Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Chozi la Jenerali Mabeyo akisimulia siku za mwisho za Hayati Magufuli linaashiria nini?

Tuambie wewe nani alipaswa kuwa Mkuu wa Majeshi? Maana Mabeyo wakati JPM anaingia tayari alikuwa ni moja ya makamanda wa ngazi ya juu kabisa jeshini wala si kwa kubebwa na Magufuli!

..Mabeyo aliteuliwa wakati ameshavuka umri wa kustaafu.

..Jiwe alikuwa hafuati sheria na taratibu. Mfano mwingine ni jinsi alivyomteua Dr.Bashiru kuwa Kmk.
 
..Davis Mwamunyange kazaliwa 1959.

..Venance Mabeyo kazaliwa 1956.

..Mwamunyange alipostaafu Jiwe akamteua Mabeyo.

..Sasa hamuoni kuna tatizo hapo?

Cc Nguruvi3, sambulugu

Mkuu haiwezekani 1959 kuwa ndio mwaka aliozaliwa jenerali mstaafu Davis adolf Mwamunyange, Mwamunyange amepewa nyota yake ya kwanza JWTZ mwaka 1973 batch moja na luteni jenerali Abdurahaman Amir Shimbo

Abdurahman Amir Shimbo na Davis Adolf Mwamunyange wameingia kwa pamoja vyote viwili yaani mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS) na uafisa kadeti (ni coursemates kwenye kuingia kwenye uaskari pamoja na uafisa)
 
Hii ni ishara nchi hii watu wanaongoza Kwa makundi na siyo frame of operations, hali hii inapswa kurekebisha. Ni kama vile tunaishi Kwa hisani za watu. Katiba ndiyo source ya haya yote kwakua at some point inalimbikiza Madaraka Kwa individuals badala ya kuyaweka Kwa public
Binafsi hii imenishangaza baada ya kusikiliza mahojiano
Baada ya mheshimiwa kufariki ni kama kulikuwa na sintofahamu ya nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani
Rais wa marekani alipo uwawa tu masaa machache makamu aliapishwa tena ndani ya ndege
 
Jamaa ameongea mengi, mengine angebaki nayo tu..

Hii inaonyesha wale wapumbavu wote waliosimama majukwaani wakisema "raisi yuko vizuri na anaendelea na majukumu yake" hawajui chochote na ni makapuku tu kama sisi wananchi...Yani kumbe nchi Ina kama ka-kamati Cha watu wanaopanga Mambo yaendaje??
 
Marekani wamekufa Marais wanne wakiwa madarakani,Wana experience kidogo..

Ila walivyoona raisi anaumwa tu ilibidi waanze kuchukua hatua
 
Mkuu haiwezekani 1959 kuwa ndio mwaka aliozaliwa jenerali mstaafu Davis adolf Mwamunyange, Mwamunyange amepewa nyota yake ya kwanza JWTZ mwaka 1973 batch moja na luteni jenerali Abdurahaman Amir Shimbo

Abdurahman Amir Shimbo na Davis Adolf Mwamunyange wameingia kwa pamoja vyote viwili yaani mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS) na uafisa kadeti (ni coursemates kwenye kuingia kwenye uaskari pamoja na uafisa)

..Cdf na CoS wanastaafu wakiwa na miaka 60.

..kwa hiyo bado Mabeyo aliteuliwa akiwa ameshapitisha umri.
 
Binafsi hii imenishangaza baada ya kusikiliza mahojiano
Baada ya mheshimiwa kufariki ni kama kulikuwa na sintofahamu ya nini kinatakiwa kifanyike na kwa wakati gani
Rais wa marekani alipo uwawa tu masaa machache makamu aliapishwa tena ndani ya ndege
Kwa Tanzania, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Rais kufia madarakani.

Kwa Marekani, ni marais 8 ambao wamefia wakiwa madarakani.

Marekani wana uzoefu juu ya hilo. Tanzania tumeupata uzoefu huo miaka 3 tu iliyopita.

Tujipe nafasi ya kujifunza kuhusu matukio kama hayo.
 
Kweli….si umemsikia hata Jenerali Mabeyo kasema kuwa Rais Magufuli alimwambia [CDF] awaamuru madaktari wamrudishe nyumbani lakini akasema hana mamlaka hayo.

Magufuli akashangaa kwa nini CDF hawezi kuwaamuru hao madaktari wamrudishe nyumbani. Jenerali akasema hilo ni suala la madaktari na siyo CDF.

Magufuli alikuwa anadhani kwa vile Mabeyo ni CDF, basi anaweza kutoa amri kwa yeyote yule na ikatekelezwa.

Kwa kuangalia tu juu juu, Mabeyo anaonekana kama ni mtu mwenye sense.

At least that’s how he came across in the interview.
Msaada Mr Nyani, hakuna namna ya kuweza kuitoa hiyo video kwenye youtube format?
 
Jamaa ameongea mengi, mengine angebaki nayo tu..

Hii inaonyesha wale wapumbavu wote waliosimama majukwaani wakisema "raisi yuko vizuri na anaendelea na majukumu yake" hawajui chochote na ni makapuku tu kama sisi wananchi...Yani kumbe nchi Ina kama ka-kamati Cha watu wanaopanga Mambo yaendaje??
Sio kwa kiwango unachotaka kufikiria kiongozi
Hali ya rais ilikuwa inajulikana kwa viongozi wa juu ila wakati kifo chake kinatokea wengine hawakuwepo eneo la tukio
 
Ya kutambua:

1. Jenerali Mabeyo ni mzalendo kweli kweli asiyekuwa na chembe ya tamaa ya madaraka.

2. Hapo #1 watu kama hawa ni wa kupigiwa mfano.

3. Kuna watu walionekana kuwa walisahau katiba inasema je, ndiyo maana ikachukua siku mbili tatu hadi kuapishwa badala ya masaa 24 kutokea rais kufariki.

4. Kuwa rais alijua atafariki kiasi cha kumhitaji paroko, kadinali na hata kutaka kurudishwa nyumbani akafie kwao.

5. Kumbe ma Profesa wanaotushauri makulaji walikuwa pale? Ama kweli safari ya pagak ikifika (song of lawino) no way back.

6. Aliyepo anashaurika japo kuna wanao mshauri vibaya lakini baadaye wanakaa wanayaweka mambo sawa.

7. Kwamba, hapa mkuu wasemaje? Kuna hawa wamesema hivi ..:

".. kwani waliosema hivyo ni wanajeshi, raia au wanasiasa ...?"

Pamoja na kustaafu, Jenerali Mabeyo bado ni hazina kubwa kwa taifa hili.
No 5 nimekuelewa saanaaaa yaani Dah
 
Kama umesikiliza mwishoni ile ni diplomatic language tu kwa nafasi lazima awe responsible kwenye kauli zake kutoingilia siasa zinazoendelea.

Lakini body language ndio kila kitu hasa akielezea siku za mwisho ilivyokuwa hadi mauti yanamkuta marehemu.

Itakuwa kuna kitu kinamuumiza mpaka leo yale malengelenge ya machozi sio bure na kushindwa kuzuia emotions zake ata kwenye kuongea kwa majonzi ile siÄ™ tabia ya army general kushindwa kujizuia. Kwa nafasi yake mtu kama yeye kwa kwa nilichokiona ni big deal kiaskari duniani.
Wewe nae hujawahi kulia? Kulia ni kawaida
 
Mkuu haiwezekani 1959 kuwa ndio mwaka aliozaliwa jenerali mstaafu Davis adolf Mwamunyange, Mwamunyange amepewa nyota yake ya kwanza JWTZ mwaka 1973 batch moja na luteni jenerali Abdurahaman Amir Shimbo

Abdurahman Amir Shimbo na Davis Adolf Mwamunyange wameingia kwa pamoja vyote viwili yaani mafunzo ya awali ya kijeshi (RTS) na uafisa kadeti (ni coursemates kwenye kuingia kwenye uaskari pamoja na uafisa)

..Mwamunyange ilikuwa aastaafu mwaka 2016 maana yake huo ndio mwaka aliotimiza miaka 60. Hivyo basi ni sahihi kusema Mwamunyange alizaliwa mwaka 1956.

..Taarifa za kwenye mitandao zinasema Mabeyo amezaliwa mwaka 1956. Yaani mwaka mmoja na Mwamunyange.

..Hoja yangu bado inasimama kwamba kulikuwa na walakini ktk uteuzi wa Mabeyo.
 
Back
Top Bottom