Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mara baada ya Tamko Batili la Jeshi la Polisi la Kuzuia Maandamano Halali ya Chadema, Mkurugenzi wa Itifaki wa Chama hicho, John Mrema, amesema kwamba Wajibu Pekee wa Polisi kwenye mandamano yoyote ni kuimarisha Ulinzi tu, hawana Mamlaka yoyote ya kuyazuia.
Hii ni kwa Mujibu wa Sheria za Tanzania.
Mrema amedai kwamba, Maandalizi ya Maandamano hayo yanaendelea kama yalivyopangwa yakiwa na lengo la kupaza sauti Dunia nzima ili wote waliotekwa warejeshwe au kama wameuawa kama Ally Kibao basi mifupa yao ikabidhiwe kwa ndugu zao waizike kwa Heshima..