadaa za Mazungumzo zilikuwa na lengo maalum, badala ya kutafuta utatuzi wa maswala ya kisiasa yanayo tukabili?

Sasa Lissu akikumbushia haya, ndiyo yeye alaumiwe; badala ya chama (CHADEMA) kukiri jinsi kilivyo taka kupelekwa kwenye shimo?

Bado Mwenyekiti Mbowe na wanao muunga mkono ndani ya chama, bado wanayo matumaini ya kufikia makubaliano na Samia na chama chake? Kama sivyo, malalamiko juu ya yaliyo semwa na Tundu Lissu ni ya nini na yana faida kwa nani? Siyo CCM anaye faidika sasa hivi?
 
Mbowe uwa anatumiwa na CCM
 
Kuna wasomaji na wachangiaji wengi sana ndani ya jukwaa hili la Siasa wange faidika sana na uchambuzi wako huu wa kueleza hatua kwa hatua alicho zungumzia Tundu Lissu na kwa nini alikizungumzia. Hili ni somo zuri sana kwa wengi.

Tundu Lissu hakuitisha mkutano na waandishi wa habari, akiwa na ajenda ya kukishutumu chama chake na viongozi wenzake.
Lakini mjadala sasa umegeuka (bila shaka kwa kuchochewa na mashabiki wa CCM), ionekane kwamba Tundu Lissu ndiye kaanzisha mtafaruku.

Mbaya zaidi, viongozi wa CHADEMA (Sekretariati); kwa kutoa majibu kwa alicho sema Tundu Lissu, ndio sasa wamechochea mtafaruku usio kuwa na maana yoyote.
 
Kwa namna hiyo, Tundu Antipas Lissu, hatakiwi CHADEMA.

Barua hiyo ni Sehemu bya mpango MKAKATI WA CHADEMA wa kushirikiana na CCM, kumvuruga Lissu na Chama.

Sioni Tena, ni wakati wa kugawana Mbao na Fito sasa.

Kigaila, ni tone tu ndani ya CHADEMA, hawezi kumshambulia Lissu bila maelekezo.

KWAHERI YA KUONANA CHADEMA!!
 
Sasa tunaanza kujuwa ni viongozi wapi ndani ya CHADEMA wanafanya kazi ya CCM.

Huyu mwandishi wa barua hii anayo mamlaka ya kuisemea CHADEMA juu ya jambo lolote bila ya kuhusisha viongozi wengine ndani ya chama kujadili na kuamua jinsi ya kujibu?
 
Mbowe uwa anatumiwa na CCM
Hiki kitu wengi wetu tulipokua tunaambiwa miaka kadhaa nyuma tulikua tunaweza hata kukupiga mawe, kilikua hakiingii akilini lakin kwasasa tumeanza kuona na kuamino hivyo.
Kwakifupi Mama Samia ka expose vibaya sana cover ya mbowe hapo Lumumba!.
 
Mm nakuambia wewe una akili ndogo ununaita watu wamekimbia umande. Hicho unachoita mwenyekiti wa kudumu kimeandikwa ibara ya ngapi ya katiba ya chadema?
Unaropoka kila linalokujia ili mradi uchafue watu kwa faida ya nani?
Unapofuta Ibara inayozungumzia ukomo wa uongozi na ku-replace kwa ibara isiyo na ukomo wa uongozi tafsiri yake ndo hiyo! Unatengeneza mazingira ya kuwa na Mwenyekiti wa Kudumu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…