mozila firefox
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 899
- 1,761
Yaani wew jamaa ni mnafiki mkubwa, unamtofautishaje jiwe na haya makando kando yanayoendelea? Ina maana unajifanya ufahamu aliyetugawa watanzania kufika hapa.
'mkurugenzi nimekuteua mim, nakulipa mshahara, posho, gari na nyumba alafu ole wako umtangaze mpinzani ameshinda'
'mkurugenzi nimekuteua mim, nakulipa mshahara, posho, gari na nyumba alafu ole wako umtangaze mpinzani ameshinda'
Hivi watendaji wanaonajisi mchakato wa uchaguzi, ni kiongozi gani anayewabariki kufanya wanayoyafanya bila kuchukuliwa hatua zozote madhubuti?
Wako wapi takukuru waliojinasibu kufuatilia na kukomesha rushwa na uzandiki wa kipumbafu unaofanywa na machumia tumbo?
Mimi ni shabiki sana wa Magufuli, lakini mambo wanayoyafanya viongozi aliowapa dhamana ya kusimamia uchaguzi ni matusi ya nguoni kwa serikali anayoiongoza.
Yuko wapi Jafo wa Tamisemi, kiongozi kijana anayejinasibu kutenda vema na haki kila apewapo jukumu la kusimamia?
Ccm wana hofu gani na chaguzi hizi za ngazi ya chini hadi kupelekea kujivua nguo hadharani na kutembea uchi hadharani bila ya soni?
Hivi kunafuraha gani timu pinzani kujiondoa uwanjani kabla ya mechi?
Utendaji wa Magufuli jinsi unavyokubalika, ninadhani kuna maadui wa ndani kwa ndani, wameamua ki mbinu na ujanja wa hali ya juu kumvua nguo kwanjia hiyo ili ionekane amewa tuma yeye, jambo ambalo nitakuwa wa mwisho kuamini hivyo.
Hili jambo halina manufaa hata kidogo kwake binafsi, bali kwa wale walioamua kumchafulia sifa zake alizokwisha kujizolea kwa waTz.
Haiwezekani uchaguzi wa serikali za mitaa ukachafuliwa na baadhi ya watu, halafu akaendelea kuwanyamazia na kuwakingia kifua.
Achukue hatua na hatua zionekane zimechukuliwa dhidi ya hawa wavurugaji ili kukomesha vitendo vinavyotengeneza chuki zisizo na sababu kila kifikapo kipindi cha uchaguzi.