KWANINI CHANJO YA KORONA IMELETWA
Kama kuchanja ni hiyari, na Mh. Rais ameamua kupigia debe chanjo, basi ni haki pia kwa wale ambao hawaungi mkono chanjo nao kupigia debe upande wao.
Sioni sababu ya wanaopinga chanjo kama Mh. Gwajima kutolewa kauli za vitisho na baadhi ya wana-CCM. Ndo maana ya hiyari hiyo. Hiyari ina pande mbili.
Sababu kuu haswa ya kuletwa chanjo nchini Tanzania ni kwa sababu Magufuli hayupo. Angekuwepo zisingekanyaga hapa. Kifo cha Magufuli kitatugharimu sana waTanzania.
Sababu ya pili ni ikumbukwe kwamba maudhui ya kuleta chanjo ilikuwa ni kuwasaidia mahujaji na waTanzania wengine wanaotaka kusafiri kwenda kwenye nchi ambazo zinahitaji chanjo. Lakini hata waSaudi wenyewe ni kwamba hawana imani na chanjo; na ndo maana wameamua kupiga marufuku mahujaji wa kutoka nje ya nchi yao.
Kwa mfano tuna chanjo ya homa ya manjano hapa Tanzania, lakini hakuna mtu anayehangaika nayo isipokuwa tu kama unataka kusafiri kwenda kwenye nchi ambayo wanataka uwe umechanjwa ndo wakupokee. Na hata hiyo chanjo yenyewe ya homa ya manjano kuchanja ni hiyari. Unaweza ukailipia tu na kupewa kadi kuwa umechanja ili usisumbuliwe huko uendako.
Sababu ya tatu ni ubeberu. Mh. Rais tuliona aliwapigia simu mabeberu wa EU siku ile akawaweka na loudspeaker. Kwa kuwa amejipendekeza mwenyewe kwenye anga zao ni lazima wampelekeshe wanavyotaka wao. Mabeberu siku zote hawapendi kuona fikra huru ya Mwafrika. Hawakufuruhishwa kabisaaaa na msimamo tofauti na ambao ulikuwa unaonesha matokeo chanya wa Magufuli. Matokeo chanya kwa maana ya kwamba waTanzania tumeishi kwa uhuru bila matatizo yoyote wakati wao mabeberu wakifungia ndani kama kuku.
Kwa wale wenye uzoefu naamini mtakubaliana nami kwamba Mzungu hata siku moja hayuko tayari kupokea wazo jipya na tofauti na anachojua yeye kutoka kwa ngozi nyeusi. Duniani huko watu wanatudharau ngozi nyeusi kwa kiasi kikubwa. Hilo sio tatizo. Tatizo ni pale sisi wa ngozi nyeusi tunapoanza kujidharau wenyewe. Hilo ni tatizo kubwa sana ambalo linawatafuna waAfrika wengi sana.
Leo hii mTanzania ukimwambia aachane na Ukristo au Uislam kwa kuwa sio falsafa za kiAfrika mtazozana sana.
Sasa kwa kujidharau huku leo hii tunaona serikali ikiwa imekamatwa akili na mabeberu, inaanza kufuata miongozo yao na kuagiza chanjo. Kwa hiyo sababu ya tatu ni hiyo ya ubeberu. Mabeberu walikuwa wanapambana kuhakikisha kuwa mwafrika anaendelea kuwa kwenye usingizi na kuwa kwenye himaya yao kifikra. Mwafrika kama Magufuli aliyezinduka dunia nzima kwa fikra tofauti alikuwa ni tishio kubwa kwa ubeberu.
Sasa kinachotia wasiwasi ni kauli kama ile ya kusema "Tutachanja 60%".
Ila tukirejea kwenye sababu ya pili, ni kwamba Mh. Rais ameonesha kwamba ni mpenzi wa safari za nje ya nchi. Kwa yeye kuchanja inawezekana kuwa ni lazima, maana hatujui atakwenda nchi gani safari zijazo.
Na Mh. Rais akishakuwa ni msafiri, viongozi wengine nao kama mawaziri, wakurugenzi, n.k. nao wataanza tu kusafiri.
Sasa kuyatambua mambo kama haya ndo msingi wa kujua ni tatizo gani haswa wanalojaribu kutatua kwa kupitia hizi chanjo. Sio unafuata mkumbo tu, wakati wewe maisha yako ni ya hapahapa Bongo.
Ingekuwa chanjo zimeletwa kwa ajili ya kupambana na "korona" basi zisingekuwa hiyari. Hatua zingine zinazoletwagwa kwa ajili ya kupambana na "korona" huwa si za hiyari (kama vile amri za kuvaa barakoa kwenye majengo na mabasi).
Mwisho kabisa nimalizie kwa kusema kuwa kama wewe ni Mwafrika unayeamini kwamba kichwa chako kina akili, na unaweza kufikiri, kwamba hauna haja ya kutegemea fikra za Mzungu, basi usimsahau huyu kiongozi wetu aliyetutoka. Uthubutu alioonesha na jinsi alivyokataa kabisa kushikwa akili na wazungu katika masuala fulani muhimu (madini na korona) ni jambo moja la muhimu sana katika ukombozi wa Mwafrika, ambayo bado ni safari ndefu sana. Kila kizazi kina jukumu la kusukuma gurudumu.
View attachment 1870885
Na kwa CHADEMA mliokuwa mnamlalamikia sijui mambo ya demokrasia naamini sasa hivi mmeshamuelewa kama kweli mna akili za kikubwa. Ni kwamba alikuwa anayajua matatizo yake ya moyo na kwamba alijua anakufa saa yoyote ndo maana alijitahidi sana kupeleka mambo kwa kasi atimize kabla hajafa.
Haya mambo ya kutaka kupigapiga siasa kila saa (zile Operesheni Operesheni mlizokuwa mnazipenda) hayana tija yoyote kwa mustakabali wa taifa. Naamini mnaendeshwa kwa falsafa za kiMarekani. Sasa Marekani hawajaendelea kwa sababu ya demokrasia, basi wameleta demokrasia baada ya kuendelea. Na kama mnavyoona demokrasia yao ni upuuzi mtupu, hakuna kinachofanyika kule wanazozana tu kila siku.