November 7, 2019
CHADEMA kutoshiriki uchaguzi serikali za mitaa kwamuibua Jafo.
Published on 7 Nov 2019
Muda mchache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutoa tamko la kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Waziri Waziri Ofisi ya rais TAMISEMI Selemani Jafo amesema kitendo cha viongozi wakuu wa CHADEMA kutangaza kutoshiriki uchaguzi ni kuwanyima haki ya msingi watu wengine ambao majina yao yalishateuliwa. _____________ "Muda wa kukata rufaa umefika na watu wengine fomu wanakosea kujibu kwa makusudi, Je ulikuwa mpango mkakati wa kuwaelekeza fomu ziharibike ili kujitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo ni maswali ambayo nakosa kupata majibu, mimi kwa imani yangu nadhani kwamba inawezekana wanawanyima haki ya msingi huku chini watu wengine ambao majina yao yashateuliwa, watu wengine wamekata rufaa na rufaa zao kesho zinatoka leo hii viongozi wakuu wanatangaza kujitoa katika uchaguzi"-Selemani Jafo -Waziri TAMISEMI.
Source: ITV Tanzania
May 10, 2019
Makada wa CCM kusimania chaguzi vinazohusisha vyama vingi
Hapo awali wananchi walionesha shaka ya makada wa CCM na wateuliwa wa awamu ya tano kuweza kusimamia chaguzi huru na za haki.
Leo sote tunaona ni mashahidi chaguzi za Mitaa zilivyovurugwa na makada wa CCM.
uchaguzi mkuu Oktoba 2020 tutaona vituko zaidi ya hivi toka kwa makada wa CCM kuvuruga process nzima kuelekea uchaguzi.
10 May 2019
Mahakama Kuu nchini Tanzania kanda ya Dar es Salaam imesema sheria ya uchaguzi inayowapa uhalali wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ni batili, na hivyo imetamka kuvifuta vipengele viwili katika sheria hiyo.
Source: DW Kiswahili