CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

CHADEMA yajiondoa kushiriki Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Waziri Jafo awashangaa kususia uchaguzi

inawezekana vipi usimtambue mtu unayehitaji muhuli wake kila mara?
Nani atakusikia bank kwamba humtambui mwenyekiti wako?

Maana yake ccm wanabomoa taifa. Hii ni zaidi ya kutengeneza vita ya wenyewe kwa wenyewe

Usichukulie kilahisi hivo matamko yakisiasa

Hatari kubwa mitaani unakoenda kutokea
 
Figisu na ubabaishaji katika uchaguzi serikali za mitaa ulifanywa ili kuwapitisha bila kupingwa wagombea wa CCM. Ajabu ni kuwa Chadema imejitoa ili wajitangaze washindi wa kishindo, lakini ghafla wao tena ndio wananyong'onyea na kulalama?
Vyama vingine vikiamua kuunga mkono Chadema kwenye uchaguzi litakuwa pigo kubwa kwao.
Pigo kwa lipi mkuu? Kwani ni mara ya kwanza vyama vya upinzani Tanzania kujitoa kwenye uchaguzi? CUF Mara ngapi wanajitoa? Liliishawahi kuwa pigo kwa CCM? Chadema kujitoa kwenye uchaguzi ni jambo jipya? CCM iliishapata pigo wapi kwa Chadema kujitoa? Sana sana tunaomba na mwakani mjitoe kwenye udiwani. Mjitoe kwenye ubunge na mjitoe kwenye urais. Halafu tuone kama Chadema itaendelea kuwa moja zaidi ya kuwa kama CUF ya sasa.
 
Hiyo Ndio demokrasia

Kama hujajipanga unajiandaa kwa wakati mwingine

TLP itatoa ushindani sasa
Una juhudi kuwa sana ya kuandika ili kuitendea haki posho unayopewa, lakini ni bahati mbaya kuwa eitha hakuna mawasiliano kati ya ubongo na unacho andika au kichwani hakuna ubongo at all.
Uwezo mdogo ulio nao ungeutumia kuchunga ng'ombe.
 
Usishangae Mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa sheria na katiba wakaja na sheria na Wakapitisha kwamba " chama kikijitoa au kutokushiriki uchaguzi wanakifuta". hii itawakua inawapa shavu ccm kuiba.

Hawashindwi Mkuu.
 
Usishangae Mwanasheria mkuu wa serikali na waziri wa sheria na katiba wakaja na sheria na Wakapitisha kwamba " chama kikijitoa au kutokushiriki uchaguzi wanakifuta". hii itawakua inawapa shavu ccm kuiba.
Chadema kimeshavuka huko kwenye kutishiwa kukifuta.
Kufuta Chadema ni sawa na kutangaza asubuhi moja kuwa umefuta JWTZ na unawataka askari wote warudi majumbani siku hiyohiyo watawanyike.
 
Usiwe na haraka bado mda haujafika kuna mda ukifika mambo hutokea automatically. Sasa hivi tunapata walau milo miwili kwa siku na hao wanasiasa wao wanainjoi vizuri tu. But ipo siku mambo yakiwa mabaya zaidi kwa wale haves not utashangaa namna ambavyo halitaogopwa jeshi wala kifaru na utaona watawala watakavyokuwa madhalili kama kule mashariki ya kati.
 
Msipowatambua inamaana mtaishije huko makwenu?..

Ila mlikuwa kimya hadi nimesoma hamkusaidiana kujaza fomu vizuri.. kama kawaida munasubiri.. ndio munakurupuka..
Tutaishi kama enzi za babu zetu walivyokuwa wanaishi kwa kuheshimiana, mdogo ana muheshimu mkubwa na kufuata maelekezo yake kama kiongozi.
 
Uwezo huo hawana. Tatizo ambalo limesumbua sana upinzani kwa muda mrefu ni kuwa wanasiasa ndio wana mikakati wa upinzani. Matokeo yake haya unayoyaona mtalaumu Magufuli bure. Hawakuwa na mbinu nyingine yeyote wakati wa JK; unafikiri watapata sasa? Upinzani hauitaji mbinu nyingine tu; unahitaji uongozi mpya kabisa. Kama wangeniuliza mimi. Hapa mtazungushana hadi hawa wengine watazeeka huku mkiwaangalia; angalieni ya kina Besigye... na yaliyowakuta kina Tshikedi..
Mkuu unaheshimika sana. Je unaona kuna mazingira sawa ya kisiasa nchini? juzi wagombea walitendewa haki? kwanza kuwe na mazingira sawa ya kisiasa hala ndio tulaumu mengine.. hata wakija wapya kama mazingi tuliyokweka ni hayahaya...
 
Hilo agizo la Chadema la kutowatambua viongozi wa mitaa ,vijiji na vitongoji watakaochaguliwa ni hewa,la kijinga na halitekelezeki

Ukifika eneo la kutaka kununua au kuuza nyumba,shamba au chochote kwenye Kijiji,kitongoji au mtaa utakumbana nao na utawahitaji utake usitake

Barua mbalimbali za utambulisho nk lazima utaenda tu hukwepi utawafuata mwenyewe.Unataka hata kuanzisha mgodi ujanja huna lazima utawafuata Wala hawakufuati

Chadema kwa hili agizo wanathibitisha wazi kuwa akili hawana ikiwemo Kamati kuu vichwani weupe
Kifupi Kamati kuu ya chadema ni hopeless kwenye hili
 
Chadema walionyesha tangu mwanzo hawataingia kwenye uchaguzi pale walipowakataza wanachama wake kujiandikisha. Kama walikuwa na nia ya kuingia kwenye uchaguzi kwa nini hawajaenda mahakamani kusimamisha zoezi zima la uchaguzi baada ya kuona lina dosari?
 
[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji848][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji144][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji124][emoji116]
Msipowatambua inamaana mtaishije huko makwenu?..

Ila mlikuwa kimya hadi nimesoma hamkusaidiana kujaza fomu vizuri.. kama kawaida munasubiri.. ndio munakurupuka..
 
Mbowe wewe ni kiongozi wa chama cha siasa.
Lengo kuu la chama chochote ni kushika dola.

Unatakiwa kutambua kususia uchaguzi maana yake ni kuwadhulumu wananchi.
Sio kila mtaa majina yamekatwa, sasa madudu mliyofanya huko kwenu Hai unataka tuumie na tusiousika.

Hiki chama sio cha viongozi, maana ya maamuzi yenu ni kuua chama, serikali inaanzia mtaani, kama mnaona hamtendewi haki mbona ubunge mnaendelea?

Mbowe ni jipu litumbuliwe.
Nenda kashiriki Uchaguzi, Mbowe hatokuzuia. Kilichojitoa ni chama cha CHADEMA unaweza kuchagua viongozi wa vyama vingine, kuna vyama zaidi ya 25 kwenye kitabu cha msajili wa vyama, wala usiumie sana kwa CHADEMA kujitoa.
 
OOOh, Yeah! Haya mambo ya kujiliza liza na kusema CCM wanatumia nguvu, halafu unajiondoa, hayafai. Unataka nani akusaidie hiyo kazi yako ya siasa? Mimi ni mkulima mbona jua likiwaka natafuta mbinu mwenyewe bila kuwalilia wanasiasa?

Wanasiasa wanataka tuwe mateka wa kazi yao. CHADEMA, ACT, pambana na CCM. Wakitoa virungu nanyi toeni virungu. hiyo ni kazi yenu!
Nakubaliana na wewe mkuu wanataka sie wakulima tufanye kazi yao [emoji1666]
 
OOOh, Yeah! Haya mambo ya kujiliza liza na kusema CCM wanatumia nguvu, halafu unajiondoa, hayafai. Unataka nani akusaidie hiyo kazi yako ya siasa? Mimi ni mkulima mbona jua likiwaka natafuta mbinu mwenyewe bila kuwalilia wanasiasa?

Wanasiasa wanataka tuwe mateka wa kazi yao. CHADEMA, ACT, pambana na CCM. Wakitoa virungu nanyi toeni virungu. hiyo ni kazi yenu!
wewe si juha hujui kesho yako itakuwaje!+ A new approach! of whatever means!
 
Chadema kimeshavuka huko kwenye kutishiwa kukifuta.
Kufuta Chadema ni sawa na kutangaza asubuhi moja kuwa umefuta JWTZ na unawataka askari wote warudi majumbani siku hiyohiyo watawanyike.
Kinaweza kufutwa kama chama chochote kile, na huo mtego ndio chadema wamesha uona hawaingii. Kwanza viongozi walijitokeza kuhamasisha watu kujiandikisha wakati wananchi walikuwa wamegomea zoezi hilo.

Kwa kufanya vile CCM wakapandisha mzuka na wakakaa mkao wa kula. CHADEMA kujitoa kumewapagawisha maana hapo msajili hana cha kuwashutumu chadema.

Wamehamasisha wananchi kujiandikisha, na walionyesha nia ya kushiriki, lakini Wasimamizi kwa utashi wao na wa chama chao wakaamua kuharibu.
 
Back
Top Bottom