Salama wana bodi.
Tangu kuondoka kwa Dr Slaa ,Chadema haina ubunifu wala mvuto kwa wananchi tena. Hela walizokuwa wanapata kutoka kwa wafadhili zimekatika, chama kina njaa kali lakini ukweli huu hausemwi!!.
Mathalani wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema mkoa wa Kilimanjaro hawakuweka mawakala na alipoulizwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Kilimanjaro kwa nini chama hakiweki mawakala? Alisema Chadema hakina pesa ya kuwalipa mawakala shs 5000 kwa kila siku kwa siku 30 za uandikishaji!
Freeman Mbowe baada ya kuona maji ya shingo, sasa amekuja na mbinu mpya kugomea kushiriki kila uchaguzi ulio mbele yake na akiulizwa anasema ,sababu ni ubinywaji wa democrasia wakati si kweli. Ukweli ni kwamba chama hakina pesa..
Hata mchakato wa ndani wa chama kutafuta wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema haikufanya.!!
View attachment 1256773