#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda...
GWAJIMA-Mwenyekiti SUKUMA GANG

Huyu nana elimu dunia, na hata PhD yake haijulikani alipoitoa.

huyu na wapumbavu wengine wamechomwa chanjo 13 toka kwa wamarekani, yaani chanjo zote za utoto , mabusha , Hepatitis B, C na Yellow fever, hawakuwahi kupinga wala kutilia shaka ila hii moja tu ndio wananyanyua mabakuli yao.
 
Hatuwezi kutest Chanjo kwa Taifa zima ni risk sana napendekeza hz Chanjo milion 1 tuzipeleke mkoa wa Kilimanjaro tuanzie huko kwa maana huko hali ni mbaya sana .
 
mi nawashangaa viongozi nchi nzima wamelishupalia hili la korona utafikiri ndo ajenda kuu ya nchi... hv ukichanjwa haufi? mbona wakina Biden wamechanjwa lakin bado wanajitundika mabarakoa?

kwani nini maana ya chanjo, km ukichanjwa bado unakuwa prone wa virusi?

tuendelee kunywa mtori nyama tutazikuta chini wajomba
 
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda. Mpaka sasa wapinga chanjo(anti vaxxers) wakiongozwa na jemedari wao Askofu Gwajima wanaongoza katika mtanange huu na hakuna anayeleweka kwa wakubali chanjo kuanzia January, Kigwangalla mpaka Mbowe n.k..

Naunga mkono hoja. Umewaelezea vizuri sana. Mtu hawezi kuwaelezea zaidi ya hapo:

"Wapinga chanjo(anti vaxxers) wana hoja na maswali mengi yanayodhihirisha ujinga, upumbavu na uduni wa fikra katika idadi kubwa ya raia nchini(majority).

Zaidi sana wana ujasiri na nguvu kama Simba wa kusimamia ujinga uliowajaa tofauti na wenzao. Hakuna namna ya kuwashauri kuhusu umuhimu wa chanjo, mnaofanya hivyo mnapoteza nguvu na muda wenu tu."


Hata hivyo kuna kundi jingine nadhani linapambana kuzuia kufahamika kuwa lina kesi ya kujibu kutokana na vifo vya kuzembea vilivyo na vinavoendelea kutokea. Kundi hili lina vi ID vya msaada ambavyo huibuka kama moto wa mabua.

Wanakwenda kwa waves utafikiri mwana wa Wuhan.
 
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda...
Serikali iliyipita ilichngia pakubwa sana kwa hili,Yaani upotoshaji mkubwa ulianzia hukohuko Ikulu.yaani tulianza kuaminishwa kwamba hata mashine za kupima korona hazisemi ukweli, Ila corona ikawa inawatafuna huko huko Ikulu.Kauli zilitoka Ikulu hukohuko,waziri huyuhuyu wa afya pamoja na mtangulizi wake ndiyo alikuwa mashauri mkuu wa mkuu wa nchi.

Tunachopaswa kukumbuka sasa hivi nchi imapata kiongoz mwingine mwenye maono tofauti.inawezekana ulikuwa ni mpango wa Mungu kutunusuru na janga hili kwa kutuletea Mkuu mwingine wa nchi atakayetuvusha vizuri.

Mambo mambo ya kisayansi yalianza kufanyiwa ramli.

Kuna wakati mwingine naonaga aibu kuitwa Mtanzania
 
Kwenye ujinga hekima ipo, kwenye unyonge na udhaifu ipo nguvu. Lazima pawepo na nguvu kinzani ili mizania iwe sawa
 
Kama hutaki kuchanjwa kwa nini uwadanganye wenzako watakuwa mazombi wakichanjwa?
Kwani hakuna uthibitisho wa kuwa chanjo zitawafanya watu kuwa mazombi au chanjo kukinga ugonjwa kwa asilimia mia moja, hivyo sioni mantiki ya kumuhukumu Gwajima kuwa ni muongo na hata kama akiwa anawadanganya wenzake, mara ngapi Gwajima kama Gwajima ameshasema mambo ya ajabu?

Alishasema anafufua misukule, alishasema atamfufua Amina Chifupa na mengi tu mbona hamkumwambia ni anawadanganya wenzake ila kwa hili la chanjo ndiyo sasa mnamuona muongo?

Gwajima analinda maslahi yake ya uchangaji kwani hizi protokoli mpya za kujikinga na Korona zinawanyima uhuru wa kukusanyika kwa wingi na wakati wa ibada umepunguzwa huenda hali hii ikapunguza sadaka.
 
Gwajima ni mmojawapo tu watu wengi waongo wasio na uelewa wowote wa chanjo ambao wamegeuka virologists ghafla baada ya Corona kuja.

Yeye nimemtolea mfano tu katika mamilioni ya Watanzania wenye akili kama zake hata kama hawajawahi kumsikia akizungumzia hiyo chanjo. Kupinga chanjo ni ujinga na huo ujinga ndio nauzingumzia katika ujumla wa nchi sio mtu mmoja mmoja.

Kwani hakuna uthibitisho wa kuwa chanjo zitawafanya watu kuwa mazombi au chanjo kukinga ugonjwa kwa asilimia mia moja, hivyo sioni mantiki ya kumuhukumu Gwajima kuwa ni muongo na hata kama akiwa anawadanganya wenzake...
 
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda...
1.)Hiyo chanjo si hiari? Sasa mnahangaika nini? Kwanini msichanje nyinyi ili muwe salama?

2.)Chanjo kwa definition ya CDC Marekani ambako ndiko zinakotoka, ni nini?

3.) Hiki kinachoitwa chanjo, nisi ya majaribio? Watu wafanyiwe majaribio bure? Au mtatulipa?
 
Inasikitisha lakini ndio uhalisia tulio nao. Ujinga umetamalaki, tumeruhusu wajinga kuchukua nafasi za juu za maamuzi nchini na wameambukiza jamii kubwa.
Hoja hujibiwa kwa hoja, au huzijui hoja za wanaopinga?
 
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda...
Cha ajabu ata walioingia darasani nao bado ni wajinga,ni kama watanzania tumefunikwa na ujinga wa asili,au kwa sababu watz wengi ni washirikina?
 
Huu ndio ujinga ninaouzungumzia, kama huu utakaoifanya serikali itenge muda na rasilimali kujibu hoja za watu waliobeba vichwa kama mifuko ya kuhifadhia meno badala ya kufikiri.
Hoja hujibiwa kwa hoja, kama unaweza kumuita mjinga kwa hoja zake, naamini utaweza pia kujibu hoja zake, zijibu
 
Mwandishi hajaeleweka anatupasha habari gani MPYA.
Kikubwa hoja hujibiwa kwa hoja hapo ndipo serikali imekwama.
1.uhakika kama chanjo haina madhara.
2.kuweka chaguo kutopenda kuwajibishwa kama chanjo italeta madhara
3.licha mtu akichanjwa inaonesha ataambukizwa NA achukue tahadhari kama hajachanjwa
4.hawajatafiti
5.wanaenda kujaribu nchi nzima je ikitokea madhara?
Sasa kwanini Nikubali ujinga huu.
Au umeambiwa kenya korona imeisha?

Ushawahi saini consent form hospital ?
Hii chanjo sio inafanyiwa majiribio ilishafanyiwa majaribio na result zake zipo na WHO wamezipitisha tayari
 
Back
Top Bottom