CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Kuna uzi niliuna jana hapa jukwaani kwamba polepole angeongea na vyombo vya habari.

Kuna chochote cha maana kasema?
 
Mazingira sio wezeshi hii imeepusha mambo mengi Sana .mazingira yawekwe sawa .
 
Natoa pongezi kwa CHADEMA kujitoa maana kushiriki ktk kitu kinacho nasibishwa na uchaguzi ni kuwadanganya wananchi na jumuiya ya kimataifa kuwa kuna kitu kinachoitwa uchaguzi huru na wa haki nchini Tanzania chini ya utawala huu wa awamu ya tano.

Kujitoa kwa chama hiki makini cha upinzani kitapelekea Tanzania kuzidi kumulikwa kwa kurunzi ya watetezi wa demojrasia nchini na kimataifa inayopima kama kweli demokrasia ya vyama vingi ipo au la Tanzania.

Hatua hii ni Mbinyo mmojawapo kwa utawala huu kutambua kuwa haiwezi kuwaburuza wananchi kwenda ktk sanduku la kura kisa kuwapatia nguvu batili utawala wa awamu ya tano kujitangaza imewekwa mamlakani kidemokrasia wakati siyo kweli.

Turejee Kesi ya makada wa CCM kusimamia chaguzi
10 May 2019
Mahakama Kuu nchini Tanzania kanda ya Dar es Salaam imesema sheria ya uchaguzi inayowapa uhalali wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ni batili, na hivyo imetamka kuvifuta vipengele viwili katika sheria hiyo.
Source: DW Kiswahili
 
Ambacho wamesahau ni kuwa vyama vingine hasa ACT vinaona hii ni fursa kwao kujiimalisha na kuja kuwa chama kikuu cha upinzani

Vita ya mbowe na zito hapa zito ndio atakuwa mshindi japo ni snitch
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani sasa
 
Kumbe ndio maana hata kujiandikisha hawakutoa hamasa...
 
Tulishajua kuwa hawana uwezo wakushinda Si waliwahamasisha pia wanachama wao kupitia mitandao ya kijamii wasijiandikishe? Sasa walianza je kushiriki?
 
Naona hapa kinachoenda kutokea ni mabaki ya CCM kwenda kwenye vyama vingine na kugombea huko.
 
Na huu ndio mwisho wa CHADEMA Tz
 
Sasa vyama vingine ACT, NCCR nk vitangaze kujitoa ili hata upinzani CCM B kama CUF, TLP na UDP vikiungana na mume wao CCM hata wakiendelea shauri yao.
Chadema imefanya vizuri kusubiri hadi hatua hii ili ushahidi wa uzandiki wao uwe wazi
Nyama vingine sio mali ya mtu binafsi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…