CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Hahahaaa.......!

Chadema bhana washaanza kujibiwa!

Anyway wananchi watawakilishwa na yoyote atakayeshinda hiyo ndio demokrasia!
Demokrasia ya CCM, kwa ambayo lazima wao washinde hata kwa goli la mkono.
 
Mwerevu akiona hatari ukimbia na kujificha bali mpumbavu ukimbilia maovu, wametumia hekima na ushaidi wanao.
 
Rufaa zote zimetupwa, hata waliojisahau wakawapitisha wanawekewa mapingamizi, wajumbe wa rufaa unawajua?? Acha tu. Km nawe ni CCM bado furahini ktk HUZUNI. So tar 24/11 asubuhi tusio na vyama church then home kimyaaaaa!!
Nadhani viongozi wa chadema wameongeza chuki zaidi baina ya wananchi kuliko ccm,kwa sababu muda wa rufaa huu ungefaa sana kwa mazungumzo kuona kwanini wameenguliwa kuona uhalali na ubatiri na baadae ndo maamuzi yangefuata.
 
Kushiriki huu uchaguzi inapaswa uwe na kichwa maji.naunga mkono.hatua inayofuata chadema waanze kudai katiba mpya na ikiwezekana maandamano.Ni bora tuanze upya....
 
Walioenguliwa ni wale tu wenye mapungufu kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi.

Sio kwa mujibu wa wasimamizi wa uchaguzi, bali kwa maagizo waliyopewa na rais walipoenda kwenye kikao hapo Ikulu. Tuna uwezo wa utambuzi. Wananchi tunajua wako upande upi, hakuna mwananchi atakayekuwa sehemu ya huo ubatili. Anayechafua chaguzi hapa nchini anafahamika.
 
Walichofanya kitaathiri zaidi chama chao kuliko kukijenga na hapo wanaacha mwanya kwa chama kingine ku'take over'.

Kwa kinachoendelea hicho chama acha kitake over ila wananchi sasa hivi tunajitambua. Hivyo vyama vya Tiss na matawi ya ccm sio rahisi vipate support ya watu.
 
Hivi watendaji wanaonajisi mchakato wa uchaguzi, ni kiongozi gani anayewabariki kufanya wanayoyafanya bila kuchukuliwa hatua zozote madhubuti?

Wako wapi takukuru waliojinasibu kufuatilia na kukomesha rushwa na uzandiki wa kipumbafu unaofanywa na machumia tumbo?

Mimi ni shabiki sana wa Magufuli, lakini mambo wanayoyafanya viongozi aliowapa dhamana ya kusimamia uchaguzi ni matusi ya nguoni kwa serikali anayoiongoza.

Yuko wapi Jafo wa Tamisemi, kiongozi kijana anayejinasibu kutenda vema na haki kila apewapo jukumu la kusimamia?

Ccm wana hofu gani na chaguzi hizi za ngazi ya chini hadi kupelekea kujivua nguo hadharani na kutembea uchi hadharani bila ya soni?
Hivi kunafuraha gani timu pinzani kujiondoa uwanjani kabla ya mechi?

Utendaji wa Magufuli jinsi unavyokubalika, ninadhani kuna maadui wa ndani kwa ndani, wameamua ki mbinu na ujanja wa hali ya juu kumvua nguo kwanjia hiyo ili ionekane amewa tuma yeye, jambo ambalo nitakuwa wa mwisho kuamini hivyo.

Hili jambo halina manufaa hata kidogo kwake binafsi, bali kwa wale walioamua kumchafulia sifa zake alizokwisha kujizolea kwa waTz.

Haiwezekani uchaguzi wa serikali za mitaa ukachafuliwa na baadhi ya watu, halafu akaendelea kuwanyamazia na kuwakingia kifua.

Achukue hatua na hatua zionekane zimechukuliwa dhidi ya hawa wavurugaji ili kukomesha vitendo vinavyotengeneza chuki zisizo na sababu kila kifikapo kipindi cha uchaguzi.
 
Back
Top Bottom