Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda. Mpaka sasa wapinga chanjo(anti vaxxers) wakiongozwa na jemedari wao Askofu Gwajima wanaongoza katika mtanange huu na hakuna anayeleweka kwa wakubali chanjo kuanzia January, Kigwangalla mpaka Mbowe n.k.
Kwa kuangalia nyuzi,video, mijadala na michango katika mitandao ya kijamii kuanzia hapa JF na kwingineko, kwa kuwasikiliza watu wengi ninaowafamu (wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa na washika dini) wapinga chanjo na wakosoaji wake ni wengi kuliko wanaoikubali.
Wapinga chanjo(anti vaxxers) wana hoja na maswali mengi yanayodhihirisha ujinga, upumbavu na uduni wa fikra katika idadi kubwa ya raia nchini(majority).
Zaidi sana wana ujasiri na nguvu kama Simba wa kusimamia ujinga uliowajaa tofauti na wenzao. Hakuna namna ya kuwashauri kuhusu umuhimu wa chanjo, mnaofanya hivyo mnapoteza nguvu na muda wenu tu.
Hali hii inadhihirisha kiwango kikubwa sana cha ujinga katika taifa letu na inamaanisha hata wanaopigania mabadiliko mengine makubwa na muhimu katika nchi hii haitakuwa rahisi kwao kufanikiwa.
Huo ndo uhalisia na ukweli mchungu wa kusikitisha kuhusu taifa hili.Kati ya wale maadui wakubwa watatu, adui ujinga ameiganda nchi kama ruba na hatoki leo wala kesho.
Maskini Tanzania.