CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

Hao ni wa chama chao mkuu wanaingiaje kwenye serikali?.

Wanasheria 2,500? Uza ubongo huo unakaa nao kwa hasara. Huyo Bashiru anatembea na ripoti ya wamiliki wa mali za chama na alisema watapelekwa mahakamani, hao wanasheria walikuwa bado masomoni? Hata kama ni wa ccm, sasa hivi kuna tofauti ya ccm na serikali?
 
CCM ina NUKA UVUNDO VIBAYA.

Na kila mwenye pua ameshasikia harufu hiyo ya uvundo.

IMG_20191107_233522.jpeg
 
November 7, 2019



CHADEMA kutoshiriki uchaguzi serikali za mitaa kwamuibua Jafo.

Published on 7 Nov 2019
Muda mchache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kutoa tamko la kutokushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa Waziri Waziri Ofisi ya rais TAMISEMI Selemani Jafo amesema kitendo cha viongozi wakuu wa CHADEMA kutangaza kutoshiriki uchaguzi ni kuwanyima haki ya msingi watu wengine ambao majina yao yalishateuliwa. _____________ "Muda wa kukata rufaa umefika na watu wengine fomu wanakosea kujibu kwa makusudi, Je ulikuwa mpango mkakati wa kuwaelekeza fomu ziharibike ili kujitoa kwenye uchaguzi, kwa hiyo ni maswali ambayo nakosa kupata majibu, mimi kwa imani yangu nadhani kwamba inawezekana wanawanyima haki ya msingi huku chini watu wengine ambao majina yao yashateuliwa, watu wengine wamekata rufaa na rufaa zao kesho zinatoka leo hii viongozi wakuu wanatangaza kujitoa katika uchaguzi"-Selemani Jafo -Waziri TAMISEMI.
Source: ITV Tanzania

May 10, 2019
Makada wa CCM kusimania chaguzi vinazohusisha vyama vingi

Hapo awali wananchi walionesha shaka ya makada wa CCM na wateuliwa wa awamu ya tano kuweza kusimamia chaguzi huru na za haki.

Leo sote tunaona ni mashahidi chaguzi za Mitaa zilivyovurugwa na makada wa CCM.

uchaguzi mkuu Oktoba 2020 tutaona vituko zaidi ya hivi toka kwa makada wa CCM kuvuruga process nzima kuelekea uchaguzi.

10 May 2019
Mahakama Kuu nchini Tanzania kanda ya Dar es Salaam imesema sheria ya uchaguzi inayowapa uhalali wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi ni batili, na hivyo imetamka kuvifuta vipengele viwili katika sheria hiyo.

Source: DW Kiswahili
 
Wanasheria 2,500? Uza ubongo huo unakaa nao kwa hasara. Huyo Bashiru anatembea na ripoti ya wamiliki wa mali za chama na alisema watapelekwa mahakamani, hao wanasheria walikuwa bado masomoni? Hata kama ni wa ccm, sasa hivi kuna tofauti ya ccm na serikali?
Kwani hajawahi pata dharura ukatafuta wakili?,huenda ccm walishtukia mapema kuwa mwaka huu kosa dogo litakufanya uenguliwe wakawatumia mawakili.
 
Hilo nalo ni swali fikirishi la kujiuliza,ingawa huenda ujazaji wa zamani mapungufu yalikuwa yanafunikwa,kwa sasa wamekaza.
Siku ile Rais anawapisha wakurugenzi alisema 'mkurugenzi nakulipa mshahara, nakupa gari, nakupa nyumba na posho alafu ole wako umtangaze mpinzani kashinda'
Samson unanishawishi nini mim nijiandikishe na kupoteza muda wngu kwenda kupiga kura wakati mshindi anafahamika?
 
Siku ile Rais anawapisha wakurugenzi alisema 'mkurugenzi nakulipa mshahara, nakupa gari, nakupa nyumba na posho alafu ole wako umtangaze mpinzani kashinda'
Samson unanishawishi nini mim nijiandikishe na kupoteza muda wngu kwenda kupiga kura wakati mshindi anafahamika?
Hayo ni maneno tu mkuu,uchaguzi unaongozwa kwa sheria na kanuni huru,wewe nenda kapige kura.
 
Chadema wamefanya Jambo moja la maana Sana kujitoa kwasabb hawa mashetani wangejisifia na ushindi fake kila kukicha na propaganda za kishamba za hapa na pale ilimradi waonekane wanakubalika!!!!
Kwa hiki kilichotokea hawajaamini kabisa kama chadema wamejitoa.

Sidhani kama wataweza kutamba Kwa ushindi wa mezani
 
Jana niliandika uzi usemao wapinzani watakaoshiriki uchaguzi wa serikali za mitaa ni wasaliti wa watanzania. Kwa vitendo walivyofanyiwa wapinzani hakuna sababu yoyote ile inayoweza kuharalisha ushiriki wao kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa. Toka niijue Chadema leo imefanya uamuzi sahihi sana. Mpira umebaki kwa Zitto Kabwe, maana kama atashiriki uchaguzi huu huku akijua hatoshinda labda watakapotaka ccm kumwachia kwa kupenda kwao, basi Zitto atawathibitishia watanzania tetesi za muda mrefu kuwa yeye ni msaliti na mtu wa kitengo. Maana kushiriki uchaguzi huu ni kuhalalisha uchaguzi huu haramu uonekane halali.
 
November 5, 2019

WAZIRI JAFO AMEJIBU TUHUMA ZA CHADEMA KUHUSU UCHAGUZI
Kuelekea Uchaguzi mdogo wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 24, mwaka huu, kumekuwa na Malalamiko mengi kutoka kwa wanachama wa Upinzani wakilalamikia majina ya Wagombea wao kukatwa, kufungwa kwa baadhi za ofisi za Watendaji hali inayodaiwa kukwamisha zoezi la kurudisha fomu kwa wagombea hasa wa Upinzani.. Kupitia Global tv tumefanikiwa kuzungumza na Waziri mwenye Dhamana ya TAMISEMI Selemani Jafo, ambaye amejibu madai hayo..


Source: Global TV online
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani sasa
 
Back
Top Bottom