CHADEMA yajibu hoja za Tundu Lissu: "Hakuna Serikali ya Nusu Mkate, Sio Sera Yetu"

Mimi binafsi sikuamini maridhiano kama yataleta tija na sikuwa na Imani na Samia kuwa yuko genuine na alichokuwa akikisema.
Samia ana upole wa kizanzibar, Kiburi cha mwambao lakini ana ulaghai wa kiccm na ana mamlaka ya kufanya chochote anachotaka.

Mbowe na wenzake walitakiwa walisome hilo mapema kabla ya kujiingiza kwenye mazungumzo ya aina yoyote na ccm.

Turudi kwa Lissu kukikumbusha Chama chake kuwa tulipotoka kwenda kwenye meza ya mazungumzo si kosa na Wala Sina tatizo nalo.

Tatizo langu na Lissu ni yeye kuishia kuwa mlalamikaji kwa ulalamishi unaojenga taswira kuwa wenzake ndani ya Chama hawana akili na maono na kwamba wanafanya wanachofanya kwa sababu wamekula hela za Samia.

Hoja nyingine ni Lissu kutosoma mazingira ya kipi akizungumze kiimarishe taswira ya chama na kipi akiache.

Lissu tunatarajia atuuzie, maono, misimamo na mwelekeo wa Chama chake siyo kutulalamikia tu. Akumbuke kuwa nje ya chama anakuwa ni mwanaharakati tu na hawezi kufika popote.

Asikijengee taswira mbovu Chama chake wakati yeye anataka kukitumia kwenda ikulu labda Kama Hana nia hiyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…