CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Naona Channel ten kimekua chombo cha ccm, Chadema kujitoa ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji sio habari. Lkn taarifa ya katibu mwenezi kuwaambia wapinzani ni wajinga hiyo ndio habari. Mahali tulipofikia ni hatari sana kwani vyombo vya habari navyo vimeufyata
 
Salama wana bodi.

Tangu kuondoka kwa Dr Slaa ,Chadema haina ubunifu wala mvuto kwa wananchi tena. Hela walizokuwa wanapata kutoka kwa wafadhili zimekatika, chama kina njaa kali lakini ukweli huu hausemwi!!.

Mathalani wakati wa kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema mkoa wa Kilimanjaro hawakuweka mawakala na alipoulizwa mwenyekiti wa chadema mkoa wa Kilimanjaro kwa nini chama hakiweki mawakala? Alisema Chadema hakina pesa ya kuwalipa mawakala shs 5000 kwa kila siku kwa siku 30 za uandikishaji!

Freeman Mbowe baada ya kuona maji ya shingo, sasa amekuja na mbinu mpya kugomea kushiriki kila uchaguzi ulio mbele yake na akiulizwa anasema ,sababu ni ubinywaji wa democrasia wakati si kweli. Ukweli ni kwamba chama hakina pesa..
Hata mchakato wa ndani wa chama kutafuta wagombea kwa ajili ya uchaguzi wa serikali za mitaa chadema haikufanya.!!View attachment 1256773
SUSIA SUSIA Vs MABAVU MABAVU
 
Ninachokiona kilichokuwa kikitafutwa ni sababu ya kuonekana. Na wamecheza vizuri na muda.
Maeneo yaliyotokea sintofahamu ya kukatwa majina hapo hapo media zimetangaza na baadhi ya magazeti tumeona.
Wakati hili halijakaa kinaitwa kikao cha dharura kujadili hii sintofahamu.
Hapo hapo azimio la kujitoa kwenye uchaguzi.
Time management
Wamechelewa sana. Tuliwaambia wahimize watu wasijiandikishe, wao wakahimiza waende kujiandikisha. Hawa jamaa sijui kwa nini ni wagumu sana kuona hali halisi.
 
Kipanya kibonzo cha kesho sijui kitakuwaje?
 
Hongereni sana CHADEMA kwa uamuzi huu. Waache washiriki wenyewe. Afu cha kushangaza ikifika uchaguzi watawashindisha baadhi ya wapinzani ili ionekane nao walishiriki
 
Acha chuki bhana, kwa hiyo unawapangia cha kutangaza. Kama reporter wao hakuwapo.
 
Habari wakati wanywa mbege walijulikana kuwa watasusia tu
Naona Channel ten kimekua chombo cha ccm, Chadema kujitoa ktk uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji sio habari. Lkn taarifa ya katibu mwenezi kuwaambia wapinzani ni wajinga hiyo ndio habari. Mahali tulipofikia ni hatari sana kwani vyombo vya habari navyo vimeufyata
 
Bora tumejitoa haya ccm jitangazieni ushindi nchi nzima msilojua ndio mwazidi pandikiza chuki na kuukuza upinzani Mara 3 ya ilivokua 2015
 
Safi sana,naunga mkono uamuzi mzuri huu,Waache CCM wajitekenye na kucheka
 
Msiwage mnaunga mokono mapema mtu muovu hawezi badirika, tulikataa kwenda kujuandikisha mkatuhimiza sasa yako wapi. Mwizi ni mwizi tu bado muuawe na kufungwa kunawangoja.
Maagizo wanaagiza watu wao wanasimamia tumekwisha na haachii atatawala miaka 20
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ametangaza chama chake kutoshiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 kwa madai wakishiriki wanahalalisha ubatili

Maamuzi hayo yanakuja ikiwa ni baada ya Wabunge wa CHADEMA kukutana leo alasiri Novemba 7, 2019 katika Kikao cha Kamati Kuu ya dharura ya chama kilichofanyika mkoani Dodoma

Jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano, Itikadi, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema Kamati hiyo itakutana leo kutoa msimamo wao wa mchakato wa Uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia soma

Saafi
wawachie wenye waliojiandaa. Wenyewe waendelee na uchaguzi wa Mwenyekiti wao.
 
Haya maamuzi sahihi ila yamechelewa sana,sijui hata mlipopanga kushiriki mlikuwa mnafikiria nini.

Huwezi kufanya siasa na mtu asiyetayari kushindwa.

Uko sahihi ila ujue ilikuwa lazima kukusanya ushahidi na sababu za uhakika kusimamia maamuzi ya kujitoa
 
Back
Top Bottom