Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Chalamila: Huwezi kukwepa kelele Dar es Salaam

Huyu jamaa commedian sanaa .... kuna clip anasema kwa wenza ukisikia mwenzio anaimba "....mtarimbo huo mtarimbo huoo ...mtarimbo umelala doro.." ujue una la kesi

kumuita comedian ni kama ume ignore machafu chafu yake, huyu ni muhuni, hajiheshimu

Muu wa Mikoa hadharani unajadili wanawake wafupi na mitarimbo iliyolala ?

Ndio maana Mimi nikiona watu wanalilia katiba mpya nawaona kama machizi tu. Tatizo la hii nchi sio katiba ila ni usimamizi wa hiyo katiba. wanao taka katiba mpya wangehakikisha kwanza katiba na sheria zilizopo zinafuatwa kiuhakika.

Ni mara chache sana kusikia viongozi wetu iwe wa chama tawala au upinzani wakisimama na kukemea usinginaji wa katiba/ sheria
Mkuu hapo mwisho hauko sahihi. Hususan wapinzani ndani na nje ya bunge wamelalamikia sana katiba na sheria kutozingatiwa tangu awamu zilizopita. Na wengine imewagharimu vilema hadi vifo.

Tatizo bado ni katiba hii hii. Huwezi kusimamia utekelezaji wake endapo viongozi na watendaji husika wanajali kauli ya mtu mmoja tu ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi wao. Tena huyo mamlaka ya uteuzi anaweza hata kuamua nani awe mbunge au asiwe! Huyo asipotaka mtendaji mbovu aondolewe, hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kumchukulia hatua. Hata mahakama haina ubavu huo! Unategemea nini hapo?
 
Hitler baada ya kushinda uchaguzi wa kidemokrasia kwa kishindo 1933, . alichekewa hivi hivi..... Kisha akajitangaza mtawala mkuu (führer) wa Ujerumani
Enhe, alishinda kwa kishindo uchaguzi wa kidemokrasia wa 1933...
Kisha akajitangaza mtawala mkuu wa Ujerumani...
Alishinda kwa kishindo uchaguzi ili awe nani, mtawala naibu ?
 
"....huwezi kukwepa kelele hapa Dar es Salaam. Muhimu kila awaye apate uhuru wa haki yake aipendayo. Izingatiwe, hata wanywa bia wana haki ya kunywa huku wakiserebuka na hiyo ni haki yao na ni muhimu izingatiwe"

Chalamila.

============

Chalamila.jpg

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaomba Wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo huku akiongezeka kuwa Jiji la Dar es Salaam haliwezi kukwepa kelele wala kukwepa starehe.

Akiongea wakati wa Swahili Comedy Show iliyofanyika Swahili Exprience, Coco Beach Dar es salaam, amesema “Kikubwa Mimi kama RC naahidi kutoa ushirikiano wa kiulinzi lakini zaidi kufanya starehe ambazo hazitokuwa na makwazo kwasababu maana na tafsiri ya kelele bado ni jambo ambalo ni gumu kidogo, adhana ikipiga asubuhi asiye Muislamu atasema hizo ni kelele"

"Vyombo vya Kanisani vikipiga kwa nguvu asiye Mkristo atasema ni kelele, miziki ya Baa ikipigwa Mtu ambaye sio mnywa pombe atasema ni kelele, kwahiyo kuna mahali panahitaji busara kuhusu tafsiri sahihi ya kelele ili Muislamu, Mkristo wapate haki zao, mnywa pombe apate haki yake na asiye imani apate haki yake, kikubwa Dar es salaam huwezi kukwepa kilele, huwezi kwepa starehe"
 
Chanzo 👇👇

MillardAyoUPDATES
 
Huu ujinga ujinga utaisha siku CCM ikiondolewa madarakani tu.

Sheria zipo ila matamko ya kipuuzi hayaishi kila siku

Katiba mpya ni muhimu sasa
 
Wajinga njoo mshangilie, Taifa lina sheria za kisiasa tu, Naipenda Katiba ya Kenya, Gavana wa Count ndio ana fina say na haweI ingiliwa na kiongozi yoyote yule akiwemo Raisi, Ila Bongo Mkuu wa wilaya tu anaweza batilisha sheria.
 
Wajinga njoo mshangilie, Taifa lina sheria za kisiasa tu, Naipenda Katiba ya Kenya, Gavana wa Count ndio ana fina say na haweI ingiliwa na kiongozi yoyote yule akiwemo Raisi, Ila Bongo Mkuu wa wilaya tu anaweza batilisha sheria
Hapa Tz cyo kemya . TUNA NAMNA YRTU YA KUISHI KIJAMAA
 
Excellent point.

Hitler baada ya kushinda uchaguzi wa kidemokrasia kwa kishindo 1933, alichekewa hivi hivi na mamilioni ya Wajerumani akapitisha miswada kibao bungeni kubadili katiba ya kidemokrasia ya Ujerumani kujipa madaraka makubwa akidai ni muhimu ili kuimarisha taifa nyakati hizo za migogoro mingi ya kimataifa.

Hawajakaa sawa akajaza watu wake kwenye taasisi zote muhimu za nchi pamoja na majeshi yote. Kisha akajitangaza mtawala mkuu (führer) wa Ujerumani na kutawala kama absolute dictator hadi kifo chake akiacha Ujerumani hoi zaidi ikigawanywa na kutawaliwa na US/Europe upande wa Magharibi na USSR upande wa Mashariki.

Ndio hasara ya kuchekea watu waovu.
Sasa huko ndo magufuli alikokua akitupeleka lilikua ni swala la muda tu....!
 
Mkuu hapo mwisho hauko sahihi. Hususan wapinzani ndani na nje ya bunge wamelalamikia sana katiba na sheria kutozingatiwa tangu awamu zilizopita. Na wengine imewagharimu vilema hadi vifo.

Tatizo bado ni katiba hii hii. Huwezi kusimamia utekelezaji wake endapo viongozi na watendaji husika wanajali kauli ya mtu mmoja tu ambaye ndiye mamlaka ya uteuzi wao. Tena huyo mamlaka ya uteuzi anaweza hata kuamua nani awe mbunge au asiwe! Huyo asipotaka mtendaji mbovu aondolewe, hakuna mtu mwingine mwenye uwezo wa kumchukulia hatua. Hata mahakama haina ubavu huo! Unategemea nini hapo?
Nimekusoma mkuu
 
Back
Top Bottom