Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Kifaduro
Kwani tuna shida gani mpaka tuchanjwe?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwani tuna shida gani mpaka tuchanjwe?
Nenda kapate chanjo ,achana na maneno ya vichochoroni,akili ya kuambiwa changanya na zakwako.
Je, COVID-19 ni nini?
COVID-19 ni maambukizi yanayosababishwa na virusi vya Corona, virusi hivi ni sawa sawa na vile vinavyosababisha mafua ya kawaida tofauti na mafua, virusi vya corona vinaweza kuambukiza mwingine kabla hata ya huyo mtu hajaanza kuonesha dalili. Tofauti ni kwamba, watu wenye matatizo mengine ya kiafya kama matatizo ya mapafu au ugonjwa wa kisukari, wamo katika hatari kubwa ya kuhisi kuhisi matatizo makali ya mapafu.
Watu walio na virusi vya COVID-19 kwa kawaida wataonyesha dalili zifuatazo: homa kali na kikohozi au kuhisi kuishiwa na pumzi. Athari zikizidi, wanaweza kuwa na matatizo makubwa ya kupumua na watahitaji kulazwa hospitalini au katika chumba maalum cha wagonjwa mahututi wengine hupoteza maisha.
Je, COVID-19 inaenezwa vipi?
Virusi vya COVID-19 huenezwa hasa kwa kutangamana na mtu ambaye aliyeambukizwa na kuathirika au kuguza vifaa ambavyo viliguzwa au kupigiwa chafya na mgonjwa aliye na COVID-19. Virusi hivi hupatikana kwenye chembechembe za mate au makamasi. Vinaingia mwilini kwa kuguza au kupitia kwa kinywa, Pua au macho.
Jinsi ya kujizuia kupata ugonjwa wa COVID-19
Kunawa mikono kwa sabuni yako na kuepuka kugusa uso wako kwa mikono yako ni njia bora zaidi za kuepuka kupata magonjwa. Kujitenga kijamii (kudumisha angalau umbali wa mita 2 au futi 6 mbali na wengine) na kukaa nyumbani kama vile iwezekanavyo pia ni njia nzuri ya kuzuia kupata huu ugonjwa. Ili kuzuia kuambukiza virusi hivi kwa wengine, watu wanapaswa kukohoa au kupiga chafya huku wakifunika mdomo wao kwa sehemu ya ndani ya visugudi na sio kwa viganja zao na kuvaa Barakoa
COVID-19 ilianza lini?
Virusi vya Corona vimeingia Afrika Mashariki baada ya mgonjwa wa kwanza kuripotiwa nchini Kenya tarehe 13 Mar 2020 na 16 Machi 2020 Mgonjwa wa Kwanza akagundulika Nchini Tanzania. Mlipuko wa Virusi vya Korona (kwa Kiingereza: Coronavirus) ulibainika rasmi tarehe za katikati za mwezi Desemba mwaka 2019 katika mji wa Wuhan huko Nchini China.
Hadi sasa, zaidi ya Watu Milioni 3.81 wamepoteza Maisha kutokana na Ugonjwa wa COVID-19 Huku Watu zaidi ya Milioni 176 Wakiwa Wameambukizwa Duniani Marekani, India na Brazili zikiwa zinaongoza. WHO Coronavirus (COVID-19) Dashboard
NINI MCHANGO WA WANASAYANSI KATIKA KUPAMBANA NA COVID-19?
Kutokana na kuenea kwa kazi kwa ugonjwa wa COVID 19 ambao hadi sasa bado dawa yake haijapatikana, Watafiti wanaendelea kufanya Jitihada Pamoja na kutafuta Chanjo ya Ugonjwa.
Baadhi ya Chanjo za COVID-19 zimeonesha ubora katika kupambana na Maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19
CHANJO YA COVID-19
Nchi nyingi sasa zinatoa Chanjo za COVID-19 bure ili kujilinda na Maambukizi.
Kutokana na Chanjo ya COVID-19 kuonesha ubora wa kupamba na COVID-19 Baadhi ya Chini sasa ni lazima kuchoma sindano ya Chanjo ili uweze kuingia Nchi hizo.
Baadhi ya Mataifa ya Afrika yanayotoa chanjo na chanjo wanazotumia ni:
Morocco (AstraZeneca na Sinopharm)
Algeria (Sputnik V)
Misri (Sinopharm)
Kusini mwa jangwa la Sahara, mataifa yanayotoa chanjo ni:
Afrika ya kati(Johnson & Johnson)
Ushelisheli (Sinopharm na AstraZeneca)
Rwanda (taarifa zinasema wanatumia Pfizer na Moderna)
Mauritius (AstraZeneca)
Zimbabwe (Sinopharm)
Mataifa mengine kama vile Senegal na Guinea ya Ikweta yamepokea chanjo za Sinopharm lakini bado hazijaanza kutoa chanjo kwa umma.
Guinea ilitoa chanjo 60 za Sputnik V kutoka Urusi kwa watu kwa majaribio.
JE, KUNA UMUHIMU WA TANZANIA KUKUBALI KULETEWA CHANJO? MTIZAMO WAKO NI UPI?
Hivi karibuni Kamati maalum ya wanasayansi iliyoundwa na rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutoa thathmini kuhusu hali ya ugonjwa Corona nchini, imeonya kuwa nchi ipo katika hatari ya kukabiliwa na wimbi la tatu iwapo hatua hazitochukuliwa.
Ripoti ya Kamati hiyo, ilitaka Serikali kuanza kuchukua hatua za kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa huo, kuanza kutangaza watu walioambukizwa virusi vya corona, na kuagiza chanjo. Kamati hiyo ilishauri serikali kupitia vyombo vyake kulishughulikia suala la chanjo kwa kujiunga na mpango wa COVAX ulio chini ya mwamvuli wa GAVI. Mpango wa COVAX unalenga kuhakikisha nchi masikini kote duniani zinapata mgao sawa wa chanjo licha ya ufinyu wa uwezo wao wa kiuchumi.
Wakati hayo yakiendelea, Rais Hussein Mwinyi wa Zanzibar, amewataka Wananchi wanaotaka kwenda Kuhijji, Wajiandae kuchanjwa kwani huwezi kuingia Maka Saudi Arabia bila kuchanjwa.
Hivi Sasa Serikali imeanzisha utaratibu wa kupima COVID -19 tena mara msafiri anapowasili kutokana na kuwepo vyeti vya COVID-19 vya kughushi huku wengine wakipata maambukizi wakiwa safarini na kuingiza Ugonjwa nchini.
“Kipimo tunachotumia sasa kinaonyesha majibu kwa muda mfupi na hata kama Mtu amepata maambukizi ndani ya saa mbili au tatu zilizopita tunambaini. Hii ndiyo namna ya kudhibiti maambukizi yasiingie nchini,”alisema Mkurugenzi wa huduma za kinga, Dk. Leonard Subi.
GHARAMA ZA KUPIMA UNAPOWASILI UWANJA WA NDEGE
Kwa mujibu wa utaratibu wa sasa msafiri yeyote anatakiwa kujaza fomu ya kuomba kupima Corona mtandaoni, kisha kwenda kwenye hospitali au kituo husika na kupima.
Gharama za malipo ni Dola za Marekani 100 (sawa na Sh. 230,000 ), Sh. 10,000 ya Hospitali au kituo ulichopimiwa na siku ya kurudi au kuingia nchini unatakiwa kulipa Dola 25 (sawa na Sh. 57,750)
MAMBO UNAYOHITAJI KUFAHAMU KUHUSU CHANJO YA COVID-19
Usalama wa chanjo za COVID-19 ni kipaumbele cha juu. Chanjo ya COVID-19 imethibitishwa kuwa salama na yenye ufanisi.
Nchini Marekani, hatua nyingi zimewekwa ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama na zenye ufanisi. Hatua hizi zinajumuisha waliojitolea kutoka makundi mbalimbali ya rangi, kabila na umri wanaoshiriki katika majaribio ya kitabibu ili kuhakikisha kuwa chanjo ni salama kwa jamii mbalimbali. Taarifa na takwimu kutoka kwenye majaribio zinakaguliwa kwa kujitegemea na wanasayansi, wataalamu wa tiba, na wataalam wa afya ya umma kabla ya wewe kupewa chanjo.
Vituo vya Kudhibiti Magonjwa (CDC) vimeunda zana mpya ya kugundua haraka maswala yoyote ya usalama kuhusiana na chanjo za COVID-19. "V-safe" ni zana mpya inayotumika kwenye simu mahiri, ya kukagua afya baada ya chanjo. Itatolewa kwa watu wakati watakapokuwa wanapokea chanjo ya COVID-19.
Chanjo ya COVID 19 itakusaidia kujikinga kutokana na kupata COVID-19. Dozi mbili zinahitajika
Unahitaji dozi 2 za chanjo ya sasa ya COVID-19 ili kupata kinga kubwa zaidi dhidi ya ugonjwa huu mbaya.
Hivi sasa kuna usambazaji mdogo wa chanjo ya COVID-19 nchini Marekani, lakini usambazaji utaongezeka katika wiki na miezi ijayo
Kila mtu ataweza kupata chanjo dhidi ya COVID-19 mara tu idadi kubwa ya kutosha ya chanjo itakapopatikana. Chanjo ikishapatikana kwa wingi, kutakuwa na watoaji wa chanjo maelfu kadhaa.
Mnamo tarehe 13 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Pfizer-Biotech ili kuzuia COVID-19.
Mnamo tarehe 20 Disemba 2020, ACIP ilitoa mapendekezo ya matumizi ya chanjo ya COVID-19 ya Moderna ili kuzuia COVID-19.
Ukosefu wa fedha za kulipa, hali ya uhamiaji, au ukosefu wa bima havitakuzuia kupata chanjo dhidi ya COVID-19
Dozi za chanjo zitatolewa kwa watu bila malipo bila kujali hali ya uhamiaji au ikiwa wana bima au la. Watoaji wa chanjo wanaweza kutoza ada za usimamizi wa kutoa chanjo. Watoaji wa chanjo wanaweza kulipwa ada hii na kampuni ya bima ya umma au ya binafsi ya anayepokea chanjo.
Baada ya chanjo ya COVID-19, unaweza kupatwa na athari za kawaida. Hii ni ishara kwamba mwili wako unajenga kinga
Athari ni dalili kwamba chanjo inafanya kazi, athari zinaweza kuwa kama homa na zinaweza hata kuathiri uwezo wako wa kufanya shughuli za kila siku, lakini zinapaswa kuondoka baada ya siku chache.
Kama Mwananchi, upi mtizamo wako juu ya Chanjo ya Corona na njia zinazotumika kupambana na Covid - 19 hapa nchini Tanzania?
Pia, soma:
1). Mtazamo, Maoni, Ushauri na Mapendekezo kwa Serikali na Wananchi kuhusu Ugonjwa wa Corona - COVID-19
2). Coronavirus: Fahamu kiundani kuhusu Virusi hivi | Usambaaji, Dalili na Kinga
Haya lete ripoti kama sio kilaza.Ha haa! believe me mimi siyo kilaza hata kidogo. Siye yule anayesema mRNA inakwenda kubadilisha DNA.
Tangu Serikali iruhusu chanjo ya Corona kuingizwa nchini mjadala mkali umezuka kati ya wapinga chanjo hiyo na wale wanaoikubali, hali hii ni tofauti kabisa na mataifa mengine kama majirani zetu Kenya ua Rwanda. Mpaka sasa wapinga chanjo(anti vaxxers) wakiongozwa na jemedari wao Askofu Gwajima wanaongoza katika mtanange huu na hakuna anayeleweka kwa wakubali chanjo kuanzia January, Kigwangalla mpaka Mbowe n.k.
Kwa kuangalia nyuzi,video, mijadala na michango katika mitandao ya kijamii kuanzia hapa JF na kwingineko, kwa kuwasikiliza watu wengi ninaowafamu (wengi wao wakiwa wasomi wazuri kabisa na washika dini) wapinga chanjo na wakosoaji wake ni wengi kuliko wanaoikubali.
Wapinga chanjo(anti vaxxers) wana hoja na maswali mengi yanayodhihirisha ujinga, upumbavu na uduni wa fikra katika idadi kubwa ya raia nchini(majority).
Zaidi sana wana ujasiri na nguvu kama Simba wa kusimamia ujinga uliowajaa tofauti na wenzao. Hakuna namna ya kuwashauri kuhusu umuhimu wa chanjo, mnaofanya hivyo mnapoteza nguvu na muda wenu tu.
Hali hii inadhihirisha kiwango kikubwa sana cha ujinga katika taifa letu na inamaanisha hata wanaopigania mabadiliko mengine makubwa na muhimu katika nchi hii haitakuwa rahisi kwao kufanikiwa.
Huo ndo uhalisia na ukweli mchungu wa kusikitisha kuhusu taifa hili.Kati ya wale maadui wakubwa watatu, adui ujinga ameiganda nchi kama ruba na hatoki leo wala kesho.
Maskini Tanzania.
Hizo chanjo sikuwa na utambuziWatakuambia mbona chanjo ya ndui ulikubali? na hii kubali tuu
Ni mpumbavu tu ambaye haelewi legacy ya Magufuli. Tuna wapumbavu wengi tu wa aina yako hapa Afrika.
I'm sure wewe huwezi kuingia kwenye kundi la hao wenye akili!!! Sasa kama pamoja na kutokuwa na ubavu wa kuingia kwenye kundi la wenye akili, bila shaka utakuwa umepata jibu anatukuzwa na watu gani!!!Ila kwa wenye akili ndo utakuta wanamtukuza sana kwa kirefu.
Hapa ndipo unapothibitisha ujuha wako manake katika posts zangu hakuna hata sehemu moja niliyoweka habari za media kujibu hoja za kisayansi, na kama papo, onesha!!Soma jarida hili (link hiyo chini) kuanzia ukurasa wa tisa, sio unajaza kichwa upuuzi wa CNN na BBC.
Halafu hapa ndo ujiite una akili?! Typical Magu Supporter....
Halafu niambie nani mwingine hapa Tanzania (ukiondoa Nyerere) amepata hadhi hiyo ya kupigiwa saluti na Afrika.
Kama ulikuwa hujui ripoti za utafiti wa kitaaluma huwa zinawekwa mtandaoni.
Kwa hiyo usiwe na akili fupi ukadhani ni vitu vya siri.
Kwa hiyo niliyemuuliza swali alete link tu kwamba ripoti ni hii.
Ila kiufupi hakuna utafiti wowote uliofanyika na hao wanaoitwa "wataalam" wetu.
Ni kwamba wamepewa tu maelekezo na wazungu kwamba habari ni hii.
Wewe ni JUHA tu!!Kama ulikuwa hujui ripoti za utafiti wa kitaaluma huwa zinawekwa mtandaoni.
Kwa hiyo usiwe na akili fupi ukadhani ni vitu vya siri.
Kwa hiyo niliyemuuliza swali alete link tu kwamba ripoti ni hii.
Ila kiufupi hakuna utafiti wowote uliofanyika na hao wanaoitwa "wataalam" wetu.
Ni kwamba wamepewa tu maelekezo na wazungu kwamba habari ni hii.
Wewe usiyepinga chanjo tupe sababu zako.
Wewe ni mpumbavu wa kwanza kabisa. Hebu usiniwekee zogo hapa sina muda wa kupoteza kwa wapumbavu wasiojelewa.Wewe ni JUHA tu!!
Weka hapa Ripoti ya Kitaalamu iliyoifanywa na Watafiti wetu kuhusu chanjo za surua, ndui, polio, na zinginezo!!!
Ulivyo mpumbavu unasahau kwamba chanjo zote zinazotumika nchi hii, huku zingine wewe mwenyewe na ukoo wako mkiwa mmezitumia, zote hizo zinatoka kwa Wazungu halafu hapa unakuja na porojo zenu za Kijuha eti Wazungu wanawaletea chanjo ili kuwamaliza... ni ujinga ulioje!!!
Hivi wewe na ukoo wako wote mna kipi cha maana cha kuwafanya wazungu wawatengenezee chanjo za kutaka kuwadhuru?
Kwamba eti wamepewa tu maelekezo na Wazungu ni ujuha mwingine!! Yaani unataka kuaminisha watu kwamba Wataalamu wetu ni bora kuliko wataalamu wa WHO walioidhinisha hizi chanjo!!!
Wewe ni Juha unapojaribu kuonesha Chanjo zilizoidhinishwa na WHO haziwezi kuwa salama kwa sababu tu Magufuli na Gwajima wamesema hivyo, kwa sababu kila nikikuambia weka hapa credible source inayo-support madai yenu ya kiwehu, bado umeshindwa kufanya hivyo zaidi ya kuweka vipeperushi vya kuokoteza online!!!
Huyo Gwajima na Magufuli waliwahi kuifanyia utafiti hiyo chanjo na kutoa majibu ya kisayansi mnayoyaimba hivi sasa?
Wewe ni mpumbavu wa kwanza kabisa. Hebu usiniwekee zogo hapa sina muda wa kupoteza kwa wapumbavu wasiojelewa.
Kwa hiyo hoja yako ni ya mazoea.Nimechomwa chanjo za mabeberu tangu nikiwa mwaka 0