#COVID19 Chanjo za Kupambana na Corona (COVID-19): Nini Maoni na Mtazamo wako?

Ni mpumbavu tu ambaye haelewi legacy ya Magufuli. Tuna wapumbavu wengi tu wa aina yako hapa Afrika.

Ila kwa wenye akili ndo utakuta wanamtukuza sana kwa kirefu.

Soma jarida hili (link hiyo chini) kuanzia ukurasa wa tisa, sio unajaza kichwa upuuzi wa CNN na BBC.


Halafu niambie nani mwingine hapa Tanzania (ukiondoa Nyerere) amepata hadhi hiyo ya kupigiwa saluti na Afrika.
 

Je, COVID-19 ni nini?
COVID-19 ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona, virusi hivi ni sawa sawa na vile vinavyosababisha mafua ya kawaida tofauti na mafua, virusi vya corona vinaweza kuambukiza mwingine kabla hata ya huyo mtu hajaanza kuonesha dalili. Tofauti ni kwamba, watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama matatizo ya mapafu au ugonjwa wa kisukari, wamo katika hatari kubwa ya kuhisi kuhisi matatizo makali ya mapafu.

Watu walio na virusi vya COVID-19 kwa kawaida wataonyesha dalili zifuatazo: homa kali na kikohozi au kuhisi kuishiwa na pumzi. Athari zikizidi, wanaweza kuwa na matatizo makubwa ya kupumua na watahitaji kulazwa hospitalini au katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi wengine hupoteza maisha.

Je, COVID-19 inaenezwa vipi?
Virusi vya COVID-19 huenezwa hasa kwa kutangamana na mtu ambaye aliyeambukizwa na kuathirika au kuguza vifaa ambavyo viliguzwa au kupigiwa chafya na mgonjwa aliye na COVID-19. Virusi hivi hupatikana kwenye chembechembe za mate au makamasi. Vinaingia mwilini kwa kuguza au kupitia kwa kinywa, Pua au macho.

Jinsi ya kujizuia kupata ugonjwa wa COVID-19
Kunawa mikono kwa sabuni yako na kuepuka kugusa uso wako kwa mikono yako ni njia bora zaidi za kuepuka kupata magonjwa. Kujitenga kijamii (kudumisha angalau umbali wa mita 2 au futi 6 mbali na wengine) na kukaa nyumbani kama vile iwezekanavyo pia ni njia nzuri ya kuzuia kupata huu ugonjwa. Ili kuzuia kuambukiza virusi hivi kwa wengine, watu wanapaswa kukohoa au kupiga chafya huku wakifunika mdomo wao kwa sehemu ya ndani ya visugudi na sio kwa viganja zao na kuvaa Barakoa

COVID-19 ilianza lini?
Virusi vya Corona vimeingia Afrika Mashariki baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini Kenya tarehe 13 Mar 2020 na 16 Machi 2020 Mgonjwa wa Kwanza akagundulika Nchini Tanzania. Mlipuko wa Virusi vya Korona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ulibainika rasmi tarehe za katikati za mwezi Desemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko Nchini China.

Hadi sasa, zaidi ya Watu Milioni 3.81 wamepoteza Maisha kutokana na Ugonjwa wa COVID-19 Huku Watu zaidi ya Milioni 176 Wakiwa Wameambukizwa Duniani Marekani, India na Brazili zikiwa zinaongoza. WHO Coronavirus (COVID-19) Dashboard

NINI MCHANGO WA WANASAYANSI KATIKA KUPAMBANA NA COVID-19?
Kutokana na kuenea kwa kazi kwa ugonjwa wa COVID 19 ambao hadi sasa bado dawa yake haijapatikana, Watafiti wanaendelea kufanya Jitihada Pamoja na kutafuta Chanjo ya Ugonjwa.

Baadhi ya Chanjo za COVID-19 zimeonesha ubora katika kupambana na Maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19

CHANJO YA COVID-19
Nchi nyingi sasa zinatoa Chanjo za COVID-19 bure ili kujilinda na Maambukizi.

Kutokana na Chanjo ya COVID-19 kuonesha ubora wa kupamba na COVID-19 Baadhi ya Chini sasa ni lazima kuchoma sindano ya Chanjo ili uweze kuingia Nchi hizo.

Baadhi ya Mataifa ya Afrika yanayotoa chanjo na chanjo wanazotumia ni:
Morocco (AstraZeneca na Sinopharm)
Algeria (Sputnik V)
Misri (Sinopharm)
Kusini mwa jangwa la Sahara, mataifa yanayotoa chanjo ni:

Afrika ya kati(Johnson & Johnson)
Ushelisheli (Sinopharm na AstraZeneca)
Rwanda (taarifa zinasema wanatumia Pfizer na Moderna)
Mauritius (AstraZeneca)
Zimbabwe (Sinopharm)
Mataifa mengine kama vile Senegal na Guinea ya Ikweta yamepokea chanjo za Sinopharm lakini bado hazijaanza kutoa chanjo kwa umma.

Guinea ilitoa chanjo 60 za Sputnik V kutoka Urusi kwa watu kwa majaribio.

JE, KUNA UMUHIMU WA TANZANIA KUKUBALI KULETEWA CHANJO? MTIZAMO WAKO NI UPI?
Hivi karibuni Kamati maalum ya wanasayansi iliyoundwa na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa thathmini kuhusu hali ya ugonjwa Corona nchini, imeonya kuwa nchi ipo katika hatari ya kukabiliwa na wimbi la tatu iwapo hatua hazitochukuliwa.

Ripoti ya Kamati hiyo, ilitaka Serikali kuanza kuchukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo, kuanza kutangaza watu walioambukizwa virusi vya corona, na kuagiza chanjo. Kamati hiyo ilishauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa COVAX ulio chini ya mwamvuli wa GAVI. Mpango wa COVAX unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi.

Wakati hayo yakiendelea, Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, amewataka Wananchi wanaotaka kwenda Kuhijji, Wajiandae kuchanjwa kwani huwezi kuingia Maka Saudi Arabia bila kuchanjwa.

Hivi Sasa Serikali imeanzisha utaratibu wa kupima COVID -19 tena mara msafiri anapowasili kutokana na kuwepo vyeti vya COVID-19 vya kughushi huku wengine wakipata maambukizi wakiwa safarini na kuingiza Ugonjwa nchini.

“Kipimo tunachotumia sasa kinaonyesha majibu kwa muda mfupi na hata kama Mtu amepata maambukizi ndani ya saa mbili au tatu zilizopita tunambaini. Hii ndiyo namna ya kudhibiti maambukizi yasiingie nchini,”alisema Mkurugenzi wa huduma za kinga, Dk. Leonard Subi.

GHARAMA ZA KUPIMA UNAPOWASILI UWANJA WA NDEGE
Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa msafiri yeyote anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kupima Corona mtandaoni, kisha kwenda kwenye hospitali au kituo husika na kupima.

Gharama za malipo ni Dola za Marekani 100 (sawa na Sh. 230,000 ), Sh. 10,000 ya Hospitali au kituo ulichopimiwa na siku ya kurudi au kuingia nchini unatakiwa kulipa Dola 25 (sawa na Sh. 57,750)

MAMBO UNAYOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU CHANJO YA COVID-19

Usalama wa chanjo za COVID-19 ni kipaumbele cha juu. Chanjo ya COVID-19 imethibitishwa kuwa salama na yenye ufanisi.


Nchini Marekani, hatua nyingi zimewekwa ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama na zenye ufanisi. Hatua hizi zinajumuisha waliojitolea kutoka makundi mbalimbali ya rangi, kabila na umri wanaoshiriki katika majaribio ya kitabibu ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama kwa jamii mbalimbali. Taarifa na takwimu kutoka kwenye majaribio zinakaguliwa kwa kujitegemea na wanasayansi, wataalamu wa tiba, na wataalam wa afya ya umma kabla ya wewe kupewa chanjo.

Vituo vya Kudhibiti Magonjwa (CDC) vimeunda zana mpya ya kugundua haraka maswala yoyote ya usalama kuhusiana na chanjo za COVID-19. "V-safe" ni zana mpya inayotumika kwenye simu mahiri, ya kukagua afya baada ya chanjo. Itatolewa kwa watu wakati watakapokuwa wanapokea chanjo ya COVID-19.

Chanjo ya COVID 19 itakusaidia kujikinga kutokana na kupata COVID-19. Dozi mbili zinahitajika
Unahitaji dozi 2 za chanjo ya sasa ya COVID-19 ili kupata kinga kubwa zaidi dhidi ya ugonjwa huu mbaya.

Hivi sasa kuna usambazaji mdogo wa chanjo ya COVID-19 nchini Marekani, lakini usambazaji utaongezeka katika wiki na miezi ijayo
Kila mtu ataweza kupata chanjo dhidi ya COVID-19 mara tu idadi kubwa ya kutosha ya chanjo itakapopatikana. Chanjo ikishapatikana kwa wingi, kutakuwa na watoaji wa chanjo maelfu kadhaa.

Mnamo tarehe 13 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-Biotech ili kuzuia COVID-19.

Mnamo tarehe 20 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Moderna ili kuzuia COVID-19.

Ukosefu wa fedha za kulipa, hali ya uhamiaji, au ukosefu wa bima havitakuzuia kupata chanjo dhidi ya COVID-19
Dozi za chanjo zitatolewa kwa watu bila malipo bila kujali hali ya uhamiaji au ikiwa wana bima au la. Watoaji wa chanjo wanaweza kutoza ada za usimamizi wa kutoa chanjo. Watoaji wa chanjo wanaweza kulipwa ada hii na kampuni ya bima ya umma au ya binafsi ya anayepokea chanjo.

Baada ya chanjo ya COVID-19, unaweza kupatwa na athari za kawaida. Hii ni ishara kwamba mwili wako unajenga kinga
Athari ni dalili kwamba chanjo inafanya kazi, athari zinaweza kuwa kama homa na zinaweza hata kuathiri uwezo wako wa kufanya shughuli za kila siku, lakini zinapaswa kuondoka baada ya siku chache.

Kama Mwananchi, upi mtizamo wako juu ya Chanjo ya Corona na njia zinazotumika kupambana na Covid - 19 hapa nchini Tanzania?

Pia, soma:

1). Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19

2). Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga
Nenda kapate chanjo ,achana na maneno ya vichochoroni,akili ya kuambiwa changanya na zakwako.
 
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda. Mpaka sasa wapinga chanjo(anti vaxxers) wakiongozwa na jemedari wao Askofu Gwajima wanaongoza katika mtanange huu na hakuna anayeleweka kwa wakubali chanjo kuanzia January, Kigwangalla mpaka Mbowe n.k.

Kwa kuangalia nyuzi,video, mijadala na michango katika mitandao ya kijamii kuanzia hapa JF na kwingineko, kwa kuwasikiliza watu wengi ninaowafamu (wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa na washika dini) wapinga chanjo na wakosoaji wake ni wengi kuliko wanaoikubali.

Wapinga chanjo(anti vaxxers) wana hoja na maswali mengi yanayodhihirisha ujinga, upumbavu na uduni wa fikra katika idadi kubwa ya raia nchini(majority).

Zaidi sana wana ujasiri na nguvu kama Simba wa kusimamia ujinga uliowajaa tofauti na wenzao. Hakuna namna ya kuwashauri kuhusu umuhimu wa chanjo, mnaofanya hivyo mnapoteza nguvu na muda wenu tu.

Hali hii inadhihirisha kiwango kikubwa sana cha ujinga katika taifa letu na inamaanisha hata wanaopigania mabadiliko mengine makubwa na muhimu katika nchi hii haitakuwa rahisi kwao kufanikiwa.

Huo ndo uhalisia na ukweli mchungu wa kusikitisha kuhusu taifa hili.Kati ya wale maadui wakubwa watatu, adui ujinga ameiganda nchi kama ruba na hatoki leo wala kesho.

Maskini Tanzania.

Wewe usiyepinga chanjo tupe sababu zako.
 
Ni mpumbavu tu ambaye haelewi legacy ya Magufuli. Tuna wapumbavu wengi tu wa aina yako hapa Afrika.
Legacy.png

Kuna upumbavu kama huo wa kwako wa kutaka tuchukue maneno ya mtu asiye na taaluma yoyote ya kitabibu kwenye masuala ya kitabibu?!

REMEMBER:- Mtaji Mkubwa wa Magu ulikuwa Jeshi Kubwa la Wajinga lililokuwa nyuma yake! Na hili Jeshi la Wajinga ndio mtaji mkubwa wa watu aina ya Askofu Rasheed!!!

Ila kwa wenye akili ndo utakuta wanamtukuza sana kwa kirefu.
I'm sure wewe huwezi kuingia kwenye kundi la hao wenye akili!!! Sasa kama pamoja na kutokuwa na ubavu wa kuingia kwenye kundi la wenye akili, bila shaka utakuwa umepata jibu anatukuzwa na watu gani!!!

Mi nasema hivi... ungekuwa na akili usingeweka vitabu vya simulizi kujibu argument za kisayansi!! Ni kilaza pekee ndie anaweza kufanya huo ujinga!!!
Soma jarida hili (link hiyo chini) kuanzia ukurasa wa tisa, sio unajaza kichwa upuuzi wa CNN na BBC.
Hapa ndipo unapothibitisha ujuha wako manake katika posts zangu hakuna hata sehemu moja niliyoweka habari za media kujibu hoja za kisayansi, na kama papo, onesha!!

Kinyume chake, ni wewe mwenyewe ndie umeweka kitabu kilichoandikwa na mwandishi wa habari asiye na taaluma yoyote ya kitabibu, etu kujibu hoja ya kitabibu...

Muulize hata mtoto wa jirani yako hapo sasa ni nani kati yetu ni mpuuzi!!!

Halafu niambie nani mwingine hapa Tanzania (ukiondoa Nyerere) amepata hadhi hiyo ya kupigiwa saluti na Afrika.
Halafu hapa ndo ujiite una akili?! Typical Magu Supporter....

Yaani bado tu hujajua kwamba unatakiwa kuwa na Majuha wenzako ndipo unaweza kuokoteza sources uchwara online na kuzileta hapa?!

Ungekuwa na akili kama unavyojaribu kudai, ungeanza kwanza kuangalia Site Metrics kabla hujakuja kutujazia server!! Na ungefanya hayo, ungeona metrics za kiblog chako ni kama ifuatavyo....
Bl;og.png


Kumbe ki-blog chenyewe hakina hata online engagement halafu ndo unakileta hapa kama reference? Tafiri ya blog yenye metrics za aina hiyo ni blog uchwara kwa sababu hakina hata idadi ya maana ya watu wanaokitembelea hicho ki-blog! Ukiingia hapa, utaona Site Metrics za Blog ya Le Mutuz...

Lakini hata ukichukua hiyo magazine yenyewe... ina uzito upi?! Na kama haina uzito wowote, utashangaa nini ikiwa hata waandishi wenyewe ni makanjanja aina yako...

Next time, acha kuokoteza okoteza vihabari kutoka blogs uchwara wakati huna uwezo wa kuchuja!!!
 
Habarini Wanajukwaa,
Nawapa pole kwa shughuli zenu za hapa na pale katika kujitafutia ridhiki zenu za kila siku,na katika harakati za ujenzi wa taifa letu tukufu.

Hivi karibuni hapa Nchini kuna vuguvugu ambalo linaendeshwa na mchungaji Gwajima juu ya kukataza Watanzania wasipate Chanjo za Korona,katika kutetea hoja zake anajaribu kukonga hisia za watanzania wengi.

Na ukweli ni kwamba,tofauti na Wenzetu wa Ulaya na Marekani,jamii nyingi za kiafrika ziko tayari kuzipa kisogo tafiti za Kisayansi na kuamini uvumi ilimradi uvumi huo unakonga nyoyo zao.

Mimi nimeamua kupitia jukwaa hili niweke uzi huu ambao utamwezesha mtu yeyote mwenye mashaka,Swali au dukuduku kuhusu Chanjo hizi za Korona aweze kuuliza.

Nitajitahidi kujibu kila swali kadri nitakavyo weza.

Karibuni sana.
 
Anaetaka akachanjwe,asietaka aache.

Mimi nitasuburi kwa zaidi ya miaka 3 Ili nione upepo unaendaje,kama kuna uwezekano wa kufoji documents nitafanya hivyo.Najua CORONA haiwezi kunifanya chochote,au laah ningekuwa nimefukiwa tangu mwaka Jana maana si kea life ninaloishi.

NB:Sitaki ushauri.
 
Kuna umuhimu gani wa kuwa na chanjo isiyoweza kuzuia ugonjwa husika?
Endapo itatokea variant nyingine ya Corona chanjo hii itaendelea kuwa na manufaa au tutapaswa kuchanjwa upya?
 
Dawa nyingi kabla ya kumpatia mgonjwa lazima wachunguze kama kuna uwezekano wa allergic reaction kutokea.

Sasa kwann uchunguzi wa aina hii haufanyiki kabla ya kumpa mtu chanjo ya korona? Hudhanii kuwa hii ndiyo sabb ya damu kuganda kwa baadhi ya watu wanaopatiwa chanjo ya korona??
 
Kama ulikuwa hujui ripoti za utafiti wa kitaaluma huwa zinawekwa mtandaoni.

Kwa hiyo usiwe na akili fupi ukadhani ni vitu vya siri.

Kwa hiyo niliyemuuliza swali alete link tu kwamba ripoti ni hii.

Ila kiufupi hakuna utafiti wowote uliofanyika na hao wanaoitwa "wataalam" wetu.

Ni kwamba wamepewa tu maelekezo na wazungu kwamba habari ni hii.

Acha ujinga ukidhani unakuwa mwelevu.. Scienrific Journal Papers ziko kibao mtandaoni.. Kuanzia Science journal mpaka Journal za wahindi na wachina.. Watabe waliosoma mashule ya ukweli wanaelewa vizuri wapi wanapata nyanga za kibabe. Nenda Google scholar, scimago, Web of science au Science Direct katafute usome.. Usituletee ukilaza wako hapa..
Hivi humu JF kuna vilaza zaidi yako?
 
Bila ya kujali kuwa Rais Samia na kundi lake wamechomwa Janssen au hapana; haituondolei uhalali wa sisi kuhoji na kujadili kwa mapana bila ya kupotosha ufanisi na ubora wa Janssen Vaccine. Aidha, hii ni ukweli kwamba kati yetu sisi hakuna anaeweza thibitisha au kutothibitisha kuwa ni kweli Rais na kundi lake wamechomwa Janssen Vaccine au hapana .
Hili libaki kuwa lao na MUNGU wao.

Kama independent entity;
a. Tulitegemea kuona baada ya kuwasili kwa chanjo, Wizara ya Afya ifanye random trials kwa namna ambayo inafaa kabla ya kuwapa watanzania kutokana na record ya Janssen Vaccine. Hili halijafanyika, je wizara imeamua kutufanya sisi Lab testing rats [emoji232] ?

b. Kamati iliyoundwa juu ya UVIKO-19!ilikuwa ni theoretical based yaani ni ku google na google, na mapendekezo yake yalikuwa ni theoretical based dhidi ya existing research za wengine; kamati kama kamati Ilifanya testing gani katika kuishauri serikali juu ya chanjo za aina mbalimbali? kamati ilipendekeza chanjo ya aina gani? na kwa vigezo gani ambavyo ni experimental ?

c. Short na long term effects za Janssen zimebainishwa kwa mantikia gani? au ndiyo sisi tunatakiwa kuzitolea taarifa hizo long term na short term effects post vaccination?

d. Science kwa sasa ni weapon hatari sana, iweje sisi tunaendea haya mambo bila ya kuweka practical base? Integrity's na authenticity ya wizara ya afya ipo wapi? Dhamana dhidi ya watanzania ni kutusomea documents za wazungu au kututhibitishia by testing and trialing scientifically as independent entity?

La mwisho, lakini ambalo si la mwisho kabisa; nashauri kwamba kama Wizara ya Afya, inataka kufanikiwa katika hii vita, iwe PROACTIVE badala ya kuwa REACTIVE. Ni wakati wa kusikiliza zaidi kwasababu Wizara kama Wizara haijafanya experiment yoyote kwenye Janssen, kilichofanyika ni paper based na kupokea maagizo kutoka juu.

Hata hivyo, nashauri kwamba tusishawishi watu kutokwenda kuchanjwa; Wanasiasa na maigizo yao wasiwe ni sehemu ya kukukataza au kukushawishi kwenda au kutokwenda.
Maisha ni yako na MAAMUZI ya kwenda au kutokwenda yatoke kwako.
 
Kwani mkuu wewe ni virologist au ni kama askofu Rashid au hata kibwetere tu?
 
Kama ulikuwa hujui ripoti za utafiti wa kitaaluma huwa zinawekwa mtandaoni.

Kwa hiyo usiwe na akili fupi ukadhani ni vitu vya siri.

Kwa hiyo niliyemuuliza swali alete link tu kwamba ripoti ni hii.

Ila kiufupi hakuna utafiti wowote uliofanyika na hao wanaoitwa "wataalam" wetu.

Ni kwamba wamepewa tu maelekezo na wazungu kwamba habari ni hii.
Wewe ni JUHA tu!!

Weka hapa Ripoti ya Kitaalamu iliyoifanywa na Watafiti wetu kuhusu chanjo za surua, ndui, polio, na zinginezo!!!

Ulivyo mpumbavu unasahau kwamba chanjo zote zinazotumika nchi hii, huku zingine wewe mwenyewe na ukoo wako mkiwa mmezitumia, zote hizo zinatoka kwa Wazungu halafu hapa unakuja na porojo zenu za Kijuha eti Wazungu wanawaletea chanjo ili kuwamaliza... ni ujinga ulioje!!!

Hivi wewe na ukoo wako wote mna kipi cha maana cha kuwafanya wazungu wawatengenezee chanjo za kutaka kuwadhuru?

Kwamba eti wamepewa tu maelekezo na Wazungu ni ujuha mwingine!! Yaani unataka kuaminisha watu kwamba Wataalamu wetu ni bora kuliko wataalamu wa WHO walioidhinisha hizi chanjo!!!

Wewe ni Juha unapojaribu kuonesha Chanjo zilizoidhinishwa na WHO haziwezi kuwa salama kwa sababu tu Magufuli na Gwajima wamesema hivyo, kwa sababu kila nikikuambia weka hapa credible source inayo-support madai yenu ya kiwehu, bado umeshindwa kufanya hivyo zaidi ya kuweka vipeperushi vya kuokoteza online!!!

Huyo Gwajima na Magufuli waliwahi kuifanyia utafiti hiyo chanjo na kutoa majibu ya kisayansi mnayoyaimba hivi sasa?
 
Uzi huu ni kwa ajili ya kupashana habari za kisayansi za afya za binadamu.
Kwa kuanza, tumeona kitu kinaitwa chanjo kikipigiwa chapuo kwa nguvu na watu walio na wasio na utaalamu wowote kuhusu afya. Lakini pia nguvu kubwa inatumika kushawishi watu wapate chanjo inayoitwa kuwa ni ya covid 19. Na kwa nyongeza ni jambo ambalo halijawahi kutolewa ufafnuzi wa kitaalamu ni kwa sababu gani dunia inakaza sana kuzungumzia chanjo, badala ya kuwekeza katika tiba kama ilivyo kwa magonjwa mengine.

Tumsikilize huyu mtaalam wa afya na mwenye ushauri chanya atoa hapa ili tujadiliane kwa utaalamu, uvumilivu na umakini.

Ninaanza na hii clip.

 
Wewe ni JUHA tu!!

Weka hapa Ripoti ya Kitaalamu iliyoifanywa na Watafiti wetu kuhusu chanjo za surua, ndui, polio, na zinginezo!!!

Ulivyo mpumbavu unasahau kwamba chanjo zote zinazotumika nchi hii, huku zingine wewe mwenyewe na ukoo wako mkiwa mmezitumia, zote hizo zinatoka kwa Wazungu halafu hapa unakuja na porojo zenu za Kijuha eti Wazungu wanawaletea chanjo ili kuwamaliza... ni ujinga ulioje!!!

Hivi wewe na ukoo wako wote mna kipi cha maana cha kuwafanya wazungu wawatengenezee chanjo za kutaka kuwadhuru?

Kwamba eti wamepewa tu maelekezo na Wazungu ni ujuha mwingine!! Yaani unataka kuaminisha watu kwamba Wataalamu wetu ni bora kuliko wataalamu wa WHO walioidhinisha hizi chanjo!!!

Wewe ni Juha unapojaribu kuonesha Chanjo zilizoidhinishwa na WHO haziwezi kuwa salama kwa sababu tu Magufuli na Gwajima wamesema hivyo, kwa sababu kila nikikuambia weka hapa credible source inayo-support madai yenu ya kiwehu, bado umeshindwa kufanya hivyo zaidi ya kuweka vipeperushi vya kuokoteza online!!!

Huyo Gwajima na Magufuli waliwahi kuifanyia utafiti hiyo chanjo na kutoa majibu ya kisayansi mnayoyaimba hivi sasa?
Wewe ni mpumbavu wa kwanza kabisa. Hebu usiniwekee zogo hapa sina muda wa kupoteza kwa wapumbavu wasiojelewa.
 
Nimechomwa chanjo za mabeberu tangu nikiwa mwaka 0
Kwa hiyo hoja yako ni ya mazoea.

Sasa hiyo nayo unaona ni hoja?

Kwani hujui kuwa hata jambazi kuna wakati alikuwa ni mtu mwema?

Au unajua yule jamaa aliyegonga treni juzi pale Kilosa ilikuwaje? Ni kwa sbb alikuwa amezoea anapita kila siku pale hakutani na treni.

Funguka akili mwafrika usiishi kwa mazoea mtu anakuchukulia poe kuwa ushakuwa teja lake.
 
Back
Top Bottom