Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Chato: Yaliyojiri Mapokezi ya mgombea Urais wa JMT kupitia CHADEMA, Tundu Lissu

Leo hao Interahamwe walioandaliwa na Gwajima tuwaone ,tunajua Gwajima kapewa kugombea ubunge kwa kazi yake yenye ushahidi kila mahali kuwa anaongoza kundi la msituni la kikabila eti lenye lengo la kumlinda Magufuli , as if TISS na Vyombo vimeshindwa ....na tunajua kuwa leo wanataka kufanya vurugu kubwa sana .......kwenye demokrasia hakuna jambo la ajabu ...Dr Slaa alifanya kampeni hadi kijijini Msoga na alimuweka kwenye hot soup Kikwete kwa kuwa na nyumba nzuri huku wanajijiji wenzake wana nyumba za nyasi .....baada ya ule uchaguzi kikwete alijitahidi kuboresha uchumi na nyumba za wanakijiji wanaomzunguka ....
Hadi Lupaso kampeni zilifanyika na Mkapa akachekwa kwa kutokuwa na nyumba ya maana kijijini , AKAJENGA ....HIII NDIO DEMOKRASIA .....wanaotaka wapinzani wasifanye kampeni Chato wanaweka predecence ya ajabu sana ..sio utamaduni wetu huo
Great Sir. big salute...
 
Ndugu yangu sikifichi katika watu wajanja Tundu Lisu ni mmoja wao. Watu wanashupaza shingo kuongea ugoro ugoro akati mjanja Tundu Lisu anafanya utalii wa ndani.
Inakulikana kabisa jeshi la msituni lililoandaliwa base yake iko chato TISS leo ndio siku ya kulilinda taifa ....tusikubali nchi iingie kwenye machafuko kwa ajili ya watu wasio angalia mbele .......
kuna watu walijiapiza kuwa mgombea aendi chato na yeye anajua kura hatapata chato kaenda tu ili kuweka record sawa kuwa hajaogopa kufanya kampeni popote ..
Lakini kama nilivyosema hakuna rais aliyewahi kuzuia siasa ndani ya kijiji chake .....kuna hadi marais ndani ya familia zao waliruhusu demokrasia ya watoto na wajukuu zao kuamini vyama wanavyotaka ...hiyo ndio TANZANIA
 
..TUME YA UCHAGUZI ndiyo imempangia TUNDU LISSU kwa siku ya leo afanye kampeni CHATO.

..Siyo kwamba Lissu amejiamulia tu kibabe kwenda Chato kufanya kampeni.

Ratiba ya TUNDU LISSU inaonyesha ifuatavyo:

October 10 to 11 amepangiwa kuwa Chamwino, Mvumi, Ikungi, Manyoni, Mkalama, Singida .

October 12 amepangiwa kuwa Tabora [Igunga, Nzega] Shinyanga[ Kahama].

October 13 amepangiwa kuwa Geita [ Mbogwe, Bukombe, Chato].

October 14 amepangiwa kuwa Mwanza[ Ukerewe ], Mara [ Rorya ].

October 15 amepangiwa kuwa Simiyu [ Itilima, Meatu, Bariadi ].

October 16 amepangiwa kuwa Tabora [ Tabora, Urambo,Kaliua].

October 17 amepangiwa kuwa Singida[ Manyoni], Dodoma [ Bahi, Kongwa, Dodoma ].

Ratiba ya SALUM MWALIMU inaonyesha kati ya October 10 to 17th atakuwa maeneo ya Iringa, Mbeya, Songwe, Rukwa, Kigoma, na Kagera.
 
Kuna watu sijawahi ona, uwanja wa Chato uwanja wa Chato, hivi Chato ni wananchi wa wapi? Wao hawana haki ya kuwa na uwanja? Mbona mnakuwa wapumbavu kiasi hiki?

Mnatukana kila siku Chato utafikiri wao hawatakiwi kuwa na uwanja. Kwa taarifa yenu wananchi wa Chato si wajinga, muulizeni mgombea wenu alichokipata Buselesele na Katoro hadi akasitisha kwenda Chato, haya yote ni siasa mbovu isiyo na staha, hata kama unachallenge tumia lugha rafiki, don't be so biased to that extent, watu wa Chato amewatukana sana, Buselesele na Katoro yalikuwa maeneo ya upinzani lakini kutokana na dharau za Lissu matokeo yake CHADEMA leo inazomewa, Lissu asingezomewa Buselesele kwa namna ile, Awe na akiba ya maneno kwani anaowatukana wanasikia .

Inashangaza sana unatukana halafu bado eti unaenda kuwaomba kura,,,,, unatukana barabara kujengwa huku unazitumia, unatukana ndege huku unazipanda huo ni U CHICHIDODO.

Hopeless kabisa , let's stay tuned leo.

Unaongea ujinga gani mbona hizi flyover zinajengwa Dar siyo huko mikoani, pesa ya umma inatakiwa kutumika kwa malengo ya kuleta unafuu katika maisha sasa kuna abiria gani huko kijijini mbona hakuna mwaka watanzania wamewahi kulalamikia ujenzi wa miundo mbinu. Ni kosa kubwa sana kuamuwa kujenga uwanja chato si kutokana mahitaji lakini kwakuwa Rais anatoka hapo.

Tangu uwanja umekamilika hakuna ndege zinakwenda huko pamoja na kwamba ATCL ina Ndege mpya kabisa. Sasa uwekezaji wa hivo una tofauti gani ule ewekezaji wa mabuto kule kijijini kwake akiwa Rais was Congo
 
Unatembeleaje uwanja unaouponda kila siku? Aende akatembelee na traffic lights
Inafikiri anaenda kutembelea kwa kufurahia huo uwanja
Yeye mwenyewe hatumii hoja na anatumia lugha za kuudhi, kebehi dharau na uongo uliosheheni matusi ya reja reja, iweje yeye ajibiwe kwa hoja?? Mfano jana anatukana mabango ya mgombea mwenzake, nani kamzuia kuweka yake? Lissu anapanda jukwaani badala ya kunadi plan na sera za chadema anaanzisha ajenda za "Yatokanayo kwenye mikutano ya mwenzake'" na kuanza kumshambulia badala ya kuja na ilani ya chama chake, amekua ana ugomvi binafsi moyoni na Mhe Magufuli, kutwa kucha yuko mdomoni kwake,i ni wapi Magufuli alimshambulia personally? Lissu ni mbwa tu
Umesahau 2015 mlivyokuwa mnamshambulia Lowassa kwa matusi na kumdhalilisha?

Isitoshe, Lissu hamtukani bali anaelezea mapungufu/makosa yake kama kiongozi.
 
Jamaa yangu yuko Chato anasema CCM inawalazimisha Wananchi wafanye vurugu nami na kikosi changu hapa Geita tunaelekea Chato kwenda kumlinda #NI YEYE
 
Nahisi watamzuia kutembelea huo uwanja.Na kwakuwa huko ni nyumbani kwa mgombea yule,nina wasiwasi pia anaweza fanyiwa hujuma katika kampeni zake huko lengo kuhakikisha hapati watu au ashindwe kuhutubia.

Ni imani yangu Lissu haendi kufurahia uwanja,bali anaenda kufanya tathimini physically ya huo uwanja kwa kuingilia kilichojengwa (kupata picha ya kilichojengwa) na ulazima wake pamoja na umuhimu wa kujenga uwanja katika eneo hilo.

Ushauri:Tundu Lissu vaa helmet muda wote ukiwa huko Chato na kuwaambia wananchi kila mtu awe mlinzi kwa kumtupia macho alie jirani yake katika mikutano na misafari atayofanya huko Chato(kwenye msafara wa mamba, hata kenge wamo).

Nasema hivi kwasababu,teyari dalili zinaonyesha kuwa lolote linaweza kutokea leo hii, hivyo ni bora kuchukua tahadhari zote zinazowezekana kuchukuliwa.
Lissu ni noma
 
Jamaa yangu yuko Chato anasema CCM inawalazimisha Wananchi wafanye vurugu nami na kikosi changu hapa Geita tunaelekea Chato kwenda kumlinda #NI YEYE

Lissu awe makini sana huko ikiwezekana asipite
 
Back
Top Bottom