Unaandika porojo sizizo za maana nimekuleta andiko
Hivi kila mtu akilazimisha hoja pinzani isomeke kama tu ^porojo zisizo na maana,^ utakuwepo umantiki wowote wa kuendelea kujadiliana?
Umesema umeniletea andiko. Nami nimekujibu kwa mifano dhahiri takriban kumi itokanayo na maandiko. Hapo porojo iko wapi?
Au pengine hujaelewa? Rudia kusoma tena, na pia unaweza kuomba ufafanuzi wa ziada.
kwa hiyo Mgonjwa akiombewa na ukisamehewa dhambi zake ikatokea kafariki anarudishiwa dhambi zake??
Kwa sababu aliombewa akiwa mgonjwa na akafariki??
1. Una hakika gani kwamba waliokuwa wakimwombea mgonjwa walikuwa na ^imani^ anayoitamka Yakobo kwamba ni kigezo cha msingi sana ili kumwokoa na kumwinua mgonjwa husika?
2. Unathibitishaje kwamba alisamehewa dhambi zake?
3. Je, unaamini kwamba kila ombi linaleta matokeo ambayo mwombaji anatarajia?
4. Kwa mantiki hiyo, rejea kwenye maswali yangu yaliyopita (#411), unipatie majibu yake kwa kuzingatia mtazamo wa wazo hili hapa kwenye swali la 3.
Mathalani, mfano mmojawapo, Mfalme Daudi alifunga siku 7 akimwombea mwanawe aponywe, lakini akafa (2 Sam. 12:15-23).
Hapa ni wazi kabisa alitarajia jambo moja, ila likatokea lingine kinyume kabisa na dua yake.
Ikiwa na maana kwamba mapenzi ya Mungu yalitimia katika kifo cha mwanawe. Na Daudi alitambua hilo.
Ndiyo maana wakati wa kuomba, Kristu amefundisha tuseme: ^Mapenzi Yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni.^
Alipokuwa anakaribia kusulubiwa, aliomba:
^Ee Baba, ikiwa ni mapenzi Yako, niondolee kikombe hiki; walakini si mapenzi Yangu, bali Yako yatendeke.^ Luka 22:42.
Maneno ya Mfalme Daudi, baada kufiwa mwanawe, yanatusaidia kuelewa wazo hilihili kwamba hata pale tunapoomba, tukitarajia majibu fulani ya maombi yetu, tunapaswa kuomba ili mapenzi ya Mungu daima ndiyo yatendeke.
Mfalme Daudi alipoulizwa kwa nini alifunga na kumlilia Mungu kwa ajili ya mwanawe, lakini baada ya kufariki, mfalme akainuka na kujipaka mafuta na kubadili mavazi yake na kumwabudu Mungu kana kwamba haukuwepo msiba wowote uliokuwa umetokea, alisema:
^Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia; kwa maana nalisema, Nani ajuaye kwamba Bwana
atanihurumia, mtoto apate kuishi?^ (2 Sam. 12:22).
Iwapo mtoto alikufa, unadhani Mfalme Daudi aliipata hiyo
huruma kwa namna aliyokuwa akiitarajia???
Maana yake nini? Ni kwamba Mfalme Daudi alitambua kuna mapenzi ya Mungu yaliyo juu kabisa ya utashi wa mwanadamu.
Ndiposa, nakuuliza swali la msingi: Je, unatambua mapenzi ya Mungu kuhusu lile tukio la Machi 17?
Umekiri kwamba mtu anaweza kufariki, japo ameombewa na kupakwa mafuta ya kiroho.
Hilo sina mashaka nalo. Nakubali 100% kwa sababu Mungu ameruhusu iwe hivyo; ni mapenzi Yake.
Nami, kwa mantiki hiyohiyo, nakuuliza, Hivi kila anayeombewa na kupakwa mafuta wakati wa umauti, anakuwa mrithi wa ufalme wa mbinguni?
Kwa nini tusiruhusu na hapa pia mapenzi ya Mungu yatimizwe?
Kwamba ikitokea ile siku ya mwisho ya kiama mpendwa wetu fulani hajawepo mbinguni (Mungu aepushie mbali), tutamlalamikia Mungu tukimhoji kwa nini hayupo peponi wakati tulimwombea na kumtia mafuta ya upako wakati wa umauti wake???
This is crazy!
Mapenzi ya Mungu yatimizwe daima hapa duniani na huko juu mbinguni!
Hekima Yake ni kuu kuliko ya mwanadamu, kama ambavyo mbingu iko juu kuliko dunia!
Suala la nani ataokolewa au nani atahukumiwa, si jukumu la mwanadamu hata kidogo!!!
Naomba niletee andiko linalosema kuombewa kwa mgonjwa mahututi ni jambo moja. Kuokolewa hatimaye katika ufalme wa Mungu siku ya mwisho ya Kiama, ni jambo lingine tofauti kabisa!
Kama nilivyofafanua hapo juu, hivi unaweza kunithibitishia kwamba kila mgonjwa anayeombewa na kutiwa mafuta ya upako, basi hapo amepata tiketi ya kwenda mbinguni?
Namaanisha kwamba kama tunaweza kumwombea mgonjwa apone na kumtia mafuta ya upako lakini akafa, kwa nini matokeo kama hayo yasitarajiwe pia kuhusu kuurithi ufalme wa mbinguni—kwamba unaweza kuomba aokolewe, mgonjwa akafanyiwa upako, mwisho wa siku akapotea milele?
Au matokeo yanayokuja tofauti na matarajio ya maombi na upako yanahusiana na kupona maradhi ya kimwili tu, ila linapokuja suala la kuurithi uzima wa milele, basi kila aliyefariki kwa jinsi hiyo huwa mrithi wa Ufalme wa Mungu?