CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

‪Mbona WAMENUNA? Maana Nilitegemea LEO wale waliokuwa wanashangilia wagombea wao kupita bila kupingwa ndio wangegalagala chini kabisa kwa FURAHA, kwani tumewaachia Mitaa,Vijiji na Vitongoji vyote, ‬
‪Haya Sasa WATENDAJI tokeni uko MAFICHONI mkaendelee na KAZI na Muwashe SIMU zenu🤪‬
 
Haya mambo mnayafurahia ila mwisho wake ni mbaya sana kwa CCM.
Dhambi hii haiwezi kuwaacha salama, kitakachowakuta ni kugawanyika wenyewe kwani hata 2020 mtakuwa na timu ndani ya CCM na uchaguzi ukiisha mtaanza kunyoosheana vidole wenyewe msijue adui yenu ni nani na hapo ndio maandiko yatatimia.
Mmeshindwa kushindana..sasa mnaombea adui mabaya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jafo anashangaa nini?
Walikuwa na muda wa kuweka mambo sawa na watendaji wasifunge ofisi zao. Muda wa yeye kucheza sindimba na kufurahia.
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani sasa
 
Afadhali wametuokolea mda na gharama japo hizo gharama sijui km zitarudishwa serikalini.
Lkn gharama na hasara ya chadema kujitoa ni kubwa kwa baadae kuliko ambavyo ingeshiriki lkn hii dhana inahitaji kwa mtu mwenye jicho la mwewe ndio ajue ninamaanisha nini,

Wewe unaona hilo cdm haifi siku yatakapo kupata kisu cha ma t ko kikikuingia akili itakukaa viziri
 
Well said kuna ushahidi wa kutosha na sababu za kutosha watu kujibu kisasi watakavyo ,kijani hakitavalika mtaani, sitarajii yeyote kushangilia ushindi feki.
Hapo ndipo pa kumpima zito
 
Mmeshindwa kushindana..sasa mnaombea adui mabaya [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Ndio itakavyokua, nafasi za uongozi Zitageuka dili CCM Mwishowe wanayofanyiwa wapinzani wataanza Kufanyiana wenyewe.
 
Leo nilikuwa msibani na wananchi wa kawaida. Kimsingi wengi wamepobgeza masmuzi ya CHADEMA, hadi Viongozi walioteuliwa kutoka CCM. Tayari wana hofu na kilichofanyika kwamba kitaathiri maisha YAO na mahusiano. Hawana Amani kabisaaaaaa. Sijui tuendako
 
jaffow ni mpuuzi kama walivyo wapuuzi wengine,,
 
Waswahili husema kufa kufaana baada ya chama kikuu cha upinzani nchini kujitoa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa kimetoa fursa kwa chama cha ACT wazalendo kuimarika zaidi.

Maana yake ni kwamba kwa sasa Chadema itakosa uwakilishi katika serikali za mitaa jambo ambalo ni hatari sana kwa ustawi wake.

Nina imani Zitto na maalimu Seif hawatasusia uchaguzi ila watapanga mbinu muafaka za kumkabili mwenzao waziri Jafo kwenye uwanja wa uchaguzi kwani waswahili wanasema.......Waarabu wa Pemba hujuana kwa vilemba.

Poleni sana Chadema

Maendeleo hayana vyama!
Mbona hueleweki mkuu?
Au hujui kuwa hata wagombea wa ACT- Wazalendo nao wamekatwa?
Sasa hao ACT- Wazalendo watang'aa vipi bila ya kuwa na wagombea!
 
Ila hii strategy ya kususa imefeli miaka yote!

Kwa nini msibadilishe action plan?

Dhulma ya wazi kabisa imetendeka hapa si kwa CDM tu.

It's high time now mtoke nyuma ya keyboards tuone ukamanda wenu.
 
Back
Top Bottom