China kuipatia silaha Russia dhidi ya Ukraine

Faida sie tunaiona ,,nyie kwa mahaba yenu na nyie mnaona yenu...........upepo ulivyokua miaka 2 nyuma ni tofauti na sasa,,,,,,China hawezi akaenda kichwakichwa ila lengo lange linaeleweka,,,, hadi kumsumbua mmarekani kiuchumi pia hakwenda kichwa kichwa kama ingekua hivyo wangeshamminya mapema kabla hata hajafikia level za kuwasumbua......mambo bado aisee kuna kama miaka 7 -10 mbele......
 
Kama nchi za Magharibi zimeamuwa kupigana vita ya mawakala na Urusi kupitia Ukraine basi washirika wa Urusi wana haki ya kumsaidia mshirika wao.
Pole. Tusubirie china ijichanganye mifumo Yao ifungwe duniani na walivyotawanyika sijui wataishi vipi
 
Sasa si wajitokeze wazi kumsaidia?!!kama nchi za ulaya zinavyofanya?!!wanaogopa nini?
Huo ni mtizamo wenu na hio ni jadi ya wamagharibi kuonyesha kila wafanyacho aidha kwa kujaza watu hofu au kupitisha propaganda za uongo ,,,,watu wanakimbiza mwizi kimyakimya kwa sasa japo ujumbe unasomeka huu upande mwingine hawataki kujijenga kama walivyojijenga wamagharibi kwa showoff za kijinga na ubabe wa kigoroko
 
Mkuu hizo faida unazoziona wewe na putin tu ni zipi?!!china hawezi kuwa superpower kwa miongo hii ya karibuni,
 
Nyie si mlilipasua lile puto lao angani sasa subirini na wao wafanye yao msiwaingilie na msiwapangie cha kufanya kila nchi Ina maamuzi binafsi
 
Ni Sawa tu,
Bado KK nayo itaipa Urusi silaha,Iran tayari.
Hii maana yake Kila mtu na maswahiba wake.
N ndivyo hata NATO wakiingiza majeshi kamili nao wachina watatia timu uwanjani,bila kumsahau kiduku na marafiki wengine.
Patamu sana hapo... Ngoja tusubiri inyeshe tuone panapovuja
 
Mkuu hizo faida unazoziona wewe na putin tu ni zipi?!!china hawezi kuwa superpower kwa miongo hii ya karibuni,
Na hawajasema wanataka kua superpower shida mnaenda na akili za kimagharibi,,hao hawataki kua superpower na kuonyesha mabavu kwa wengine, wao lengo lao kila mtu awe huru na mambo yake, na ndo inapokuja hio multipolar world, hawatafuti u superpower kama akili za wamagharibi zinavyofikiria,,,,hao wanachotaka kila nchi iheshimu mipaka ya wenzie na nchi zisiingilie maamuzi ya wengine,,, na hilo ndo wanalolipika huko brics na kwenye miungani yao mengine , ndo maana mrusi au mchina haitaji resource nyingi kua superpower kwasababu hilo sio lengo lao , lengo watu waheshimiane baaas.............hizi mambo za usuper power ni ideology za kimagharibi
 
Huo sio uchawi!!unadhania kuwa taifa kubwa duniani,kiuchumi na kisiasa utaweza kwa kuwa eti kimya kimya?!?Mfano china ki uchumi yupo juu ila nguvu ya kisiasa duniani hana!! Huyo putin sasa ndio anatafuta ushawishi wa kisiasa huko W.Africa.
Propaganda?!!lnenda baharini huko ndipo utaona kweli kumbe hii dunia bila USA kuweka ulinzi sijui ingekuwaje!??
 
Ndo nachokwambia hao hawatafuti wanachokitafuta wamagharibi,,,,,wamashariki wana ideology tofauti kabisa,,,wangekua wanataka hayo hadi sasa na wao wangeanza kupeleka upepo kwenye sarafu zao, mchina angekua ana force yuan na mrusi rubble, ila hawa wanachokipambania kinaonekana ,kila nchi ifanye biashara kwa sarafu yake., kitu ambacho mabepari wakimagharibi hawataki sababu wanajua wanavyoinyonya dunia na sarafu zao,, huku Africa ni muda tu na kuna nchi zinaonyesha muamko taratibu ,,,,,hao jamaa hawana haja ya kupiga kelele sababu lengo lao ni tofauti na wamagharibi,,,........wamagharibi ndo waliowekeza sana kwenye propaganda tena zile hasi na vyombo vyao, ....narudia tena mrusi na mchina hawautafuti usuper power wao wanachotafuta ni uhuru wa kufanya mambo yao bila kuingiliwa bas,,huku magharibi wanasaka na kutaka ku maintain usuper power ili waingilie nchi nyingine na kuzipelekesha watakavyo
 
Sasa hiyo bricks nayo ina impact gani toka iundwe?!!lazima dunia iwe na kilanja mkuu wa kuweka mambo sawa!!hao china,urusi,iran,n.korea wao kitu demokrasia na uhuru wa watu kwao sio kipaumbele.kwakuwa UN imeshindwa kufanya majukumu yake ipasavyo ndio maana US anakuwa ndio kama UN!!Na hii dunia kama putin ndio angekuwa kilanja wa dunia kusingekuwa kuwa na dunia tena
 
Toka iundwe imefanya nini hadi sasa? Ina memba wangapi?? Ndo kwanza inafufuka we unataka ikuonyeshe lipi la ajabu.....hio UN yenyewe hadi kupata nguvu si hadi watu waliposhikishana adabu kwani waliamka tu leo UN ikawa na nguvu,,,,,,,,kikubwa wanaonyesha njia na wanachokipigania kinaonekana tena bora kwa miaka hii kuliko huko nyuma ndo ilikua giza kabisa.....leo Mali anaweza mkoromea mfaransa kisa urusi je miaka 5 nyuma huko aliweza??? Nchi za afrika kwa sasa zinaweza kupelekana puta na wamagharibi sababu wanajua option nyingine zipo.......mambo taraatiiiiibu yente yente......... ....nyie bakini na usuper power wa dunia yenu tu hata mkiwa nchi 20 na superpower wenu fresh hamna atakaewaingilia na mambo yenu, kikubwa msifosi mambo yenu kwa wengine
 
Huo umoja wao BRICS sasa ni miaka 22 toka wauunde kuna nini wamekifanya ili kujinusuru na hali hiyo?!!kwani wengi waliamini kuwa huo umoja ndio mwisho wa ubabe wa magharibi?sio jambo rahisi hivyo kusema kuwa eti dolar isitumike kwenye biashara za kimataifa?!!huyo mrusi wakati vita inaanza akatoa amri watumiaji wote wa gesi yake walipe kwa rubble,nchi za ulaya zikalataa alifanya nini?
 
Nchi za ulaya bado zinachukua gesi ya mrusi?? Na kawabembeleza??hadi bwana yao akaamua kulipua bomba kwani mrusi alijikomba kwao............ndo hivyo watu wanapiga biashara sasa bila hata ya dola national currency kwa national currency mambo yanaenda......brics miaka 22 ina member wangapi??? Na hao waliopo umeona wanapelekeshwa na ushoga wa wamagharibi?
 
Population ya china, india na Brazil ni robo tatu ya dunia na ndiko huko Russia anafanya biashara
Wewe mwehu kumbe hauna hata akili. Ukubwa WA soko sio Population. Ingelikuwa hivyo basi Tanzania Ingelikuwa na soko kubwa (Watu 61M) kuliko Israel (watu 7M). Licha ya India kuwa na watu 1300M lakini zaidi ya watu 900M ni makapuku ambao hawamdu milo 3 kwa siku. Sasa wewe hiyo biashara ya Urusi inayokwenda India anagawa Bure au?
 

Madhara ni kwamba baraza la kudumu la usalama la Umoja wa Mataifa litagawanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…