MwajabuOmary
JF-Expert Member
- Jul 11, 2013
- 384
- 418
SUSIA SUSIA Vs MABAVU MABAVUSalama wana bodi.
Tangu kuondoka kwa Dr Slaa ,Chadema haina ubunifu wala mvuto kwa wananchi tena. Hela walizokuwa wanapata kutoka kwa wafadhili zimekatika, chama kina njaa kali lakini ukweli huu hausemwi!!.
Mathalani wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema mkoa wa Kilimanjaro hawakuweka mawakala na alipoulizwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Kilimanjaro kwa nini chama hakiweki mawakala? Alisema Chadema hakina pesa ya kuwalipa mawakala shs 5000 kwa kila siku kwa siku 30 za uandikishaji!
Freeman Mbowe baada ya kuona maji ya shingo, sasa amekuja na mbinu mpya kugomea kushiriki kila uchaguzi ulio mbele yake na akiulizwa anasema ,sababu ni ubinywaji wa democrasia wakati si kweli. Ukweli ni kwamba chama hakina pesa..
Hata mchakato wa ndani wa chama kutafuta wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema haikufanya.!!View attachment 1256773
Wa ubunge pia watajitoa. Tu beti!!!
Wamechelewa sana. Tuliwaambia wahimize watu wasijiandikishe, wao wakahimiza waende kujiandikisha. Hawa jamaa sijui kwa nini ni wagumu sana kuona hali halisi.
Naona Channel ten kimekua chombo cha ccm, Chadema kujitoa ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji sio habari. Lkn taarifa ya katibu mwenezi kuwaambia wapinzani ni wajinga hiyo ndio habari. Mahali tulipofikia ni hatari sana kwani vyombo vya habari navyo vimeufyata
Duh,samahani kiongozi uko Tanzania au nje ya Tanzania?Kwani hata kama mngeshiriki mgeshinda? Mmekimbia aibu ambayo mngepata, hamna lolote
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili
Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma
Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Pia soma
Uchaguzi S/Mitaa 2019: Wagombea wa Upinzani asilimia kubwa wameenguliwa kugombea, CCM wengi wapitishwa
Huyo anayeandika "Amekizi vigezo" ni mtumishi anayelipwa na serikali?!www.jamiiforums.com
Haya maamuzi sahihi ila yamechelewa sana,sijui hata mlipopanga kushiriki mlikuwa mnafikiria nini.
Huwezi kufanya siasa na mtu asiyetayari kushindwa.